Wednesday, March 2, 2016

Serikali yaahidi kuwapatia vijana mitaji kwa ajili ya kilimo cha kisasa

 Mkurugenzi Maendeleo ya Vijana Taifa Ofisi ya Waziri Mkuu;Sera,Uratibu,Bunge,kazi,Ajira,Vijjana na watu wenye Ulemavu James Kajugusi (katikati) akipata ufafanuzi juu ya kilimo cha mbogamboga toka kwa Mwenyekiti Kinondoni Saccoss Neema Urio (Kulia) katika ufunguzi mafunzo ya kilimo cha kisasa kwa vijana kulia mwa Mkurugenzi Maendeleo ya Vijana ni Mkurugenzi Msaidizi Mafunzo Idara ya Vijana Venerose Mtenga na kushoto ni Mkurugenzi Uhamasishaji Idara ya Vijana Esther Riwa.
 Mkurugenzi Maendeleo ya Vijana Taifa Ofisi ya Waziri Mkuu;Sera,Uratibu,Bunge,kazi,Ajira,Vijjana na watu wenye Ulemavu James Kajugusi (katikati) akipata ufafanuzi juu ya matumizi ya jiko linalotumia nishati ya jua toka kwa Meneja wa Tanzania Agriculture Productivity Programme Praygod Mushi (Kulia) katika ufunguzi mafunzo ya kilimo cha kisasa kwa vijana kushoto ni Mkurugenzi Uhamasishaji Idara ya Vijana Esther Riwa.
 Mkurugenzi Maendeleo ya Vijana Taifa Ofisi ya Waziri Mkuu;Sera,Uratibu,Bunge,kazi,Ajira,Vijjana na watu wenye Ulemavu James Kajugusi (mwenye koti la Draft) akitoa ushauri kwa wajasiriamali toka Pop Up the Best Tailoring wa Sinza Dar es Salaam walioshiriki mafunzo ya usajasiriamali yaliyofanyika Jijini Dar es salaam, kushoto ni Mkurugenzi Uhamasishaji Idara ya Vijana Esther Riwa.
 Mkurugenzi Uhamasishaji, Idara ya Vijana Esther Riwa akizungumza na washiriki (Hawapo pichani) wa mafunzo ya ya kilimo cha kisasa kwa vijana yaliyofanyika Jijini Dar es salaam.

 Mkurugenzi Msaidizi Mafunzo Idara ya Vijana Venerose Mtenga akiongea na washiriki wa mafunzo ya kilimo cha kisasa kwa vijana kushoto ni  Mkurugenzi Maendeleo ya Vijana taifa James Kajugusi.

 Mkurugenzi Maendeleo ya Vijana Taifa Ofisi ya Waziri Mkuu;Sera,Uratibu,Bunge,kazi,Ajira,Vijjana na watu wenye Ulemavu James Kajugusi akizungumza na washiriki (Hawapo pichani) wa mafunzo ya ya kilimo cha kisasa kwa vijana yaliyofanyika Jijini Dar es salaam.
 Baadhi ya vijana wakimsikiliza mtoa mada(Hayupo pichani) juu ya juu ya kilimo cha kisasa kwa vijna katika mafunzo yaliyofanyika Jiji Dar es salaam na kushirikisha vijana toka Dar es salaam na pwani. 
 Mmoja wa washiriki wa mafunzo ya kilimo cha kisasa kwa vijana Bi. Jasmin John akitoa neno la shukrani kwa mgeni rasmi mara baada ya kufungua mafunzo hayo yanayofanyika kwa siku tatu Jijini Dar es salaam.
 Mkurugenzi Maendeleo ya Vijana Taifa Ofisi ya Waziri Mkuu;Sera,Uratibu,Bunge,kazi,Ajira,Vijjana na watu wenye Ulemavu James Kajugusi akipongezana na Mkurugenzi Msaidizi Mafunzo Idara ya Vijana Venerose Mtenga mara baada ya kufunguliwa kwa mafunzo ya kilimo cha kisasa kwa vijina yanayofanyika jijini Dar es Salaam.
Mkurugenzi Maendeleo ya Vijana Taifa Ofisi ya Waziri Mkuu;Sera,Uratibu,Bunge,kazi,Ajira,Vijjana na watu wenye Ulemavu James Kajugusi akisalimiana na Mwenyekiti wa mafunzo ya kilimo cha kisasa kwa vijana Bi Mary Lucian Mdendemi mara baada ya kufunguliwa kwa mafunzo ya kilimo cha kisasa kwa vijina yanayofanyika jijini Dar es Salaam, katikati ni Mkurugenzi Uhamasishaji, Idara ya Vijana Esther Riwa.Picha zote na Raymond Mushumbusi ( WHUSM)  


Na Shamimu Nyaki-WHUSM 02/03/2016

Katika kuboresha na kuongeza  ajira  hapa nchini Serikali imeahidi kuwapatia Vijana  mtaji na maeneo kwa ajili ya kilimo cha kisasa ili waweze kujiendeleza na  kukuza kipato chao.

Akizungumza katika ufunguzi wa mafunzo ya kilimo cha kisasa cha “Green Houses” Mkurugenzi wa Maendeleo ya Vijana  Ofisi ya Waziri Mkuu Sera, Uratibu, Bunge, Vijana, Kazi,  Ajira na watu wenye Ulemavu, Bw. James Kajugusi  amesema  kuwa ni wakati muafaka  kwa vijana kutumia fursa mbalimbali zinazojitokeza katika kilimo kwa kuwa ndio uti wa mgongo wa Taifa letu.

Ameongeza kuwa Serikali inaendelea kuwawezesha kupata mikopo kwa riba nafuu na kutoa elimu kuhusu kilimo bora  cha kisasa ili kuondoa fikra zilizopo kwa vijana kuwa kilimo ni kwa ajili ya watu waliokosa elimu,wenye maisha duni na wale wanaoishi maeneo ya vijijini.

“Ni lazima tutumie fursa zinazojitokeza katika kunufaika,nina imani mtatumia fursa hii kwa manufaa yenu na elimu mtakayopata itawasaidia kuzalisha bidhaa bora na kuondoa utegemezi. Alisema Mkurugenzi Kajugusi”.

Aidha mwezeshaji wa mafunzo hayo Bw Praygod Mushi amewataka vijana hao kuamini kuwa kilimo kinaweza kubadilisha maisha yao  kama watatumia fursa zote zinazojitokeza  katika sekta ya kilimo kuanzia ngazi ya familia mpaka Taifa.

Naye mmoja wa washiriki katika mafunzo hayo Bi Jasmini John ameishukuru Serikali kwa kuaandaa mafunzo hayo na kusema kuwa atatumia elimu atakayopata kuendeleza kilimo kama ajira kwa kutumia pembejeo za kisasa atakazoelekezwa katika mafunzo hayo.

Mafunzo ambayo vijana hao  wamepewa  ni  jinsi ya kutumia dawa na mbegu bora katika kilimo,kunufaika  na mazao yatokanayo na kilimo cha Green House,utunzaji wa mazingira kwa kutumia Nishati ya mwanga wa jua pamoja na ubunifu wa shughuli  za vijana katika jitihada za kukuza viwanda  kwa kutumia mali ghafi za humu nchini.

Mafunzo hayo yanatolewa kwa siku tatu kuanzia leo na yameshirikisha vijana kutoka Mkoa wa Dar es Salaam na Pwani.

No comments: