Monday, February 1, 2016

JAJI MKUU MOHAMED CHANDE OTHMAN ATOA SIKU SABA KWA MAHAKIMU 508 WATOE MAELEZO KWANINI WASIFUNGULIWE MASHITAKA KWA KUFANYA KAZI CHINI YA KIWANGO.

Jaji Mkuu wa Tanzania  Mohamed Chande Othman (katikati), akizungumza katika mkutano na waandishi wa habari (hawapo pichani), Dar es Salaam leo mchana , kuhusu utendaji wa mahakimu wa mahakama za hakimu mkazi, mahakama za wilaya na mahakama za mwanzo ambapo alitoa siku saba kwa mahakimu 508 watoe maelezo kwani ni wasifunguliwe mashitaka ya nidhamu na kuwajibishwa kwa kufanya kazi chini ya kiwango. Kushoto ni Jaji Mkuu wa Zanzibar, Omari Mallungu na kulia ni Jaji Kiongozi wa Tanzania, Shaban Omari Lila. Jaji Chande alitoa kauli hiyo kwenye maonyesho ya wiki ya Sheria yanayoendelea viwanja vya Mnazi Mmoja.
Jaji Mkuu wa Tanzania Mhe. Mohamed Chande Othman akikaribishwa kutembelea mabanda mbalimbali kwenye maonesho hayo.
Mkurugenzi Msaidizi Ukaguzi na Maadili Mahakama ya Tanzania, Warsha Ng'humbu (kushoto), akimuelekeza jambo Balbina Mrosso (kulia), kutoka Babati mkoani Manyara aliyetembelea banda la Idara ya Malalamiko kuomba msaada wa kisheria katika maonyesho hayo.
Jaji Mkuu wa Tanzania Mhe. Mohamed Chande Othman  akisoma moja ya daftari katika banda la Idara ya Malalamiko kwenye maonyesho hayo. Kulia ni Mkurugenzi Msaidizi Kitengo cha Malalamiko Mahakama ya Tanzania, Happiness Ndesamburo.
Jaji Mkuu wa Tanzania Mhe. Mohamed Chande Othman (kulia), akielekezwa jambo katika banda la Divisheni ya Biashara katika maonesho hayo. 

No comments: