Monday, April 18, 2016

MKUU WA MKOA WA KILIMANJARO MHE. SAIDI MECK SADIKI ATEMBELEA LANGO LA LONDOROSI HIFADHI YA TAIFA KILIMANJARO

Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro Mh. Saidi Meck Sadiki (watatu kutoka kulia) na Mkuu wa Wilaya ya Siha Dk. Charles Mlingwa ( wa kwanza kulia) wakiwasili katika lango la Londorosi, Hifadhi ya Taifa Kilimanjaro. Katikati ni mwenyeji wao Betrita Loibooki, Mkuu wa Hifadhi ya Taifa Kilimanjaro.
Mkuu wa Hifadhi ya Taifa Kilimanjaro akiwasilisha taarifa fupi ya Hifadhi ya Kilimanjaro kwa Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro Mhe. Saidi Meck Sadiki akiwa katika lango la Londorosi.
Mkuu wa Idara ya Utalii Hifadhi ya Taifa Kilimanjaro, Charles Ngendo akionyesha maeneo ya hifadhi kwenye ramani kufafanua taarifa ya Mkuu wa Hifadhi.
Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro Mhe. Saidi Meck Sadiki akiongea na watumishi wa hifadhi, wilaya na mkoa katika lango la Londorosi.
Watumishi wa Hifadhi ya Kilimanjaro, Wilaya ya Siha na Mkoa wa Kilimanjaro wakimsikiliza kwa makini Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro.
Akiongozwa na Mhifadhi Imani Kikoti, Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro alipata fursa ya kutembea kwa miguu kupanda mlima kuelekea uwanda wa Shira.
Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro na ujumbe wake kutoka mkoani na Wilaya ya Siha wakipewa maelezo juu ya vivutio na jiolojia ya uwanda wa Shira kutoka kwa Charles Ngendo, Mhifadhi Utalii wa Hifadhi ya Taifa Kilimanjaro.
Picha ya pamoja ya Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro alipotembelea Hifadhi ya Taifa ya Kilimanjaro. Hapa akionekana na msafara wake na viongozi wa hifadhi ya Kilimanjaro wakiwa uwanda wa Shira (mita 3962)

No comments: