Saturday, April 9, 2016

MAMLAKA YA MAPATO TANZANIA TRA YAENDELEZA ZOEZI LA KUBOMOA MTANDAO WA WAFANYA BIASHARA YA MAGENDO UKANDA WA KUSINI MWA PWANI

Na Mwandishi Wetu-Kilwa.

Siku ya tarehe 6/4/2016 maofisa wa Mamlaka ya Mapato Tanzania kikosi cha (FAST)  wakiwa na maofisa wa Polisi walifanya upekuzi kwa lengo la kutafuta magendo kwenye nyumba ya mfanyabiashara Yusuf Barkat Sareh.

Upekuzi huo ulifanyika baada ya kupata taarifa za kiintelijensia zilizofanyiwa kazi muda mrefu.

Bidhaa mbalimbali kutoka nje ya nchi zilikamatwa kama zifuatazo
Sukari ya India kilo 50 jumla mifuko762Sukari ya nje iliyokamatwa kwenye mifuko ya viwanda vya hapa nchini kilo 25 jumla mifuko 135,Mafuta ya kula lita ishirini (20) aina mbalimbali kutoka nje jumla madumu 49,Betri aina ya tigger katoni 223,Amira katoni 135,Sabuni za kufulia katoni 48

Vitu mbalimbali vilivyokamatwa kama ushahidi wa biashara haramu ya magendo ya sukari.Mashine mbili (2) za kushonea kwenye mifuko ya iliyowekwa sukari inatoka nje ya nchi na kuwekwa kwenye mifuko ya viwanda vya nchini nya sukari vya Kilombero,TPC na Mtibwa Sugar.
Mifuko mitupu mipya ya sukari kilo 25 toka India  2000
Mifuko iliyotumika ya kilo 50 mitupu ya sukari36,000
mifuko ya sukari iliyotumika ya Viwanda vya Tanzania ya kilo25 kiasi cha 1150
Madumu mafuta ya nje mchanganyiko ya kula lita 20 kiasi cha 609
Madumu matupu ya lita 10 ya nje kiasi cha 310.
Nyumba hii ndiyo Ofisi ya Bosi ambayo hutumika kuweka bidhaa kabla ya kusambazwa sokoni iliyopo Somanga njia nne eneo la Kikanda Wilaya ya Kilwa mkoa wa Lindi.
sehemu ya kuweka sukari na kupima.
Nyumba inayotumika kuweka sukari
Mkurugenzi wa Elimu kwa walipa kodi Mamlaka ya Mapato Tanzania TRA, Richard Kayomboakionesha ndoo zinazotarajiwa kuwekwa mafuta.
Sukari na viroba vya kuweka kwa matayarisho ya kuingizwa sokoni.
Hii ni Sukari iliyomwangwa chini kabla ya kuwekwa kwenye viroba
Askari wakisimamia zoezi la kuvunja mlango

Mkurugenzi wa Elimu kwa walipa kodi Mamlaka ya Mapato Tanzania TRA, Richard Kayombo akizungumza na waandishi.
Mkurugenzi wa Elimu kwa walipa kodi Richard Kayombo wa Mamlaka ya Mapato Tanzania TRA akionesha sukari.
Mkurugenzi wa Elimu kwa walipa kodi Richard Kayombo wa Mamlaka ya Mapato Tanzania TRA 
Aina ya mafuta kutoka nje ya nchi tayari kuwekwa kwenye ndoo kwa kupeleka Sokoni
Polisi akilinda viroba vyenye sukari kutoka nje ya nchi.
Madumu yaliyokua na mafuta ya kula na ndoo zinazotarajiwa kuwekwa mafuta
Nyumba ya mtuhumiwa Yusuf Sareh iliyopo Somanga Njia nne Kikanda.

1 comment:

Anonymous said...

The mdudu, tunaomba afungwe maisha na afilisiwe kila kilicho chake, huyu kwanza amemzarau na kumpuuza rais wetu mpendwa John Pombe Magufuli kukemea kote kule lakini yeye amejikuta yeye ndio yeye hakuna mtu wa kumgusa kwenye nchi yetu na tunaomba msako kama huo ufanywe usiku na mchana nchi nzima coz wapo wengi sana na ndio hao waliokua wanamchezea JK na serikali yake ila umefika mwisho wao