Tuesday, March 1, 2016

SIMU TV: HABARI KUTOKA TELEVISHENI

Simu.tv: Wananchi wilayani Mbozi mkoani Mbeya walalamikia hatua ya mtu mmoja kuamia eneo la ekari zaidi ya 40 na kufyeka miti katika eneo hilo huku wakidai eneo hilo lilitengwa kwa ajili ya matumizi ya shule.https://youtu.be/077XNbgbOgI

Simu.tv: Mamlaka ya udhibiti wa huduma za nishati na maji EWURA yatangaza bei kikomo za bidhaa za nishati ya mafuta hapa nchini huku bei za mafuta ya Petrol na diesel zikishuka. https://youtu.be/L9Suz00kPuM

 Simu.tv: Ujumbe wa viongozi wa waandamizi wa ukanda huru wa kibiashara kutoka falme za kiarabu watua nchini kutafuta fursa za ushirikiano katika Nyanja mbalimbali za kibiashara na ujasiriamali. https://youtu.be/LDktZ6Lc_yY

Simu.tv: Baada ya kuibuka na ushindi katika pambano lake la ubingwa wa mabara, bondia Francis Cheka azungumza na watanzania kupitia vyombo vya habari. https://youtu.be/_3RHvlIj-4c
  
Simu.tv: Serikali kupitia wizara ya habari, utamaduni sanaa na michezo yatoa kiasi cha shilingi milioni 15 kwa ajili ya timu ya taifa ya wanawake ya mpira wa miguu Twiga Stars, kama motisha kuelekea mchezo dhidi ya Zimbabwe.https://youtu.be/rIhhhWIgQyc

 Simu.tv: Wajasiriamali zaidi ya 70 mkoani Dar es salaam wapatiwa mafunzo ya usindikaji na ufugaji kutoka shirika la viwanda vidogo vidogo SIDO.https://youtu.be/T1wx9wh-bac

 Simu.tv: Baadhi ya wakuu wa nchi wanachama wa Jumuiya ya Afrika Mashariki waanza kuwasili Arusha kushiriki mkutano wa 17 wa jumuiya hiyo;https://youtu.be/jDkxQBpSq_8

Simu.tv: Rais wa Uganda, Yoweri  Museveni ampongeza Rais John Magufuli kwa utendaji kazi wake toka alipoingia madarakani;https://youtu.be/DH6nOkbZNh4

 Simu.tv: Serikali yaiagiza kampuni ya Degretmont Spencon Consortium kukamilisha haraka ujenzi wa mradi wa maji katika halmashauri ya Musoma ifikapo Juni 30 mwaka huu; https://youtu.be/AWT-c8mFs58

Simu.tv: Baadhi ya walimu na wanafunzi katika shule ya msingi Juhudi mkoani Kigoma waiomba serikali kuboresha miundombinu ya shule hiyo;https://youtu.be/NlvzHIKgt_Y

Simu.tv: Wakazi wa Kikuyu kusini mjini Dodoma wamuomba waziri wa ardhi, Mhe. William Lukuvi kuingilia kati mgogoro wa ardhi uliopo baina yao na manispaa ya Dodoma; https://youtu.be/z1tccJoG1n8

Simu.tv: Shirika la utangazaji Tanzania TBC linatarajia kufungua studio ya radio kanda ya kaskazini ili kuweza kuifikishia jamii  habari mbali mbali kwa ukaribu zaidi; https://youtu.be/dMTRakUcRRg

Simu.tv: Mkurugenzi wa idara ya habari maelezo , Assah  Mwambene aliitaka gazeti la Dira ya Mtanzania kuomba radhi kutokana na habari iliyochapishwa katika gazeti hilo toleo namba 404 kuhusu katibu mkuu Balozi Ombeni Sefue;https://youtu.be/Qf6icyPJ_Gc


Simu.tv: Mamlaka ya chakula na dawa nchini TFDA jijini Dar es Salaam yakamata chupa zaidi ya 5300 za Marashi bandia;https://youtu.be/fMS7JdK0WiU

Simu.tv: Mfuko wa hifadhi ya jamii wa LAPF umefanikiwa kukusanya  jumla ya shilingi bilioni 210  na kutoa mafao yenye thamani ya bilioni 88 hadi kufikia mwishoni mwa mwaka jana; https://youtu.be/P1egbBJ1oo8

Simu.tv: Inaelezwa kuwa bei ya nishati ya mafuta nchini yashuka kutokana na kushuka kwa bei  ya mafuta katika soko la dunia; https://youtu.be/CfkNV-XBOpM


Simu.tv: Wizara ya Habari, Utamaduni , Sanaa na Michezo imekusanya jumla ya shilingi milioni kumi na tano kwa ajili ya timu ya taifa ya wanawake ya Twiga stars inayojiandaa kucheza na timu ya taifa ya wanawake ya Zimbabwe;https://youtu.be/BHMGQ7J31Z8

Simu.tv: Bondia Francis Cheka amekanusha taarifa juu ya kubebwa katika pambano lake dhidi ya bondia Geard Ajetovic lililochezwa siku ya  jumamosi ya wiki iliyopita ; https://youtu.be/yZVYKzD1pN4

Simu.tv: Rais wa Zanzibar Dkt.Ali Mohamed Shein amesema juhudi kubwa zimechukuliwa na serikali ya mapinduzi Zanzibar katika kuimarisha miundombinu ya sekta ya afya  ili kuimarisha zaidi huduma za afya kwa wananchi katika maeneo mbalimbali ya mjini na vijijini;https://youtu.be/6V4AEEpU2jU

Simu.tv: Mamlaka ya  mjini mkongwe Zanzibar yabomoa bango kubwa katika milango ya maduka ya mfanyabiashara  Said Bakhresa kwa kukiuka sheria  ya ujenzi ya uhifadhi wa mjini mkongwe; https://youtu.be/RCY5HrXRZyc

Simu.tv: Naibu wa kilimo, uvuvi na mifugo Waziri William Ole Nasha aagiza watuhumiwa wa wizi wa milioni 160 za SACCOS ya Sanya juu kufikishwa mahakamani na kufilisiwa. https://youtu.be/jl81edFJ7tc

No comments: