Thursday, April 14, 2016

SIMU TV: HABARI KUTOKA TELEVISHENI

SIMU.tv: Takukuru mkoani Mwanza yaitumbua halmashauri ya jiji hilo baada ya kubaini udanganyifu kwenye mawasilisho ya watumishi hewa. https://youtu.be/Uo75veOvtPI  

SIMU.tv: Waziri wa nchi ofisi ya waziri mkuu, sera, bunge, kazi, ajira na walemavu Jenister Mhangama asema asilimia 71 ya watanzania hawana utamaduni wa kufanya kazi zinazochangia pato la taifa. https://youtu.be/WjucsqAzVs0

SIMU.tv: Waziri wa habari, utamaduni, sanaa na michezo Nape Nnauye amesema serikali iko mbioni kuliboresha shirika la utangazaji nchini TBC kwa kulipa uwezo wa kutimiza majukumu yake ya kuhudumia umma kwa ufanisi zaidi.https://youtu.be/7i_MB4-DqwM

SIMU.tv: Rais Dk.John Magufuli atengua uteuzi wa mhariri mtendaji wa magazeti ya serikali TSN Gabriel Nderumaki na kumteua Tuma Abdallah kukaimu nafasi hiyo.https://youtu.be/G_gJ5N4BXbY

SIMU.tv: Mkuu wa mkoa wa Morogoro Dr. Steven Kebwe awasimamisha kazi maafisa 2 wa halmashauri ya Morogoro pamoja na kukamatwa kwa watu 3 wakiwemo raia wawili wa China kwa tuhuma za kuisababishia halmashuri hiyo hasara ya milioni 92 kwa kukwepa kodi. https://youtu.be/PbL2x51po1c

SIMU.tv: Makamo wa Rais Samia Suluhu aiagiza sekta binafsi nchini kujadili na kutoa mapendekezo ya namna itakavyoshiriki kwenye mapendekezo mapya ya maendeleo.https://youtu.be/WTgB-PylYgQ

SIMU.tv: Rais Salva Kiir wa Sudan Kusini anatarajiwa kuwasili nchini hapo kesho kwa ajili ya ziara ya kikazi ya siku moja. https://youtu.be/ztqh3jUCOcw

SIMU.tv: Waziri wa nchi ofisi ya Rais tawala za mikoa na serikali za mitaa TAMISEMI aifuta bodi ya soko ya Machinga Complex pamoja na kuwasimamisha kazi watumishi wanaosimamia soko hilo kwa kushindwa kuwasimamia wafanyabiashara wadogo.https://youtu.be/HzF1CyNwrUA

SIMU.tv: Mvua kubwa zinazonyesha nchini hivi sasa zaleta madhara makubwa baada ya kubomoa nyumba 100 na kuharibu mali mkoani Kilimanjaro.https://youtu.be/ZeQOmbJsLaA

SIMU.tv: Licha ya serikali kutoa tamko la kuifunga shule ya sekondari ya Mt.Peter iliyoko mkoani Tabora baada ya kutokea kwa tukio la moto, uongozi wa shule hiyo wadai shule hiyo haijafungwa na wanafunzi wanaendelea na masomo huku tukio la moto likifanyiwa uchunguzi wa kina. https://youtu.be/uk6PRQ3dyqU

 SIMU.tv: Jeshi la polisi mkoani Shinyanga lafanikiwa kuwaua watu 3 wanaosadikiwa kuwa majambazi katika tukio la mapambano la kuzima tukio la kupora fedha katika duka la mfanyabiashara mmoja mkoani humo. https://youtu.be/Q0S4oUnAlZY

SIMU.tv: Walinzi wawili wa mgodi walioko kitalu B katika mji mdogo wa Mererani wajeruhiwa kwa kupigwa na risasi na mmiliki wa mgodi ulioko jirani na mgodi huo baada ya wafanyakazi wa migodi hiyo miwili kutobozana chini ya ardhi wakati wakichimba madini ya Tanzanite. https://youtu.be/ve84q9OOd3Q
  
 SIMU.tv: Mahakama ya hakimu mkazi Kisutu yamuachia huru aliyekuwa mkurugenzi mtendaji wa shirika la umeme nchini TANESCO na wenzake 4 waliokuwa wakikabiliwa na mashitaka 6. https://youtu.be/kbn_JIAy6HY

SIMU.tv: Taasisi ya Benjamini William Mkapa inakusudia kutumia zaidi ya shilingi bilioni 136 kwa ajili ya kufadhili na kugharamia miradi ya afya inayokusudiwa kunufaisha watanzania milioni 20. https://youtu.be/ILG66j-YCIU

No comments: