Monday, February 1, 2016

Wanakijiji Mungere kupewa bure miche ya miti kukabili maafa ya upepo

Alaigwanani wa mila, Saibulu Olemariki akimuongoza Mkurugenzi wa Idara ya uratibu maafa Ofisi ya Waziri Mkuu, Brigedia Jenerali Mbazi Msuya kukagua athari za upepo kwa mashamba ya migomba kijiji cha Mungere, wilayani Monduli, tarehe 31 Januari , 2016.
Alaigwanani wa mila, Saibulu Olemariki akionesha sehemu ya mgomba iliyoanguka baada ya upepo mkali kuathiri shamba lake la ekari 3, wakati Idara ya uratibu maafa Ofisi ya Waziri Mkuu, ilipokuwa ikikagua athari za maafa hayo katika kijiji cha Mungere, wilayani Monduli, tarehe 31 Januari , 2016.
akimueleza jambo Alaigwanani wa mila, Saibulu Olemariki mara baada ya kukagua athari za upepo kwa mashamba ya migomba katika kijiji cha Mungere, wilayani Monduli, tarehe 31 Januari , 2016.
Alaigwanani wa mila, Saibulu Olemariki akimuonesha Mkurugenzi wa Idara ya uratibu maafa Ofisi ya Waziri Mkuu, Brigedia Jenerali Mbazi Msuya baadhi ya ndizi zilizo katwa kwenye migomba iliyoanguka baada ya upepo mkali kuathiri shamba lake la ekari 3, wakati Idara ya uratibu maafa Ofisi ya Waziri Mkuu, ilipokuwa ikikagua athari za maafa hayo katika kijiji cha Mungere, wilayani Monduli, tarehe 31 Januari , 2016.
Alaigwanani wa mila, Saibulu Olemariki akimshika bega Mkurugenzi wa Idara ya uratibu maafa Ofisi ya Waziri Mkuu, Brigedia Jenerali Mbazi Msuya kama ishara ya kumshukuru mara baada ya kukagua athari za maafa ya upepo mkali katika kijiji cha Mungere, wilayani Monduli, tarehe 31 Januari , 2016.
Alaigwanani wa mila, Saibulu Olemariki akimuonesha Mkurugenzi wa Idara ya uratibu maafa Ofisi ya Waziri Mkuu, Brigedia Jenerali Mbazi Msuya maeneo upepo mkali ulioleta maafa katika mashamba ya migomba katika kijiji cha Mungere, wilayani Monduli, mara baada ya kukagua athari za maafa hayo , tarehe 31 Januari , 2016. (Picha na Ofisi ya Wazairi Mkuu )

Na. Mwandishi maalum

Serikali kupitia Ofisi ya Waziri Mkuu, Idara ya Uratibu maafa itatoa mbegu bure za miti ili kukabili maafa ya upepo mkali kwa wakazi 3,000 wa kijiji cha Mungere, ambao mashamba yao ya migomba yalikumbwa na maafa ya upepo mkali uliosababisha ekari 250 kati ya ekari 300 za mashamba hayo kuathiriwa  na upepo huo.

Akiongea wakati wa ziara ya kukagua athari za maafa hayo katika kijiji cha Mungere, wilayani Monduli Tarehe 31 Januari, 2016, Mkurugenzi wa Idara ya uratibu maafa Ofisi ya Waziri Mkuu, Brigedia Jenerali Mbazi Msuya amebainisha kuwa serikali imeamua kuwagawia bure mbegu za miti itakayopandwa kwa kuzunguka mashamba yao ili waweze kukabili maafa hayo ya asili.

“Ofisi ya Waziri Mkuu idara ya uratibu maafa inalojukumu la kuratibu shughuli za maafa katika hali ya kujiandaa, kuzuia, kukabili na kurudisha hali ya kawaida pindi maafa yanapotokea kwa hapa kijijini Mungere tumeamua kukabili maafa yatokanayo na upepo kwa kuwapa wakulima wa zao la ndizi waweze kuipanda miti hiyo itakayowezesha kupunguza kasi ya upepo mkali ambao husababisha migomba kuanguka katika mashamba yao.” amesema Brig. Jen. Msuya

Msuya aliongeza kuwa  idara yake  itatoa chakula cha msaada kwa waathirika wa maafa hayo ili waweze kuwa na chakula cha kutumia wakati  baadhi ya migomba yao iliyoathirika ikiendelea kuchipuka  na mingine kukomaa ambapo wataweza kupata chakula lakini pia  na kujipatia fedha kwa kuuza zao hilo.

Awali akiongea katika ziara hiyo, Alaigwanani wa mila, Saibulu Olemariki alifafanua kuwa upandaji miti ndio njia pekee ya kuwajengea uwezo wakulima wa zao la ndizi kuweza kukabili maafa ya upepo katika kijiji hicho kwa kuwa mashamba yao yamekuwa yakikumbwa na maafa ya upepo mkali ambao umekuwa ukiangusha migomba ambayo tayari inakuwa imeshabeba ndizi kubwa na zilizo komaa.

“Kama kiongozi wa kimila nitawahamasisha wanakijiji wenzangu hasa wakulima wa mashamba ya migomba kuhakikisha kuwa kila mtu anazungusha miti ya kutosha katika shamba lake lakini pia kuhakikisha kuwa miti hiyo inatunzwa kwa kuimwagilia maji na kutokatwa ovyo.” alisisitiza Alaigwanani Olemariki.

Alaigwanani Olemariki alieleza masuala yanayo kuwa kikwazo kwa wakulima hao kuwa ni  miundo mbinu ya barabara na Umwagiliaji kwa kueleza  kuwa pamoja na kijiji hicho kuwa na maafa ya upepo ambayo huathiri mashamba yao ya migomba lakini pia miundo mbinu ya barabara imekuwa kikwazo cha wakulima hao kwa kushindwa kusafirisha ndizi ili waweze kulifikia soko kwa wakati .

“Tunaomba serikali iweze kuiboresha barabara inayokuja kijijini hapa ili kuweza kuhamasisha wafanyabiashara wengi kufika kijijini hapa kununua ndizi kwa kuwa kama tunakuwa hatujapatwa na maafa tunaouwezo wa kuzalisha ndizi nying na hili niombe serikali kuwa sisi tunazalisha ndizi nyingi amabazo tukijengewa mazingira mazuri ya kilimo chetu ikiwa ni pamoja na kujengewa mfereji bora wa maji tunao uwezo wa kuilisha Monduli nzima na hata nje ya hapo.” alisisitiza Alaigwanani Olemariki.

No comments: