Tuesday, March 8, 2016

UNDP WAFANYA KONGAMANO LA VIJANA, LENGO NI KUWASAIDIA KUFANYA MAAMUZI SAHIHI

Hawa Dabo

Mkurugenzi Mkazi wa UNDP nchini, Awa Dabo akitoa neno la ufunguzi katika kongamano la vijana na maendeleo, kongamano lililofanyika katika Ukumbi wa Nkrumah uliopo katika Chuo Kikuu cha Dar es Salaam.(Picha zote na Zainul Mzige wa Modewjiblog).


Shirika la Umoja wa Mataifa la Maendeleo (UNDP) kwa kushirikiana na Chuo Kikuu cha Dar es Salaam limefanya kongamano la vijana na maendeleo kujadili jinsi vijana wanavyoweza kutumika kusaidia kuleta maendeleo nchini na kubadili mfumo wa vijana katika kufanya maamuzi yaliyo sahihi.

Akizungumzia kongamano hilo limelofanyika siku ambayo UNDP imetiza miaka 50 tangu kuanzishwa, Mkurugenzi Msaidizi wa UNDP nchini, Amon Manyama alisema kuwa vijana wana nafasi kubwa katika jamii na kama wakitumika vizuri wanaweza kusaidia kupatikana kwa maendeleo na hivyo kupitia kongamano hilo wanataraji kuwapa mbinu mpya.

Alisema mbali ya kuangala jinsi wanavyoweza kusaidia kupatikana kwa maendeleo pia wanajadili kwa pamoja ili kuona jinsi gani wanaweza kubadili mfumo wa vijana wa kufanya maamuzi ambao wengi wao wamekuwa wakifanya maamuzi ambayo baadae yanaonekana kutokuwa sahihi.

“Tunafanya kongamano hili na vijana kutoka vyuo mbalimbali ili kuona mustakabali wa vijana wa Tanzania, kuona jinsi gani wanaweza kusaidia kupatikana kwa maendeleo Tanzania na hata kubadili mfumo wao wa kufanya maamuzi,” alisema Manyama.
Youth and Development Symposium UNDP, Tanzania
IMG_5271
Mkurugenzi Msaidizi wa UNDP nchini na mshereheshaji wa kongamano hilo, Amon Manyama akizungumza katika kongamano la vijana na maendeleo.

Nae Mkurugenzi Mkazi wa UNDP nchini, Awa Dabo alisema vijana wana nafasi kubwa kusaidia uapatikanaji wa maendeleo nchini na wao kama UNDP wamekuwa wakisaidia na serikali ili kuwasaidia vijana kwa kuwapa mbinu ambazo wanaweza kutumia ili kufikia malengo waliyonayo.

Alisema licha ya kuwepo changamoto zilizopo katika sera ya vijana lakini pia vijana wamepoteza udhubutu wa kufanya maamuzi na hivyo kongamano hilo wanaweza kukuza uwezo wao wa kujiamini na kufanya maamuzi ambayo yanakuwa ni sahihi.

“Vijana wanatakiwa kuwa na malengo na kukuza uwezo wa kujiamini … vijana wanaweza kusaidia kupatikana maendeleo Tanzania na wana hamasa ya kusaidia kupatikana maendeleo hivyo wanatakiwa kupewa nafasi katika kufanya maamuzi,” alisema Bi. Dabo.
IMG_5296
Mkurugenzi Mkazi wa UNDP nchini, Awa Dabo akitoa neno la ufunguzi katika kongamano la vijana na maendeleo, kongamano lililofanyika katika Ukumbi wa Nkrumah uliopo katika Chuo Kikuu cha Dar es Salaam.
IMG_5323
Sehemu ya vijana kutoka vyuo mbalimbali wakimsikiliza Mkurugenzi Mkazi wa UNDP nchini, Awa Dabo wakati akitoa neno la ufunguzi wa kongamano hilo.

Kwa upande wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam kupitia kwa Mkuu wa Idara ya Uchumi, Jehovaness Aikaeli alisema vijana wanaweza kutumiwa kama fursa hasa katika kipindi hiki ambacho kunakuwa na vijana wengi ambao wanatoka vijijini na kukimbilia mijini na hivyo kama wakishirikishwa wanaweza kusaidia kupatikana maendeleo.
IMG_5369
Mkuu wa Idara ya Uchumi katika Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, Jehovaness Aikaeli akizungumza na waandishi wa habari katika kongamano hilo.
Nae mmoja wa vijana aliyeshiriki katika kongamano hilo, Ncheye Revina alisema mifumo inayotumika sasa nchini inawabana vijana kusaidia kupatikana kwa maendeleo na kama watakuwa wanataka vijana wahusike kikamilifu basi wawatolee vikwazo vinavyowabana kushiriki akitolea mfano katika ajira kwa ajili wengi kutaka wafanyakazi walio na uzoefu mkubwa wa kazi jambo ambalo ni ngumu kupata vijana.
IMG_5571
Mmoja wa vijana aliyeshiriki katika kongamano hilo, Ncheye Revina.
IMG_5413
Benedict Kikove kutoka Ubalozi wa Japan nchini akiwaelezea vijana fursa zilizopo kwa vijana na changamoto wanazokumbana nazo wakati wa kongamano la vijana na maendeleo lililoandaliwa na UNDP.
IMG_5450
Afisa Mipango wa Shirika la Umoja wa Mataifa la Kujitolea (UNV), Stella Karegyesa akifuatilia kwa makini kongamano la vijana na maendeleo.
Hawa Bayumi
Meneja Huduma za Jamii wa Airtel, Hawa Bayumi (kushoto) nae alikuwa ni miongoni mwa watoa mada katika kongamano hilo.
IMG_5666Afisa Habari wa kituo cha Habari cha Umoja wa Mataifa (National Information Officer-UNIC), Bi. Usia Nkhoma- Ledama (wa kwanza kulia) akifuatilia kilichokuwa kikiendelea katika kongamano hilo lililoandaliwa na UNDP.
IMG_5394Fatma Mohamed kutoka Shirika la Umoja wa Mataifa la Kujitolea (UNV) akizungumzia changamoto wanazokutana nazo vijana katika kutafuta mafanikio.
IMG_5507Mwakilishi wa Wizara ya Katiba na Sheria kutoka Zanzibar, Saleh Mubarak akielezea washiriki jinsi serikali inavyowasaidia vijana katika kongamano la vijana na maendeleo.
IMG_5390
Baadhi ya washiriki wa kongamano hilo ambao ni vijana na wadau kutoka mashirika na taasisi mbalimbali nchini lililofanyika katika Ukumbi wa Nkrumah uliopo Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM).
Youth Symposium -UNDP Tanzania
Youth Symposium -UNDP Tanzania
IMG_5679
Afisa wa Utawala Bora kutoka Shirika la Umoja wa Mataifa la Maendeleo (UNDP), Godfrey Mulisa akielezea jinsi washirika wa maendeleo wanavyotoa fursa kwa vijana na jinsi fursa hizo zinavyoweza kuwasaidia vijana wa Tanzania.
IMG_5687
Mkurugenzi Mkazi Shirika la Umoja wa Mataifa linaloshughulikia Idadi ya Watu (UNFPA), Natalia Kanem akizungumza wakati wa kongamano hilo.
IMG_5749
Pichani juu na chini ni vijana kutoka vyuo mbalimbali nchini wakishiriki kutoa maoni kwenye kongamano hilo.
Youth Symposium -UNDP Tanzania
IMG_5796
Makamu Mkurugenzi Mkazi wa UNDP nchini, Titus Osundina akitoa neno la hitimisho la kongamano la vijana na maendeleo.

No comments: