Monday, April 18, 2016

MAKAMU WA RAIS MHE. SAMIA AZINDUA MBIO ZA MWENGE WA UHURU MKOANI MOROGORO LEO

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan, akiwasha Mwenge wa Uhuru kuzindua rasmi mbio za Mwenge wa Uhuru Mwaka 2016 leo Aprili 18, 2016.  sherehe iliyofanyika katika uwanja wa Jamhuri Mkoani Morogoro. Kulia ni Waziri wa Uwezeshaji Ustawi wa Jamii, Vijana, Wanawake na Watoto - Zanzibar Mhe. Modelin Kastiko.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan, akimkabidhi Mwenge wa Uhuru kiongozi wa mbio za Mwenge kwa mwaka 2016 George Jackson Mbijima kutoka mkoa wa Mbeya kwa ajili ya kukimbiza mwenge huo katika Mikoa na wilaya zote za Tanzania.Picha na OMR
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan, akihutubia Taifa kwenye Sherehe za uzinduzi wa Mwenge wa Uhuru kitaifa zilizofanyika leo april 18, 2016 katika Uwanja wa Jamhuri Mkoani Morogoro.

No comments: