Friday, January 8, 2016

LEO JANUARI 8,NI SIKU YA KUMBUKUMBU YA KUZALIWA KWA MWANZILISHI NA MMILIKI WA MALUNDE1 BLOG,IJUE HISTORIA YAKE HAPA

MENEJIMENTI na Wafanyakazi wa Malunde1 blog,kwa bashasha wanatoa salamu za pongezi kwa mwanzilishi wa Malunde1 blog,Fahari ya Shinyanga ndugu Kadama Malunde kwa kujaaliwa , leo Januari 08,2016;kuadhimisha siku ya kumbukumbu ya kuzaliwa kwake. 

Kadama Malunde aliyelelewa na wazazi wake kwa maadili ya kabila la Kisukuma ndiye mwanzilishi pia Mmiliki wa Malunde1 blog, alizaliwa katika kijiji cha Zobogo wilaya ya Shinyanga mkoani Shinyanga miaka kadhaa iliyopita. 

Wazazi wake waliamini kuwa elimu ndiyo urithi pekee utakaomfaa mtoto wao.

Mwaka 1995 alianza safari yake ya kujipatia Elimu,kwa kuanza darasa la kwanza katika Shule ya Msingi Bugisi wilaya ya Shinyanga,hadi mwaka 2001 alipohitimu Elimu hiyo ya msingi. 

Mwaka 2002 hadi 2005,alijiunga katika shule ya sekondari Kituli iliyopo wilayani Shinyanga kwa masomo ya kidato cha Kwanza hadi Nne;ndipo alipojiunga katika shule ya sekondari Ngudu iliyopo mkoani Mwanza kwa masomo ya kidato cha Tano na Sita mwaka 2006/2008.

Mwaka 2008/2011 alijiunga katika shule kuu ya Uandishi wa Habari na Mawasiliano ya Umma(SJMC) katika chuo kikuu cha Dar es salaam kwa ajili ya masomo ya Uandishi wa Habari(BA In Journalism).

Tangu mwaka 2009 Kadama Malunde amekuwa akifanya kazi katika vyombo mbalimbali vya habari,vikiwemo Mlimani Radio,Kahama fm,Radio Faraja Fm,Gazeti la The Hill Observer,Zanzibar leo na Mtanzania,ambapo katika baadhi ya vyombo vya habari aliwajibika katika nyadhifa za Mhariri wa Habari,Mtangazaji na Mwandishi wa Habari.

Mbali na kuwajibika kwa nyakati kadhaa katika vyombo hivyo vya habari,amemudu kuanzisha na kutumia muda mwingi zaidi kuendesha mtandao wa kijamii wa www.malunde1.blogspot.com pamoja na kuandikia gazeti la Mtanzania.

Aidha Kadama Malunde mwenye makazi yake mjini Shinyanga ni mwanachama wa Mtandao wa wamiliki wa blogu Tanzania(Tanzania Bloggers Network-TBN) lakini pia ndiye mwenyekiti wa Klabu ya Waandishi wa Habari mkoa wa Shinyanga(Shinyanga Press Club-SPC) tangu mwezi Julai 2015. 

Malunde, Pamoja na kujivunia mafanikio yake kitaaluma lakini bado anazo ndoto nyingi katika taaluma yake na hiyo inampelekea kuamini kuwa bado anahitaji kuongeza nguvu katika kuifikia jamii hasa ya watu wa pembezoni ambayo inayokabiliwa na matatizo mbali mbali. 

Tunamtakia kila la kheri katika kusherekea kumbukumbu ya kuzaliwa kwake,Mwenyezi Mungu amjaalie umri mrefu,siha maridhawa,hekima na mafanikio katika maisha yake. 

Happy Birth day Brother!! 

Tumekuletea baadhi ya picha za Kadama Malunde,katika matukio mbalimbali 
Hapa ni katika studio ya Mlimani Radio jijini Dar es salaam Kadama Malunde akifanya kipindi cha radio mwaka 2011.
Mwaka 2012,Kadama Malunde akisoma Habari katika studio ya Radio Faraja FM Stereo ya mkoani Shinyanga.
Mwaka 2015 Kijana Kadama Malunde katika pozi
Kadama Malunde akiwa na mmoja wa wakimbiza mbio za mwenye mkoani Shinyanga mwaka 2014
Kadama Malunde akiwajibika mtaani na mwandishi wa Malunde1 blog,bwana Marco Maduhu
Kadama Malunde akiwa na msanii wa maigizo na vichekesho Senga
Mwaka 2015 Kadama Malunde alipokutana na msanii maarufu wa nyimbo za asili ambaye huimba kwa lugha ya Kisukuma Bhudagala Mwanamalonja ,akiwa katika harakati zake za kutafuta nyimbo za wasanii wa nyimbo za asili aziweke katika mtandao wake wa Malunde1 blog,kupitia kipengele cha NYIMBO ZA ASILI.
Kadama Malunde akiwa na msanii Bhudagala Mwanamaonja

Kadama Malunde akiwa na msanii Bhudagala Mwanamalonja katika show ya msanii huyo katika kijiji cha Usanda kata ya Samuye wilaya ya Shinyanga

Kadama Malunde akisalimiana na katibu mtendaji wa Baraza la Habari Tanzania(MCT) Kajubi Mukajanga.
Akiwa katika pozi.
Akiwa katika mizunguko yake.
Akichat.
Katika pozi.
Akiwa na mwenyekiti mstaafu wa Klabu ya waandishi wa habari mkoa wa Shinyanga ndugu Shija Felician(baada ya Shija,Kadama ndiyo mwenyekiti mwingine wa klabu hiyo).
Akiwa Mikumi mkoani Morogoro wakati wa ziara zake mwaka 2015.
Kadama Malinde akiwa katika pozi na waandishi wa habari Philipo Malaki (RFA)na Veronica Natalis( Radio Faraja/DW) ambao hufanya kazi kwa ukaribu zaidi na Malunde1 blog.
Kadama Malunde akiwajibika katika ofisi ya waandishi wa habari mkoa wa Shinyanga hivi karibuni.
Kadama Malunde akiwa ofisini kwake
Tisheti za Malunde1 blog.
Kadama Malunde akiwa katika ziara yake kutembelea bwawa la Ning'wa ambalo ni moja ya vyanzo vya maji katika manispaa ya Shinyanga.
Kadama Malunde akiendesha mkutano wa wadau wa habari mkoani Shinyanga siku chache kabla ya uchaguzi mkuu 2015 nchini,wakijadili namna ya kuhakikisha amani ya nchi inakuwepo kabla,wakati na baada ya uchaguzi wa madiwani,wabunge na rais wa jamhuri ya muungano wa Tanzania
Kadama Malunde akiwa na rais wa waandishi wa habari Tanzania Deo Nsokolo. 
Kadama Malunde akiwa na baadhi ya Bloggers nchini Tanzania,kulia kwake ni mwenyekiti wa Chama cha wamiliki wa Blogu nchini(TBN) bwana Joachim Mushi walipokutana katika mkutano wa kwanza mwaka 2015.
Kadama Malunde akiwa na Bloggers wenzake nchini Tanzania

No comments: