Tuesday, January 26, 2016

STIKA ZA KUTOKOMEZA MAUAJI KWA WATU WENYE UALBINO ZA ZINDULIWA JIJINI DAR LEO.

 Kamanda wa Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam, Naibu Kamishna, Simon Sirro, akizungumza na wadau mbalimbali juu ya kufanisha uzinduzi wa Stika maalumu yenye ujumbe wa kutokomeza mauaji ya watu wenye Albinism,leo jijini Dar es Salaam.
 Kamanda wa Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam, Naibu Kamishna, Simon Sirro, akikata utepe kuashiria uzinduzi wa Stika maalumu yenye ujumbe wa kutokomeza mauaji ya watu wenye Albinism jijini Dar es Salaam,kulia ni Mwenyekiti wa Albno Enteprises of Dar es Salaam Michael Lugendo.
 Kamanda wa Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam, Naibu Kamishna, Simon Sirro, akupokea tuzo kutoka kwa Mwenyekiti wa Albino kutoka Enteprises of  Dar es Salaam, Michael Lugendo leo jijini Dar es Salaam.
 Kamanda wa Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam, Naibu Kamishna, Simon Sirro, akionesha Stika mara baada ya uzinduzi wa wa Stika maalum yenye ujumbe wa kutokomeza mauaji ya watu wenye Albinism,leo jijini Dar es Salaam.
 Sehemu ya maofisa mbalimbali wa Jeshi la Polisi waliofika katika uzinduzi wa Stika maalum yenye ujumbe wa kutokomeza mauaji ya watu wenye Albinism,leo jijini Dar es Salaam.

Waandishi wa habari wakimsikiliza Kamanda wa Polisi Kanda Maalimu ya Dar es Salaam, Naibu Kamishna, Simon Sirro, leo jijini Dar es Salaam.
(Picha na Emmanuel Massaka wa Globul ya jamii)

KAMANDA wa Polisi Kanda Maalimu ya Dar es Salaam, Naibu Kamishna, Simon Sirro, leo amezindua stika za kutokomeza mauaji kwa watu wenye albinism.

Kamanda Sirro amesema lengo la stika hizo ni kutoa elimu maeneo yote hasa katika mikoa ya Kanda ya ziwa ambapo mauaji ya albino yamekithiri.

Amesema stika hizo zitasambazwa nchi nzima kwasababu ipo mikoa mbalimbali bado ina mila potofu za kishirikina ambapo watu wanaamini kuwa akipata viungo vya albino atakuwa tajiri.

Amesema kuwa kusudi ni kutotoa elimu kwa njia ya stika ni kwamba zitabandikwa katika majumba, maofisini, kwnye magari, madukani, mashuleni, vyuoni, kwenye bodaboda na bajaji na elimu hiyo itamfikia hata yule mtanzania ambaye hana redio na runinga.

“Tuna kila sababu kuhakikisha kuwa kila mmoja anaishi kwa amani na kuwalinda ndugu zetu wenye ulemavu wa ngozi(Albino.

“Sisi kama jeshi la Polisi na vyombo mbalimbali vya dola tunawajibika kupata taarifa za wale wanaotafuta viungo vya albino tutahakikisha tunapata taarifa kabla ya tukio halijafanyika,” alisema Kamanda Sirro.

Amesema jeshi hilo litashirikiana na Viongozi wa Serikali za mtaa, viongozi wa dini zote pamoja na taasisi mbalimbali zenye kutetea haki za binadamu.

Kwa upande wake Mkurugenzi wa Taasisi ya AlbinoInterprises Dar es Salaam, Michael Lugendo, alisema lengo la stika hizo ni kutokomeza mauaji lwa watu wenye albinism na kazi hiyo inahitaji ushirikishwaji wa kila mtu.

Amesema hapa nchini albino wanakabiliwa na mauaji ya aina tatu ambayo ni mauaji ya kisaikolojia yanayomgusa kila mtu mwenye albinism ambayo yalianza pale vitendo vya kukata viungo vya albino vilipoibuka.

Kugendo amesema mauaji mengine ni yale yanayosababishwa na saratani ya ngozi ambayo hutokana na ukosefu wa mafuta ya ngozi na vikingia jua kulingana na mabadiliko ya tabia nchi, pamoja na mauaji ya kukatwa viungo ambavyo jamii jamii kubwa inawatambua hadi sasa wanaofanya vitendo hivyo.

Hata hivyo aliwataka viongozi wa dini, wanasiasa, wafanyabiashara kuwasaidia michango ili kuwezesha zoezizima la usambazaji stika hizo.

Pia taasisi hiyo ilimtunuku Kamanda Sirro tuzo ya amani na upendo pamoja na kutoa cheti cha kujali jamii kwa Shirika la Taifa la Hifadhi ya Jamii (NSSF).




Kamanda Sirro amesema kuwa tuzo hiyo ni mwanzo mzuri kwake na ina mpa moyo wa kuendelea kushirikiana na albino katika kutokomeza mauaji.

No comments: