Monday, April 11, 2016

KUKOSEKANA KWA UWAJIBIKAJI KUNAFANYA MFUMO MAISHA YA WANANCHI KUHARIBIKA –DK.MPANGO.

 Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Uwajibikaji Tanzania (WIPA) ambaye ni Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali, Ludovick Utouh akizungumza katika ufunguzi wa Kongamano la  Kimataifa linalojadili juu ya Uwajibikaji katika Sekta ya ya Gesi na Mafuta  lililoandaliwa na Taasisi ya Uwajibikaji Tanzania (WIPA) jijini Dar es Salaam.
 Waziri wa Fedha na Mipango, Dk.Philip Mpango akizungumza katika ufunguzi wa Kongamano la  Kimataifa linalojadili juu ya Uwajibikaji katika Sekta ya ya Gesi na Mafuta lililoandaliwa na Taasisi ya Uwajibikaji Tanzania (WIPA) katika ukumbi wa Mwalimu Nyerere jijini Dar es Salaam leo. 
Waziri wa Fedha na Mipango, Dk.Philip Mpango na Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Uwajibikaji Tanzania (WIPA) ambaye ni Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali, Ludovick Utouh  wakikata utepe kuashiria ufunguzi wa Kongamano la  Kimataifa linalojadili juu ya Uwajibikaji katika Sekta ya ya Gesi na Mafuta lililoandaliwa na Taasisi ya Uwajibikaji Tanzania (WIPA) jijini Dar es Salaam leo.
 Waziri wa Fedha na Mipango, Dk.Philip Mpango akikabidhiwa kibao maalumu mara baada ya kuzindua Kongamano la  Kimataifa linalojadili juu ya Uwajibikaji katika Sekta ya ya Gesi na Mafuta lililoandaliwa na Taasisi ya Uwajibikaji Tanzania (WIPA) na Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Uwajibikaji Tanzania (WIPA) ambaye ni Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali, Ludovick Utouh jijini Dar es Salaam leo.
Waziri wa Fedha na Mipango, Dk.Philip Mpango akiwa katika picha ya pamoja  katika Sekta ya ya Gesi na Mafuta lililoandaliwa na Taasisi ya Uwajibikaji Tanzania (WIPA) katika ukumbi wa Mwalimu Nyerere jijini Dar es Salaam leo. 
Picha na Avila Kakingo, Globu ya Jamii.

Na Chalila Kibuda,Globu ya Jamii
WAZIRI wa Fedha na Mipango, Dk.Philip Mpango amesema kukosekana kwa uwajibikaji na utawala bora  kunafanya mfumo wa maisha ya wananchi kuharibika.

Dk.Mpango ameyasema hayo leo katika ufunguzi wa Kongamano la  Kimataifa linalojadili juu ya Uwajibikaji katika Sekta ya ya Gesi na Mafuta  lililoandaliwa na Taasisi ya Uwajibikaji Tanzania (WIPA) ,amesema katika kuweza kufikia uchumi wakati lazima lipewe kipaumbele katika uwekezaji wa Gesi na Mafuta.

Amesema jamii inayoamini uwajibikaji na utawala bora inafanya jamii hiyo kuwajibika kwa pamoja katika maendeleo ya kiuchumi.

Dk.Mpango amesema akiwa Waziri mwenye dhamana ni kuangalia uwajibikaji kwa raia katika nchi na bila kuangalia uwajibikaji na utawala bora  mfumo wa maisha ya wananchi unaharibika.

Amesema taasisi ya wajibu ni moja ya taasisi ambayo itasaidia juu ya kutafsiri wa uwajibikaji kwa wananchi kwa lugha inayofahamika na kueleweka.

Nae Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Uwajibikaji Tanzania (WIPA) ambaye ni Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali, Ludovick Utouh amesema nia ya kongamano hilo ni kutafuta mawazo ya watu wengine katika uwajibikaji wa katika sekta ya Gesi na Mafuta.

Utouh amesema kuwa kutokana na rasilimali hiyo kugundulika wameona kuna umuhimu wa kushirikisha watu wengine ambao walipata rasilimali hiyo lakini hakuweza kuwasaidia ambapo hata Tanzania tunaweza kuangukia huko.

Mkutano huo umeshirikisha watu waliobobea katika sekta ya Gesi na Mafuta katika kutoa mawazo yao juu ya Tanzania inavyoweza kufanya  katika sekta hiyo.

No comments: