Wednesday, March 16, 2016

MADAKTARI BINGWA WA AFYA YA KINYWA NA MENO WAFURAHISHWA NA HALI YA AFYA YA KINYWA NA MENO KWA WATOTO WA KITUO CHA BUHANGIJA MKOANI SHINYANGA, WATOTO 157 WACHUNGUZWA

   Daktari Bingwa wa Kinywa na Meno wa Hospitali ya Taifa Muhimbili, Conrad Mselle  akimfanyia  usafi wa nywele  mmoja wa watoto wanao lelewa katika Kituo cha watoto wenye ulemavu wa ngozi waliopo Buhangija Mkoani shinyanga walipofika katika kituo hicho kwa mwendelezo wa Wiki ya Afya ya Kinywa na Meno ambapo kilele chake ni Machi 20, Mkoani Morogoro. (PICHA ZOTE NA KHAMISI MUSSA, MKOANI SHINYANGA, BUHANGIJA)
  Daktari Bingwa wa Kinywa na Meno wa Hospitali ya Taifa Muhimbili, Conrad Mselle  akimfanyia uchunguzi wa Afya ya Kinywa na Meno Mwanafunzi wa Darasa la pili  Lucia  Eliasi wa Kituo cha watoto wenye ulemavu wa ngozi kilichopo Mkoani Shinyanga, Buhangija   ambapo ni mwendelezo wa wiki ya kinywa na meno duniani na kwa leo wameonwa  watoto157 na kesho ni mwendelezo wawale waliokutwa na matatizo.

 Daktari bingwa wa Afya ya Kinywa na Meno  Hospitali ya Mkoa wa Shinyanga Dk. Nuru Mpuya  na akimwakilisha Mganga Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga  Dk. Ntuli Kapologwe, akizungumza jambo, kushoto ni Kiongozi wa Msafara Dk.  Arnold Mtenga
  msimamizi wa Kituo cha Buhangija na Mwalimu wa Elimu Maalum na watoto wasioona,  Sasu Nyanga , akiwakaribisha Madaktari bingwa wa Afya ya Kinywa na Meno
 Daktari Bingwa wa Afya ya Kinywa na Meno wa  Wilaya ya Ngara Mkoani Kagera akitoa neno la shukrani kwa uongozi wa Kituo hicho kwa Mapokezi na uongozi huo kuboresha mambo waliyoyaomba mwaka jana   yametekelezeka, mfano,kuwekewa kituo cha afya ya kinywa na meno eneo hilo.
 Mhudunu wa Afya Mwandamizi, Scolastica Sawaki (kushoto) akimpatia Dawa ya kujipata Esther Gada (kulia) mara alipofika katika Zahanati  iliyopo kituoni hapo , ambapo mwanafunzi huyo amefadhikiwa na Claire Grubbs kutoka America na kufadhili mambo mengi shuleni hapo kwa kusomesha baadhi ya watoto Veta wengine  kwa lengo la kujifunza , Kutengeneza Batic, ufundi wa Cherehani, utengenezaji wa sabuni, anaye shuhudia ni   Mhudunu wa Afya Mwandamizi wa kituoni hapo, Felister Jagadi


 kiongozi wa msafara kutoka katika hospitali ya Taifa Muhimbili Dk. Arnold Mtenga, akizungumza na waandishi wa habari (hawapo pichani) alipokuwa akiushukuru uongozi wa kituo hicho kwa mambo muhimu waliyoyaomba yafanyike na uongozi wa kituo umeteketeza na kuzidi kuwaomba mara wanapo hitaji msaada kwa watoto haoa wasisite kutoa taarifa na wameonwa watoto 157


Baadhi wa watoto wakimlilia Mmoja wa Madaktari wa Afya ya Kinywa na Meno

No comments: