Monday, March 14, 2016

Mh. Paul Makonda amshukuru Mungu kwa kutimiza mwaka mmoja kazini

Mhe.Paul Makonda siku ya leo alikuwa anatimiza mwaka mmoja tangu ateuliwe kuwa mkuu wa Walaya Kinondoni,asubuhi ya leo katika Ibada Kanisani Living Water Center Ministry Kawe alipolelewa kiroho na anapo abudu alikuja kumshukuru Mungu na kutoa sadaka ya shukrani kwa hatua ambayo amefika.

Katika Ibada hiyo Mh Paul Makonda aliongozana na Mkee wake alipopewa kuzungumza alisema anamshukuru Mungu kwa kutimiza mwaka tangu ateuliwe kuwa Mkuu wa Wilaya Kinondoni,alisema haikuwa raisi kwake ila Mungu amemuwezesha,akaongeza kwa kusema "usishindwe kufanya mambo ya kimaendeleo kwa changamoto za kimazingira au chochote kama kwake ambavyo imekuwa ikionekana".

Mapema akimkaribisha kuzungumza Mhe.Paul Makonda Kiongozi wa Kanisa hilo Apostle Onesmo Ndegi alikuwa anaelezea jinsi ambavyo amemlea kiroho Mh.Makonda hata kabla ya kuingia kuwa mtumishi wa serikali jinsi alivyokuwa mbunifu wa shughuli mbalimbali hivyo kinachofanyika leo sio kipya kwake.

Baada ya Ibada hiyo ya shukrani Bwana akatenda zaidi kwa kumfanya kuwa Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam.

Hongera Mkuu wa Mkoa Paul Makonda kwa kuteuliwa kuwa Mkuu mpya wa Mkoa wa Dar es saam 
Maombi yalifanyika kwake na mke wake ili Mungu amtangulie katika utumishi wake serikalini .
Apostle Onesmo Ndegi,Mke wake Lilian Ndegi na Mch. Peace Matovu wakifanya maombi kwa Mh. Makonda .


Mh. Paul Makonda alipokuwa akizungumza .
Kiongozi wa Kanisa la Living Water Centre Kawe Apostle Onesmo Ndegi 
Apostle Onesmo Ndegi Kiongozi wa Kanisa la Living Water Centre alipokuwa akiwaeleza waumini kuhusu Mh. Paul Makonda 
Apostle Onesmo Ndegi Kiongozi wa Kanisa la Living Water Centre alipokuwa akiwaeleza waumini kuhusu Mh. Paul Makonda .
Mh. Paul Makonda akiwa na Mke wake akimshukuru Mungu 
Mh. Paul Makonda akiwa akifafanua jambo .

No comments: