Wednesday, March 16, 2016

BARABARA ZA MKOA WA PWANI ZAHARIBIWA NA MVUA ZINAZOENDELEA KUNYESHA KATIKA MAENEO MBALI MBALI NCHINI

Makamu Mwenyekiti wa kikao cha bodi ya barabara Mkoa wa Pwani Ridhiwani Kikwete ambaye pia ni Mbunge wa Jimbo la Chalinze akifafanua jambo katika kikao hicho kilichofanyika kwenye ukumbi wa ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Pwani.


NA VICTOR MASANGU, PWANI  

IMEELEWA kwamba kutokana  na mvua zinazoendelea kunyesha katika maeneo mbali mbali hapa nchini zimeweza kusababisha uharibifu mkubwa wa miundombinu ya barabara  na madaraja katika baadhi ya maeneo ya mkoani Pwani hali ambayo imekuwa ni kero kubwa  kwa wananchi kutokana  na magari kukwama hivyo  kutokupitika kwa urahisi.

Hayo yamesemwa  na  Mhandisi mkuu wa kitengo  cha mipango kutoka Wakala wa barabara Tanroad Mkoa wa Pwani Zuhura Amani wakati akiwakilisha taarifa ya utekelezaji  wa kazi za matengenezo na miradi ya maendeleo kwa wajumbe  wa kikao cha bodi ya barabara cha Mkoa, ambapo amesema kuwa kuharibika kwa miundombinu hiyo  kunarudisha nyuma jitihada za serikai katika kuleta huduma kwa jamii.

Zuhura alisema    kuwa jumla ya kiasi cha shilingi bilioni 20.9 zilipangwa kutumika kwa ajili ya matengenezo ya barabara kwa kipindi cha mwaka wa fedha wa 2014 hadi 2015 lakini kutokana na kuwepo kwa ufinyu wa bajeti zoezi hilo halikuweza kufanikiwa kwa wakati uliopangwa.

Meneja wa wakala wa barabara Tanroad Mkoa wa Pwani Tumaini Salakikye akitolea ufafanuai na kujibu maswali yalioulizwa na wajumbe wa kikao hicho juu ya miundombinu ya barabara.

Kwa upande wao wajumbe waliohudhuria  katika kikao hicho  akiwemo Mwenyekiti wa CCM  katika Wilaya ya Kibaha Mji,Maulid Bundala  pamoja na Katibu msaidizi wa Mkoa wa Pwani  Shangwe Twamala walisema hai hiyo ya ubovu wa barabara inachangia kwa kiasi kikubwa kukwama kwa magari hivyo kupelekea usumnufu mkubwa hasa katika kipindi cha mvua.

 Nao baadhi wa wabunge wa Mkoa wa Pwani akiwemo Ridhiwani Kikwete Mbunge wa Jimbo la Chalinze ambaye ndio alikuwa makamu Mwenyekiti katika kikao hicho alisema kwamba baadhi ya maeneo ya barabara kwa sasa zipo katika hali mbaya ktokana na nyingine kupita kwake ni vigumu kutokana na kuwa na mashimo mengi.

“Kwa hii kwa kweli Meneja na timu yako inabidi kuliangalia kwa macho matatu kwani kuna baadhi ya barabara nyingine katika Mkoa wetu wa Pwani zipo katika hai mbaya sana maana wakati mwingine nashindwa kuelewa tatizo ni nini kwa suala hili naomba mfanya jitihada za kufanya ukarabati ili barabara zetu ziweze kupitaka kwa urais,”alisema Ridhione.
Mbunge wa Jimbo la Rufiji Mohamed Mchengerwa akichangia hoja katika kikao hicho cha bodi ya barabara.

  Kwa upande wake Mbunge wa Jimbo la Rufiji Mohamed Mchengerwa alisema kwamba katika jimbo lake kuna barabara ni muhimu sana ya kutoka Nyamwage kulelekea Utete ambapo ndipo makao makuu wa Wilaya hiyo inahitajika ifanyiwe matengenezo ili iweze kupitika kwa urahisi.

“Asilimia 19 la pato la Taifa inategemea katika Wilaya ya Rufiji kutokana na misitu iiyopo hivyo kunahitajika juhudi za makusudi kabisa kuhakikisha barabara ambazo ni kiunganishi kikubwa zifanyiwe ukarabati na zingine ziwekwe katika kiwango cha lami ili kuweza kuleta chachu ya maenedlea kwa wananchi wa rufiji na Taifa zima kwa ujumla,” alisema Mchengerwa.

 Akijibu malalamiko hayo Meneja wa wakala wa barabara Tanroad Mkoa wa Pwani Tumaini Salakikye amekiri kuwepo kwa hali hiyo na kuongeza kwamba changamoto kubwa inayowakabili katika utekelezaji wa majukumu yao  ni kutokana na bajeti kuwa ndogo.

Barabara zenye kiwango cha changarawe na  udongo katika baadhi ya maeneo katika Mkoa wa Pwani kwa sasa  zimeharibika kutokana na mvua zinazoendelea kunyesha katika maeneo mbali mbali hivyo kunahitajika nguvu ya makusudi kutoka serikalini ili ziweze kufanyiwa matengenezo ya haraka.
Mwenyekiti wa halmashauri ya mji wa Kibaha Leornad Mlowe akitolea ufafanuzi kuhusiana na kero ya ubovu wa barabara katika Wilaya ya Kibaha.
Mbunge wa viti maalumu Mkoa wa Pwani Zainabu Vulu (kushoto) akiwa na wajumbe wengine waliohudhuria katika kikao hicho, wa kati kati ni Mwenyekiti wa halmashauri ya Wilaya ya Kisarawe Hamisi Dikupatile.(picha zote na Victor Masangu).

No comments: