Wednesday, February 24, 2016

WIZARA YA MAMBO YA NDANI YA NCHI AMUAGA MWAKILISHI MKAZI WA UNHCR, JOYCE MENDS-COLE

Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Charles Kitwanga (watatu kulia) akiwa na Mwakilishi Mkazi wa Shirika la Kimataifa la Kuhudumia Wakimbizi (UNHCR) nchini, anayemaliza muda wake, Joyce Mends-Cole (wapili kushoto), Katibu Mkuu wa Wizara hiyo, Meja Jenerali Projest Rwegasira (kulia), Naibu Katibu Mkuu, Balozi Simba Yahya (kushoto) na Mkurugenzi wa Idara ya Wakimbizi, Harrison Mseke (wapili kulia) wakielekea katika hafla fupi iliyoandaliwa na Wizara hiyo kwa ajili ya kumuaga Mwakilishi wa UNHCR nchini, iliyofanyika katika Hoteli ya Serena, jijini Dar es Salaam leo.
Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Charles Kitwanga akizungumza katika hafla ya kumuaga Mwakilishi Mkazi wa Shirika la Kimataifa la Kuhudumia Wakimbizi (UNHCR) nchini, anayemaliza muda wake, Joyce Mends-Cole (watatu kulia). Katika hotuba yake fupi, Waziri Kitwanga alimshukuru Mwakilishi huyo kwa ushirikiano wake mzuri kati ya Wizara na UNHCR, pia alimtakia safari njema na mafanikio mema arudipo nyumbani kwake. Joyce anatarajia kustaafu rasmi katika nafasi hiyo mwezi ujao. Wanne kulia ni Naibu Waziri wa Wizara hiyo, Injinia Hamad Masauni, kushoto aliyekaa ni Katibu Mkuu, Meja Jenerali Projest Rwegasira, na Naibu Katibu Mkuu, Balozi Simba Yahya.
Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Charles Kitwanga (kushoto) akimkabidhi zawadi ya picha Mwakilishi Mkazi wa Shirika la Kimataifa la Kuhudumia Wakimbizi (UNHCR) nchini, anayemaliza muda wake, Joyce Mends-Cole, kwa ajili ya kumbukumbu yake kutokana na ushirikiano mzuri kati ya Shirika lake la UNHCR na Wizara. Hafla hiyo fupi ya kumuaga iliyoandaliwa na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi ilifanyika katika Hoteli ya Serena, jijini Dar es Salaam.
Mwakilishi Mkazi wa Shirika la Kimataifa la Kuhudumia Wakimbizi (UNHCR) nchini, anayemaliza muda wake, Joyce Mends-Cole akimshukuru Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Charles Kitwanga (wapili kushoto) pamoja na viongozi wengine wa Wizara hiyo, kwa ushirikiano mkubwa waliompa wakati anaiongoza UNHCR. Pia katika hotuba yake, Joyce alimpongeza Rais John Magufuli kwa uongozi wake mzuri pamoja na ushirikiano mkubwa wanaoupata kutoka katika Serikali yake. Wakwanza kushoto ni Katibu Mkuu wa Wizara hiyo, Meja Jenerali Projest Rwegasira. Watatu kushoto ni Katibu Mkuu wa Ofisi ya Makamu wa Rais, Mbarak Abdulwakil ambaye aliwahi kuwa Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi. Wapili kulia ni Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Balozi Simba Yahya, na Wanne kushoto ni Mkurugenzi wa Idara ya Wakimbizi, Harrsion Mseke.
Mkurugenzi wa Idara ya Wakimbizi, Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Harrsion Mseke akizungumza katika hafla ya kumuaga Mwakilishi Mkazi wa Shirika la Kimataifa la Kuhudumia Wakimbizi (UNHCR) nchini, anayemaliza muda wake, Joyce Mends-Cole (watatu kulia). Katika hotuba yake, Mseke alimshukuru Joyce kwa ushirikiano wake mkubwa aliouonyesha wakati wa uongozi wake. Wapili kushoto ni Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Charles Kitwanga ambaye aliiongoza hafla fupi iliyofanyika katika Hoteli ya Serena, jijini Dar es Salaam. Wanne kulia ni Naibu Waziri wa Wizara hiyo, Injinia Hamad Masauni. Kushoto ni Katibu Mkuu wa Wizara hiyo, Meja Jenerali Projest Rwegasira. Watatu kushoto ni Katibu Mkuu wa Ofisi ya Makamu wa Rais, Mbarak Abdulwakil ambaye aliwahi kuwa Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi. Wapili kulia ni Naibu Katibu Mkuu, Balozi Simba Yahya.
Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Injinia Hamad Masauni (kushoto) akimuaga Mwakilishi Mkazi wa Shirika la Kimataifa la Kuhudumia Wakimbizi (UNHCR) nchini, anayemaliza muda wake, Joyce Mends-Cole mara baada ya kumaliza sherehe fupi iliyoandaliwa na Wizara ya kumuaga kiongozi huyo wa UNHCR. Hafla hiyo fupi ilifanyika katika Hoteli ya Serena, jijini Dar es Salaam leo na kuhudhuriwa na Viongozi Wakuu wa Wizara akiwemo Waziri wa Wizara hiyo, Charles Kitwanga.
Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Charles Kitwanga (wanane kushoto), Naibu Waziri wa Wizara hiyo, Injinia Hamad Masauni (watano kulia), Katibu Mkuu wa Wizara hiyo, Meja Jenerali Projest Rwegasira (wasaba kushoto), Katibu Mkuu wa Ofisi ya Makamu wa Rais, Mbarak Abdulwakil ambaye aliwahi kuwa Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi (wanne kulia), Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Balozi Simba Yahya (wanne kushoto), Mwakilishi Mkazi wa Shirika la Kimataifa la Kuhudumia Wakimbizi (UNHCR) nchini, anayemaliza muda wake, Joyce Mends-Cole (wasita kulia) wakiwa katika picha ya pamoja na Maafisa wa Wizara pamoja wa UNHCR mara baada ya hafla fupi ya kumuaga Joyce, iliyofanyika katika Hoteli ya Serena, Dar es Salaam leo. Picha zote na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.

No comments: