Saturday, April 16, 2016

Balozi Seif afunga mafunzo ya Uongozi mdogo wa Polisi Zanzibar

 Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi akikagua gwaride la wahitimu wa mafunzo ya uongozi Mdogo wa Polisi katika ngazi ya Ukoplo, Sajenti na Stafu Sajent hapo chuo cha Polisi Ziwani Mjini Zanzibar.
 Askari wa Kike wa Jeshi la Polisi ngazi ya Ukoplo, Sajenti na Stafu Sajenti wakipita kwa mwendo wa haraka mbele ya mgeni rasmi wakati wakimaliza mafunzo yao ya wiki nane kwenye chuo cha Polisi Ziwani.
 Wahitimu wa mafunzo ya Uongozi mdogo wa Polisi ngazi ya Koplo, Sajenti na Stafu Sajenti wakifanya vitu vyao katika kuonyesha moja ya mafunzo waliyoyapata mchezo wa Singe kwenye hafla ya kumaliza mafunzo yao.
 Baadhi ya Askari wa Jeshi la Polisi wakiwemo wale waliomaliza mafuno ya Uongozi mdogo wa Polisi wakimsikiliza Balozi Seif alipokuwa akizungumza nao kwenye ufungaji wa mafunzo hayo.
 Kikundi cha Kwaya cha Wahitimu wa mafunzo ya Uongozi mdogo wa Polisi ngazi ya Koplo, Sajenti na Stafu Sajenti wakitoa burdani ya wimbo maalum kwenye ufungaji wa mafunzo yao hapo Ziwani.
Burudani kwa wahitimu wa mafunzo ya Uongozi mdogo wa Polisi ngazi ya Koplo, Sajenti na Stafu Sajenti wakitoa burdani ya wimbo maalum kwenye ufungaji wa mafunzo yao hapo Ziwani.
 Askari Godrey Kihimba Mjanja akivishwa cheo cha Koplo na Balozi Seif baada kumaliza mafunzo yake na kufanya kufanikiwa kuwa miongoni mwa askari Tisa waliofanya vyema katika mafunzo yao.
 Balozi Seif akimvisha cheo cha Sajenti Asha Hussein Magungu baada ya kumaliza mafunzo yake na kuwa miongozi mwa askari waliofanya vizuri katika mafunzo yao.
 Kamishna wa Polisi Zanzibar Hamdan Omar Makame akitoa maelezo kujiandaa kumkaribisha Balozi Seif kuyafunza rasmi mafunzo ya Uongozi mdogo wa Polisi.
Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif akizungumza na Makamanda na wahitimu wa mafunzo ya Uongozi mdogo wa Polisi wakati akiyafunga mafuno hayo.
Picha na – OMPR – ZNZ.

No comments: