Thursday, January 7, 2016

SIMU TV: HABARI KUTOKA TELEVISHENI

SIMUTV: Idara ya uhamiaji mkoani Mara yaeleza kukamata wahamiaji haramu 435 kwa mwaka 2015. https://youtu.be/pQ87ZTFT1AQ
    
SIMUTV: Wawekezaji wazawa katika sekta ya madini mkoani Geita waiomba serikali kuwaangalia kwa jicho la pekee kama inavyowaangalia wawekezaji kutoka nje ya nchi kwani wanaweza kuchangia pato la taifa.

SIMUTV: Mamlaka ya usafiri wa nchi kavu na majini SUMATRA yasema itaendelea kukusanya maoni ya nauli zinazopaswa kutumika katika mradi wa mabasi yaendayo haraka. https://youtu.be/1_cNGxtoXpw
  
SIMUTV: Halmashauri ya jiji la Mbeya huenda ikashindwa kufikia malengo iliyojiwekea ya kukusanya mapato kupitia vyanzo vyake vya ndani kufuatia mwikitikio mdogo kutoka kwa wananchi. https://youtu.be/uccZ_Xxopyo

  SIMUTV: Rais wa Zanzibar Dr.Shein asisitiza kuwa yeye ni kiongozi halali wa Zanzibar licha ya kufutwa kwa uchaguzi uliofanyika October mwaka jana huku akiwataka wanaopinga uwepo wake kwenda mahakamani.https://youtu.be/_3SRg4CY7Uc
    
SIMUTV: Wananchi walioathirika na mafuriko wilayani Kilosa mkoani Morogoro waanza kupata msaada wa chakula wakati huu wakihifadhiwa kwenye makazi ya dharura. https://youtu.be/kIPWSRrdNVE

SIMUTV: Waziri wa elimu alitaka baraza la mitihani nchini kutoa sababu zilizopelekea kubadilishwa kwa viwango vya ufaulu;https://youtu.be/u0_Mk2og43Y

SIMUTV: Madereva wa mabasi yanayofanya safari zake kati ya Mtwara na Dar es salaam wafanya mgomo kushinikiza madereva wenzao 3 waliokamatwa na polisi kuachiwa. https://youtu.be/X_F6_2hAY-Q
  
SIMUTV: Wabunge na madiwani wa jimbo la Ukonga na Segerea kesho wanatarajia kufungua shauri katika mahakama kuu kuzuia zoezi la bomoa bomoa jimboni humo. https://youtu.be/GB-gBgZTvm4

 SIMUTV: Zaidi ya wakazi 3,000 wanaoishi katika bonde la mto Msimbazi na maeneno mengine ya halmashauri ya Kinondoni wafurika mahakama kuu ya Tanzania kupinga zoezi la bomoa bomoa baada ya nyumba zao kuwekewa alama ya X. https://youtu.be/VA7K0aowr0w

SIMUTV: Baadhi ya wananchi wa kijiji cha Busolwa mkoani Geita wasimamisha msafara wa waziri wakimtaka asikilize kero zinazowakabili katika eneo lao ikiwemo kunywa maji yenye sumu. https://youtu.be/mohugB1-98o

 SIMUTV: Rais Magufuli akutana na kufanya mazungumzo na Rais mstaafu Benjamini Mkapa pamoja na waziri mkuu mstaafu Jaji Joseph Warioba ikulu jijini Dar es salaam. https://youtu.be/FpKeXdHMp8s
  
SIMUTV: Serikali yasitisha safari za meli ya MV.Serengeti kwa muda wa siku 3 kupisha matengenezo kufuatia hitilafu iliyojitokeza siku kadhaa zilizopita;https://youtu.be/QGZi_ekgRGg

 SIMUTV: Wafanyakazi wa kiwanda cha Play and Panel cha mkoani Tanga wamemuomba mkuu wa mkoa huo kuingilia kati mgogoro uliopo baina ya wafanyakazi hao na uongozi wa kiwanda hicho;https://youtu.be/Cu_Run5zd0w

 SIMUTV: Mkuu wa jeshi la polisi nchini IGP Mangu aongoza mamia ya waombolezaji katika mazishi ya aliyekuwa msaidizi wake, Marehemu Gerald Ryoba aliyefariki katika ajali ya maji pamoja na familia yake mkoani Dodoma;https://youtu.be/qRvQtjZMdOQ

 SIMUTV: Wanajeshi wa jeshi la wananchi JWTZ wameelezwa kuwa na wajibu mkubwa wa kujenga na kulinda amani ya nchi; https://youtu.be/ayOBnK-qPVs

SIMUTV: Shirika la viwango chini TBS latangaza kupambana na waingizaji na wasambaji wa mafuta ya petrol nchini yenye kiwango hafifu;https://youtu.be/EmcwPjdLxOw

 SIMUTV: inaelezwa kuwa mshambuliaji wa kimataifa toka Uganda anayekipiga katika ligi kuu ya nchini Denmark, Emanuel Okwi aanza kuzoea soka la Ulaya;https://youtu.be/6CG731L2bYI

SIMUTV: Shirika la riadha duniani IAAF limefungia Papa Massata Diack  kifungo cha maisha kutojihusisha na mchezo wa riadha;https://youtu.be/qRvQtjZMdOQ
  
SIMUTV: Serikali imewataka wananchi wote nchini waliojenga jirani na vyanzo vya maji kuondoka mapema; http; https://youtu.be/G93QsggSO4k

 SIMUTV: Inaripotiwa kuwa zaidi ya nyumba elfu kumi na sita jijini Dar es salaam zimewekwa alama za kubomolewa toka zoezi hilo lilipoanza;https://youtu.be/lPIca9clDY0

SIMUTV: Rais John Magufuli akutana na kufanya mazungumzo na viongozi wastaafu Ikulu jijini Dar es salaam; https://youtu.be/IBPJSGZIM0k

 SIMUTV: Serikali ya Zanzibar yaweka mikakati kwa lengo la kuwasadia vijana kujiimarisha kiuchumi na kurejesha maadili kwa wananchi visiwani humo;https://youtu.be/tarpGrJgKIg
  
SIMUTV: Serikali yaingiza kiasi cha fedha tasilimu za kitanzania jumla ya shilingi bilioni 18.77 katika akaunti za shule za msingi na sekondari nchini;https://youtu.be/u9jWqwTyUtg
  
SIMUTV: Timu ya Azam ya jijini Dar es Salaam imeangukia pua kwa kutandikwa goli 2 kwa 1 na timu ya Mafunzo ya visiwani Zanzibar katika michuano ya Kombe la Mapinduzi visiwani Zanzibar; https://youtu.be/lcXuViGv3_4

No comments: