Monday, March 21, 2016

Dkt. Shein atangazwa Mshindi katika Uchaguzi wa Marudio Zanzibar, leo

Mwenyekiti wa Tume ya Uchaguzi Zanzibar Jecha Salim Jecha alipokuwa akitangaza matokeo ya Uchaguzi Mkuu wa marudio jana katika ukumbi wa Salama Bwawani Mjini Unguja,ambapo Mgombe wa Urais wa Chama cha Mapinduzi CCM Dk.Ali Mohamed Shein kaibuka kushinda uchaguzi huo.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein akiwa mgombea Urais wa Zanzibar kwa kipindi cha pili cha Uongozi kupitia CCM na Mkewe Mama Mwanamwema Shein wakishangilia kwa makofi wakati alipotangazwa kuwa mshindi na Mwenyekiti wa Tume ya Uchaguzi Zanzibar Jecha Salim Jecha jana katika ukumbi wa Salama Bwawani Mjini Unguja.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein akiwa mgombea Urais wa Zanzibar kwa kipindi cha pili cha Uongozi kupitia CCM na Mkewe Mama Mwanamwema Shein wakipongezwa na Mgombea wa Urais kupitia Chama cha ACT-Wazalendo Bw,Khamis Iddi Lila (wa pili kulia) baada ya kutangazwa mshindi wakati matokeo ya uchaguzi huo jana katika ukumbi wa Salama Bwawani Mjini Unguja.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein akiwa mgombea Urais wa Zanzibar kwa kipindi cha pili cha Uongozi kupitia CCM akipongezwa na Watoto wake baada ya kutangazwa mshindi wakati wa matokeo ya uchaguzi huo jana katika ukumbi wa Salama Bwawani Mjini Unguja.
Mgombea wa Urais kupitia Chama cha ADC Bw,Hamad Rashid Mohammed akitoa shukurani kwa niaba ya Vyama mbali mbali vilivyoshiriki uchaguzi wa marudio baada ya kutangazwa mshindi na kukabidhiwa Cheti rasmi cha ushindi na Mwenyekiti wa Tume ya Uchaguzi Zanzibar Jecha Salim Jecha jana katika ukumbi wa Salama Bwawani Mjini Unguja.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein (kulia) akiwa mgombea Urais wa Zanzibar kwa kipindi cha pili cha Uongozi kupitia CCM akipokea cheti maalum cha Ushindi wa Uchaguzi wa marudio kutoka Mwenyekiti wa Tume ya Uchaguzi Zanzibar Jecha Salim Jecha wakati wa utoaji wa matokeo ya uchaguzi huo yaliyotolewa jana katika ukumbi wa Salama Bwawani Mjini Unguja
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein akiwa mgombea Urais wa Zanzibar kwa kipindi cha pili cha Uongozi kupitia CCM akionesha Cheti maalum cha Ushindi baada ya kukabidhiwa Mwenyekiti wa Tume ya Uchaguzi Zanzibar Jecha Salim Jecha wakati wa utoaji wa matokeo ya uchaguzi huo yaliyotolewa jana katika ukumbi wa Salama Bwawani Mjini Unguja.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein akiwa mgombea Urais wa Zanzibar kwa kipindi cha pili cha Uongozi kupitia CCM akisalimiana na Wagombea wa Vyama vya Siasa baada ya kutangazwa mshindi jana na Mwenyekiti wa Tume ya Uchaguzi Zanzibar Jecha Salim Jecha wakati wa utoaji wa matokeo ya uchaguzi huo yaliyotolewa katika ukumbi wa Salama Bwawani Mjini Unguja.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein akiwa mgombea Urais wa Zanzibar kwa kipindi cha pili cha Uongozi kupitia CCM akisalimiana na Mgombea wa Urais kupitia Chama cha ADC Bw,Hamad Rashid baada ya kutangazwa mshindi na kukabidhiwa Cheti rasmi cha ushindi na Mwenyekiti wa Tume ya Uchaguzi Zanzibar Jecha Salim Jecha wakati wa utoaji wa matokeo ya uchaguzi huo yaliyotolewa jana katika ukumbi wa Salama Bwawani Mjini Unguja.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein akiwa mgombea Urais wa Zanzibar kwa kipindi cha pili cha Uongozi kupitia CCM akipongezwa na Mgombea wa Urais kupitia Chama cha AFP Said Soud Said baada ya kutangazwa mshindi na kukabidhiwa Cheti rasmi cha ushindi na Mwenyekiti wa Tume ya Uchaguzi Zanzibar Jecha Salim Jecha wakati wa utoaji wa matokeo ya uchaguzi huo yaliyotolewa jana katika ukumbi wa Salama Bwawani Mjini Unguja.
Baadhi ya Viongozi wa Chama cha Mapindiuzi (CCM) na Wananchi na Vyma vya Upinzani waliohudhuria katika hafla ya utolewaji wa matokeo ya Uchaguzi Mkuu wa Marudio katika ukumbi wa Salama Bwawani Mjini Unguja jana.
Viongozi mbali mbali wa CCM na vyama vya upinzani wakishuhudia matokeo ya uchaguzi Mkuu wa marudio yaliyotolewa jana na Mwenyekiti wa Tume ya Uchaguzi Zanzibar Jecha Salim Jecha (hayupo pichani) katika ukumbi wa Salama Bwawani Mjini Unguja.
Viongozi mbali mbali wa vyama vya upinzani wakishuhudia matokeo ya uchaguzi Mkuu wa marudio yaliyotolewa jana na Mwenyekiti wa Tume ya Uchaguzi Zanzibar Jecha Salim Jecha (hayupo pichani) katika ukumbi wa Salama Bwawani Mjini Unguja,ambapo mshindi ametangazwa Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein akiwa mgombea Urais wa Zanzibar kwa kipindi cha pili cha Uongozi kupitia CCM.

No comments: