Wednesday, February 24, 2016

SHIRIKA LA ETIHAD LAZIDI KUKUA NCHINI INDIA BAADA YA KUVUNJA REKODI YA IDADI YA ABIRIA.

SHIRIKA  la Ndege la Etihad na mshirika wake Jet Airways wametangaza ongezeko la asilimia 63 la wasafiri wanaoenda na kuondoka nchini India. Ongezeko hilo limeipa nguvu mpya ushirikiano huo na kuimarisha azma yake ya kuwa moja kati ya ndege zenye soko kubwa.

Kwa pamoja, mashirika haya yameweka rekodi ya kuasafirisha abiria milioni 3.3 baina ya vituo vyake vya Abu Dhabi na India mwaka 2015, kwa kulinganisaha mashirika hayo yalisafirisha abiria  milioni 2 ndani ya miezi 12 iliyopita.

Etihad limekuwa shirika geni la kwanza lililowekeza katika shirika la Ndege la Kihindi chini ya Sheria ya Uwezekaji kutoka nje ya nchi ya India ambapo liliwekeza dola za Kimarekani milioni 750 katika Jet Airways ili kupata hisa asilimia 24 mwaka 2013. Shirika la Etihad leo lina ndege 175 kwenda miji 11 India kila wiki. Mitandao ya Etihad na Jet Airways kwa pamoja imewezesha safari za ndege 250 kila wiki katika ya Abu Dhabi na miji 15 ya India.

Pamoja, mashirika haya yanaongoza katika soko kwa usafiri kati ya India na UAE. Kwa kuangalia soko la kimataifa, wanasafirisha asilimia 20 ya abiria kutoka na kwenda India na hii inawakilisha hisa kubwa ya sekta usafiri wa anga nchini India.

Kwa kuongezea, Etihad inafanya operesheni ya uchukuzi mara 14 kila wiki kwenda miji 4 India na inaingiza na kutoa tani 120,000 za mizigo kila mwaka- hii inawakilisha asilimia 9 ya jumla ya soko la kimataifa.

Takwimu hizi zinaonesha umuhimu wa Shirika hili katika soko la India - moja katika ya vyanzo vikubwa vya biashara kwa Etihad- kwa ushirikiano wake mkubwa na Jet Airways na kuimarisha mahusiano kati ya UAE na India.

Mahusiano kati ya nchi hizi mbili ndio yalikuwa kiini cha mazungumzo yaliyotokea Mumbai na Delhi wiki iliyopita ambayo yalileta makubaliano mapya katika sekta mbalimbali ili kukuza mikakati na biashara za kiuchumi.

Biashara kati ya nchi hizi imetabiriwa kukua kwa zaidi ya asilimia 60 ndani ya miaka 5 ijayo kutoka kiwango chake cha sasa cha dola za Kimarekani bilioni 60, katika uwezekaji na bidhaa za kuagiza na kuuza nje katika sekta mbalimbali, zikiwemo; nishati, ulinzi, viwanda, kutengeneza ndege, afya, elimu, utalii, sayansi na teknolojia. Hivi sasa UAE ni mwekezaji wa kigeni wa kumi kwa ukubwa India.

James Hogan, Rais na Mkurugenzi Mkuu wa Etihad, alisema: “mahusiano kati ya UAE na India yanaendelea kukua kutokana na miaka mingi ya urafiki na dhamira ya kuimarisha uchumi, tamaduni na biashara. Etihad na Jet Airways wanatoa siti zaidi ya 44,000 kila wiki kati ya Abu Dhabi na India, sisi ni kati ya wachangiaji wakuu wa uchumi ya India. Kuna nafasi nyingi za ukuaji zaidi na tunatazamia kutumia fursa zilizopo kuendeleza operesheni zetu.

“Uwekezaji wetu katika Jet Airways ulilenga kuwa sehemu ya simulizi ya mafanikio ya India. Awali ya hili, Etihad ilikuwa inabeba asilimia 2 tu ya wasafiri wote wanaoingia na kutoka nchini India. Tumesaidia kuirudishia Jet Airways katika wigo la faida. Leo hii Jet Airways ni mshirika wetu wa kwanza kimapato huku wakichangia abiria kwa shirika la Etihad, wakati huo huo India ni chanzo cha kwanza cha abiria wa kimataifa kwenda Abu Dhabi.

Uwanja wa Kimataifa wa Abu Dhabi umekuwa kiunganishi cha msingi kwa usafiri wa anga kati ya India na dunia, wateja wameweza kusafiri kiurahisi na wana chaguo zaidi kupitia mizunguko mbalimbali kutoka India kwenda Abu Dhabi na kwingineko.

Tangu kuzindua safari kati ya Abu Dhabi na India kupitia Mumbai mwezi wa tisa mwaka 2004, shirika la Etihad limepanua uwepo wake India kwa kasi baada ya kuzindua njia nyingine kumi na kuongeza mizunguko katika sekta nyingi, zikiwemo safari 3 kwa siku katika njia saba. Kutoka Mei 1, Shirika litazindua operesheni kwenda Mumbai kwa kutumia Airbus A380.

Hivi sasa safari za ndege za Etihad kutoka Abu Dhabi zinafika sehemu zifuatazo India; Ahmedabad, Bengaluru, Chennai, Delhi, Hyderabad, Jaipur, Kochi, Kolkata, Kozhikode, Mumbai na Thiruvananthapuram. Jet Airways inaongeza vituo kwa kufika Pune, Lucknow, Goa na Mangalore pamoja na kuunganisha vituo vya ndani ya nchi.

Dhamira ya shirika la ndege la Etihad kwa India inaonekana katika ushiriki wake katika jumuiya ya biashara. Mwaka jana, shirika la Etihad lilikuwa mwanachama mwanzilishi wa Baraza la Biashara UAE huko India. Jumuiya hii inalenga kuhamasisha mahusiano kati ya vyombo vya biashara, kubadilishana mawazo na kukuza umoja wa kiuchumi kati ya UAE na India.


Akiongezea Bwana Hogan alisema: “India ni soko muhimu si tu kwa shirika letu bali pia kwa UAE yenyewe, hivyo tunaipokea fursa hii ya kuwa mwanachama mwanzilishi wa Baraza la Biashara la UAE nchini India. Ushirikiano huu wa kimkakati na Jet Airways unamaanisha wote tunaongeza wasafiri tutakaohudumia kati ya India na UAE. Tunatazamia kutumia ushirikiano huu ili uweze kuwa na mchango zaidi kwa Baraza la Biashara nchini India.”

“Kama shirika la usafiri wa anga, tuko katika nafasi nzuri kuwezesha biashara, na kuangalia fursa kubwa zilizopo kwa ajili ya uwekezaji India kutoka UAE, tunafurahia kuwa sehemu ya simulizi ya ukuaji wa India.”

Pamoja na hayo, Etihad na Jet Airways wanaingia kwenye mkataba wa pamoja wa kuwa washirika pekee na wadhamini wa Mumbai Indians, mabingwa wa ligi ya Pepsi Indian Premier (IPL) kwa mwaka jana. Mashirika haya yamedhamini matukio mengine ya kimichezo na kijumuiya, ikiwa ni pamoja na mara mbili kuleta kambi ya mafunzo ya Manchester City Football Club nchini India na kuwawezesha vijana wa chimbuko tofauti kupata mafunzo ya hali ya juu.

Mwezi ujao, shirika la Etihad litashiriki katika mkutano wa usafiri wa anga wa mwaka 2016 nchini India, mjini Hyderabad, mkutano na maonesho kwa ajili ya sekta ya usafiri wa anga India. Ikiwa umeandaliwa na Wizara ya Usafiri wa Anga na Shirikisho la Biashara na Viwanda India, tukio hili litatoa nafasi kwa shirika la Etihad kuungana na watengeneza sera, wataalamu wa usafiri wa anga na wadau wengine wakubwa katika sekta ya usafiri wa anga India.

Mpaka kufika mwaka 2020, abiria wa kitaifa na kimataifa wanaopitia viwanja vya ndege vilivyopo India wanategemewa kufika milioni 450. Shirika la Utalii Duniani la Umoja wa Kimataifa linatabiri zaidi ya wahindi milioni 50 watasafiri nje ya nchi kufika mwaka 2020. Shirika la ndege la Etihad limedhamiria kuhudumia watalii kutoka nje na ndani ya nchi ilikutimiza mikakati yake ya ukuaji.

No comments: