Wednesday, December 23, 2015

Wanafunzi wa shule msingi International School of Tanganyika (IST) Alyanz Nasser na Shilen Dawda watengeneza mifuko mipya


Mkurugenzi Mazingira Ofisi ya Makamu wa Rais Ofisi ya Mazingira, Bwana Julius Ningu (kulia) akiwapongeza Vijana wa Shule ya International School of Tanganyika (IST) mbele ya Waandishi wa Habari leo 23 Desemba, 2015 katika Ukumbi wa Idara ya Habari (MAELEZO) kwa ubunifu wa kutengeneza mifuko kwa ajili ya utunza mazingira dhidi ya utupaji taka ovyo. Kushoto ni Mkurugenzi wa Masoko Limited, Bwana Constantine Majavika, anaemfuatia ni Alyanz Nasser na mwenzie Shilen Dauda (wa pili kulia). 
Mkurugenzi wa Masoko Limited, Bwana Constantine Majavika (kushoto) akifafanua kuhusu ubunifu uliofanywa na vijana wa Shule ya International School of Tanganyika (IST) mbele ya Waandishi wa
Habari leo 23 Desemba, 2015 katika Ukumbi wa Idara ya Habari (MAELEZO) wa kutengeneza mifuko kwa ajili ya utunza mazingira dhidi ya utupaji taka ovyo. Kushoto ni Shilen Dauda na katikati ni Alyanz Nasser.

Kijana wa Shule ya International School of Tanganyika Alyanz Nasser (katikati) aieleza dumuni lao kubwa la kubuni mifuko ya Envirobags inayowezesha kuepukana na utupaji taka ovyo nchini wakati wa mkutano na  waandishi wa habari leo 23 Desemba, 2015 katika Ukumbi wa Idara ya Habari (MAELEZO). Kulia ni Mkurugenzi Mazingira Ofisi ya Makamu wa Rais Ofisi ya Mazingira, Bwana Julius Ningu, kushoto ni Mkurugenzi wa Masoko Limited, Bwana Constantine Majavika na wa pili kulia ni kijana wa shule hiyo Shilen Dauda.
Mkurugenzi wa Masoko Limited, Bwana Constantine Majavika (kushoto) akionyesha aina za mifuko ijulikanayo kama Envirobags mbele ya waandishi  wa habari (hawapo pichani) itakayoweza kusaidia kuondokana na tatizo la utupaji taka ovyo nchini. Kulia ni Mkurugenzi Mazingira Ofisi ya Makamu wa Rais Ofisi ya Mazingira, Bwana Julius Ningu akiangalia moja ya mifuko ya Envirobags. 


Baadhi ya Waandishi wa Habari wakifuatilia taarifa ya ubunifu uliofanywa na Vijana wa Shule ya International School of Tanganyika (IST) leo 23 Desemba, 2015 katika Ukumbi wa Idara ya Habari (MAELEZO) jijini Dar es Salaam.  (Picha zote na Benedict Liwenga)
………………………………………………………
Na Skolastika Tweneshe.

VIJANA wawili wa Shule ya Msingi International School of Tanganyika (IST) Alyanz Nasser na Shilen Dawda wametangaza mifuko mipya ambayo imetengenezwa kwa malighafi nzuri
isiyoweza kuathiri mazingira.

Wakizungumza na waandishi wa habari leo jijini Dar es salaam kwa nyakati tofauti wabunifu hao wamesema kuwa wameguswa na uharibifu wa mazingira hasa unaotokana na matumizi ya mifuko ya plastiki, hivyo wamebuni mradi wa kutengeneza mifuko ambayo haitaathiri mazingira hasa kwenye fukwe za bahari.

“Watanzania ni watumiaji wa mifuko ya plastiki hasa kwenye
fukwe hivyo maji yanapoelemewa na mifuko maji yanakuwa katika hatari.” alisema Alyanz Nasser.

Mbunifu mwingine Shilen Dawda ameeleza kuwa mifuko hiyo
imetengenezwa kwa ukubwa tofauti na inauzwa kati ya shilingi 400 mpaka 1200 ambapo hadi hivi sasa wameuza jumla ya mifuko 10,000 hivyo vijana hao wanaamini kuwa kwa matumizi ya mifuko hiyo Tanzania itakuwa safi na salama.

“Mpaka sasa tumeuza mifuko 10,000 na tunaamini kwa matumizi
ya mifuko hii Tanzania itakuwa safi na salama na viumbe hai wataendelea kuishi.” Alisema Dawda. 


Kwa upande wake Mkurugenzi wa Mazingira Ofisi ya Makamu wa
Rais Bwana Julius Ningu amesema kuwa Serikali inawapongeza vijana hao kwa kuguswa na uharibifu mazingira na kuwataka watanzania wote waunge  mkono juhudi hizo za utunzaji wa Mazingira na kuacha kutumia bidhaa zinazoharibu Mazingira.

No comments: