Saturday, March 5, 2016

RAIS MAGUFULI AHUDHURIA MAZISHI YA KAKA WA RAIS MSTAAFU JAKAYA KIKWETE KIJIJINI MSOGA

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Joseph Magufuli akimpa pole Rais Mstaafu Dkt Jakaya Mrisho Kikwete kwa kufiwa na kaka yake, Mzee Selemani Mrisho Kikwete, wakati wa mazishi kijijini Msoga, Chalinze, wilayani Bagamoyo mkoa wa Pwani leo Machi 5, 2016.
Mama Janeth Magufuli, mke wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Joseph Magufuli akimpa pole Rais Mstaafu Dkt Jakaya Mrisho Kikwete kwa kufiwa na kaka yake, Mzee Selemani Mrisho Kikwete, wakati wa mazishi kijijini Msoga, Chalinze, wilayani Bagamoyo mkoa wa Pwani leo Machi 5, 2016.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Joseph Magufuli akimfariji Mjane wa Marehemu Mzee Selemani Mrisho Kikwete, wakati wa mazishi kijijini Msoga, Chalinze, wilayani Bagamoyo mkoa wa Pwani leo Machi 5, 2016
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Joseph Magufuli na mkewe Mama Janeth Magufuli wakimfariji Mjane wa Marehemu Mzee Selemani Mrisho Kikwete na wanafamilia, wakati wa mazishi kijijini Msoga, Chalinze, wilayani Bagamoyo mkoa wa Pwani leo Machi 5, 2016.
Makamu wa Rais Mhe Samia Suluhu Hassan na Mama Janeth Magufuli, mke wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Joseph Magufuli pamoja na Mama Salma Kikwete wakiwa msibani kwa kaka yake Rais Mstaafu Dkt Jakaya Mrisho Kikwete, MarehemuMzee Selemani Mrisho Kikwete, wakati wa mazishi kijijini Msoga, Chalinze, wilayani Bagamoyo mkoa wa Pwani leo Machi 5, 2016. Wengine kutoka kushoto ni Mama Asha Bilali, Mama Khadija Mwinyi, Mama Sitti Mwinyi, Mama Asha Seif Ali Iddi.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Joseph Magufuli akipokea hela ya utani toka kwa Mbunge wa Chalinze Mhe Ridhiwani Kikwete wakati wa mazishi ya Baba yake Mkubwa Mzee Selemani Mrisho Kikwete, kijijini Msoga, Chalinze, wilayani Bagamoyo mkoa wa Pwani leo Machi 5, 2016 wanaoshuhudia ni Rais wa Zanzibar Dkt Ali Mohamed Shein, Rais wastaafu Dkt Jakaya Mrisho Kikwete, Mhe. Benjamin Mkapa, Alhaj Ally Hassan Mwinyi na Waziri Mkuu Mstaafu Mhe John Malecela. Katika utamaduni wa Kitanzania Wakwere na Wasukuma ni watani.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Joseph Magufuli akimkabidhi hela ya utani kwa mkaazi wa Chalinze ambaye ni Msukuma Bwana Luhende baada ya kuipokea toka kwa Mbunge wa Chalinze Mhe Ridhiwani Kikwete wakati wa mazishi ya Baba yake Mkubwa Mzee Selemani Mrisho Kikwete, kijijini Msoga, Chalinze, wilayani Bagamoyo mkoa wa Pwani leo Machi 5, 2016 wanaoshuhudia ni Rais wa Zanzibar Dkt Ali Mohamed Shein, Rais wastaafu Dkt Jakaya Mrisho Kikwete, Mhe. Benjamin Mkapa, Alhaj Ally Hassan Mwinyi na Waziri Mkuu Mstaafu Mhe John Malecela. Katika utamaduni wa Kitanzania Wakwere na Wasukuma ni watani.
Rais wa Jamhuri ya Muungano Dkt. John Pombe Magufuli akiweka mchanga kwenye kaburi la Mzee Selemani Mrisho Kikwete huko Msoga mkoani Pwani. Mzee Selemani Kikwete alikuwa kaka mkubwa wa Rais Mstaafu wa awamu ya nne Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete.
Rais Mstaafu Dkt Jakaya Mrisho Kikwete akiweka udongo kaburini wakati wa mazishi ya kaka yake, Mzee Selemani Mrisho Kikwete, wakati wa mazishi kijijini Msoga, Chalinze, wilayani Bagamoyo mkoa wa Pwani leo Machi 5, 2016.
Aliyekuwa Mwenyekiti wa CCM mkoa wa Shinayanga, Bw. Khamis Mgeja akiongea na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Joseph Magufuli na Rais MStaafu Dkt Jakaya Mrisho Kikwete wakati wa Mazishi ya Marehemu Mzee Selemani Mrisho Kikwete, kijijini Msoga, Chalinze, wilayani Bagamoyo mkoa wa Pwani leo Machi 5, 2016.

  PICHA NA IKULU

No comments: