Monday, April 18, 2016

SIMU TV: HABARI KUTOKA VITUO VYA TELEVISHENI

Jeshi la polisi kanda maalum ya Dar es salaam lafanikiwa kumtia mbaroni jambazi sugu akiwa na silaha mbili huku moja ya silaha hizo ikiwa imefichwa kwa rafiki yake wa kike.https://youtu.be/CQpi9eWwGOY
 Baadhi ya miundombinu ya mabomba ya kusafirishia maji visiwani Zanzibar yaharibiwa vibya na mvua zinazoendelea kunyesha visiwani humo. https://youtu.be/43S8ABP6mhs
 Mvua kubwa zinazoendelea kunyesha visiwani Zanzibar zawasababishia athari kubwa wananchi baada ya makazi yao kufurika kwa maji. https://youtu.be/drbmcsM-Tww
 Shirika la kazi duniani ILO kwa kushirikiana na baraza la taifa la uwezeshaji wananchi kiuchumi waandaa mpango mkakati wa kukabiliana na tatizo la ajira kwa vijana nchini.https://youtu.be/PntHjgIr7RI
 Baadhi ya wananchi jijini Dar es salaam watoa maoni tofauti na mtazamo wao juu ya sura na namna jinsi bunge lijalo litakavyokuwa. https://youtu.be/uvV4XDcNZms
 Baadhi ya ombaomba waelezwa kutii agizo la mkuu wa mkoa wa Dar es salaam kwa kuondoka katika maeneo mengi ambayo wamekuwa wakionekana. https://youtu.be/NeXPravhhE4
 Katibu mkuu wa Jumuiya wazazi ya CCM taifa aitaka jumuiya hiyo kuvunja makundi yaliyojitokeza ndani ya chama hicho kipindi cha uchaguzi ili washirikine katika kukijenga chama na kujiandaa na chaguzi zijazo. https://youtu.be/ekU1VnuB9_4
 Jinamizi laendelea kuiandama klabu ya Barcelona kufuatia matokeo mbaya mfululizo baada ya hapo jana kutumbuliwa goli 2 kwa 1 na Valencia. https://youtu.be/qPTMpJ4Zth4
 Wakazi wa kijiji cha makao wameuomba uongozi wa kijiji hicho kufuta tofauti zilizopo kati yao na mwekezaji wa kampuni ya uwindaji ya mwiba. https://youtu.be/ZvP3wFwcGu0
 Wahamiaji wapatao mia nne kutoka Somalia wanahofiwa kuzama katika bahari ya mediterania walipokuwa wakisafiri kuelekea Ulaya https://youtu.be/v6ELKxzl198
 Uongozi wa mkoa wa Tabora wamewaombea kupunguziwa adhabu viongozi wao waliofungiwa maisha na TFF kujihusisha na mpira. https://youtu.be/mefvfcrZBbM
 Serikali inategemea kuanzisha kampuni itakayokua ikisimamia na kuboresha viwanja vyote vya michezo vinavyomilikiwa na CCM. https://youtu.be/-QWFkbJb97k
 Mshambuliaji shiza kichuya wa Mtibwa Sugar amechaguliwa kuwa mchezaji bora wa mwezi machi katika ligi kuu ya Vodacom. https://youtu.be/CkyzRurBbhE
 Jeshi la kujenga taifa JKT limetakiwa kuanzisha somo la ujasiriamali kwa vijana wanaojiunga na jeshi hilo ili kuwawezesha kupata stadi na ujuzi wa kujitegemea https://youtu.be/nR6qPPxSO5M
 Kocha wa Azam amesema ushindi kwenye mechi yao ya marudiano dhidi ya experianse ya Tunisia ni muhimu ili waweze kusonga mbele kwenye michuano hiyo https://youtu.be/ASAlWz5pNkA
 Viongozi wa vilabu vya michezo mkoani Iringa wameshauriwa kujitegemea katika kuendesha vilabu hivyo badala ya kutegemea viongozi wa kisiasa https://youtu.be/lDpnul7ddtM
 Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Paul Mkonda azidi kuwakalia kooni wahusika katika jengo la Machinga Complex; https://youtu.be/fEc5cXiqOMY 
 Shirika la habari Tanzania TBC lajipanga ili kuweza kuwafikia wananchi wote walio mijini na pembezoni mwa miji; https://youtu.be/9ki1pH23Up0
 Wafanyakazi wa kiwanda cha Maturubai na Mifuko huko mkoani Tanga wagoma kwa siku nne wakishinikiza kuongezewa mishahara; https://youtu.be/828MV29EYrM
 Naibu Spika wa Bunge Ackson Tulia aridhishwa na mfumo mpya wa bunge wa urushaji matangazo pamoja na ukarabati wa bunge hilo; https://youtu.be/CxVJA7ownBQ
 Makamu wa Rais Mama Samia Suluhu azindua rasmi mbio za mwenge wa uhuru kitaifa huko mkoani Morogoro; https://youtu.be/jMvApZKU9_U
 Rais John Magufuli awateua wakuu wa wilaya wawili akiwemo Humphrey Polepole kujaza nafasi za wilaya ya Kinondoni na Musoma; https://youtu.be/C1_XpxnR6oU
 Mvua zinazoendelea kunyesha hapa nchini zimeleta maafa makubwa huko mkoani Unguja baada ya kaya 50 kuharibiwa; https://youtu.be/UuOtAF-T6OM
 TAKUKURU mkoani Mwanza yamshikilia Afisa Utumishi wa Halmashauri ya Mwanza kwa tuhuma za ubadhilifu wa fedha; https://youtu.be/hDpqqxwbWS8
 Sakata la watumishi hewa lawaponza Mwalimu na Polisi huko wilayani Bukoba mkoani Kagera baada ya kufikishwa mahakamani kujibu tuhuma zinazowakabili ; https://youtu.be/VTfOsDcfZSc
 Mauzo ya hisa katika soko kuu la hisa jijini Dar yaelezwa kupanda kwa asilimia mia moja;https://youtu.be/BZNIFM83Cyw
 Waziri Jenista Mhagama alitaka jeshi la kujenga taifa JKT kuwafundisha vijana wanaojiunga na jeshi hilo masomo ya ujasiliamali ili kuongeza ajira; https://youtu.be/_Fk7N8Sohoc
 Timu za soka za Yanga na Azam zasema ziko tayari kuwakabili waraabu hapo kesho na keshkokutwa; https://youtu.be/K1DD0s0Tees
 Bondia Francis Cheka sasa atafutiwa pambano ili kukipiga na bondia anayekuja juu kwa kasi Dulla Mbabe; https://youtu.be/xMUih58lZE8
 Nae meneja wa bondia maarufu nchini Francis Cheka ndugu Juma Ndembile ajitosa kugombea ukatibu wa soka katika wilaya ya Kinondoni; https://youtu.be/MoXSg2hf7Ls
 Washindi wanne wa Startimes washinda kwenda kuwashuhudia akina Paul Pogba Live;https://youtu.be/vYVsbIsJuZA
 Shule ya Sekondari Makongo wapata msaada wa vifaa vya michezo kujiandaa na mashindano ya Umisseta; https://youtu.be/WIlCEGqyotE

No comments: