Thursday, March 10, 2016

BENKI YA CRDB YAIKOPESHA MANISPAA YA TEMEKE BIL.19.6

Na Mwandishi Wetu

MANISPAA ya Wilaya ya Temeke jijini Dar es Salaam, imepokea mkopo wa sh bilioni 19.6 kwa ajili ya kuwalipa fidia wakazi wa maeneo yatakayobomolewa ili kupisha mpango wa maendeleo na ustawi jiji.

Mkopo huo utakaolipwa kwa miaka sita una lengo la kufanikisha mradi mkubwa wa ujenzi na uboreshaji miundombinu ya jiji uitwao Dar es Salaam Metropolitan Development Project (DMDP).

Akizungumza na ujumbe wa viongozi na madiwani wa wilaya ya Temeke ulioongozwa na Mkuu wa Wilaya hiyo, Sophia Mjema, Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya CRDB, Dk. Charles Kimei iliyotoa mkopo huo alisema wanaunga mkono hatua za maendeleo zinazochukuliwa na Serikali Kuu na Tamisemi. 

Alisema fedha hizo zitatumika kwenye ujenzi wa mtandao wa barabara za lami wenye urefu wa kilometa 81.63 ujenzi wa masoko ya kisasa, vituo vya mabasi ya kisasa, upimaji wa viwanja 2,000 eneo al Kijichi na kuweka huduma za msingi, ujenzi wa mifereji ya mvua kilometa 22.4, dampo la kisasa eneo la Kisarawe na madaraja yanayounganisha kata mbalimbali.

“Tumetoa mikopo ya maendeleo kama huu kwenye halmashauri za Mwanza, Magu, Kinondoni, Mbeya na Mji wa Bukoba ambapo jumla ya sh trilioni tatu ambazo ni karibu sawa na bajeti ya maendeleo inayotengwa na serikali ambayo ni sh trilioni saba,” alisema Dk. Kimei.

Mjema aliwaonya watendaji wanaohusika na mradi huo kutoongeza majina ya wanaotakiwa kulipwa huku akisisitiza kwamba watakaobainika kuhujumu mradi huo na kutumia isivyostahili mkopo huo, watafukuzwa kazi na kufikishwa mahakamani.
 Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya CRDB, Dk. Charles Kimei akizungumza katika hafla ya kutia saini mkataba wa mkopo wa shs. bilioni 19.6 kwa ajili ya ulipaji fidia kwa wananchi wanaopisha mradi wa uboresha miundombinu katika Mamlaka za Serikali za Mitaa za jijini la Dar es Salaam (DMDP). (Picha ha Francis Dande)
 Mkurugenzi wa Masoko, Utafiti na Huduma kwa Wateja wa Benki ya CRDB akizungumza katika hafla hiyo.
Mkuu wa Wilaya ya Temeke, Sophia Mjema akizungumza katika hafla ya kutia saini mkataba wa mkopo wa shs. bilioni 19.6 kwa ajili ya ulipaji fidia kwa wananchi wanaopisha mradi wa uboresha miundombinu katika Mamlaka za Serikali za Mitaa za jijini la Dar es Salaam (DMDP).
Baadhi ya watumishi wa Manispaa ya Temeke.
 Baadhi ya wafanyakazi wa Benki ya CRDB.
 Baadhi ya Wakurugenzi wa Benki ya CRDB wakiwa katika hafla hiyo.
 Baadhi ya Maofisa wa Benki ya CRDB wakiwa katika hafla hiyo.
 Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya CRDB, Dk. Charles Kimei (kushoto), Naibu Mkurugenzi wa benki hiyo, Naibu Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya CRDB Bw. Saugata Bandyopadhya.
 Meya wa Manispaa  ya Temeke, Abdallah Chaurembo (kulia), Mkurugenzi wa Manispaa ya Temeke, Photidas Kagimbo (wa pili kulia), wakiwa katika hafla hiyo.
Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya CRDB, Dk. Charles Kimei (wa tatu kushto, akikabidhi Mkuu wa Wilaya ya Temeke, Sophia Mjema mfano wa hundi yenye thamani ya Shs. Bilioni 19.6 kwa ajili ya uboresha wa miundombinu katika Mamlaka zaSerikali za Mitaa za Jijini la Dar es Salaam.


 Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya CRDB, Dk. Charles Kimei (kulia), akibadilishana hati na Meya wa Manispaa ya Temeke, Abdallah Chaurembo baada ya kusaini mkataba wa mkopo wa shs. bilioni 19.6 katika hafla iliyofanyika jijini Dar es Salaam. Katikati anayeshuhudia ni Mkuu wa Wilaya ya Temeke, Sophia Mjema. 

No comments: