Sunday, October 4, 2015

WANANCHI WA KIJIJI CHA KENYAMANYORI WILAYANI TARIME WANASTAHILI PONGEZI.

Kwa mbali kabisa, Kamera ya Binagi Media Group-BMG ikapata fursa ya kunasa picha za Shule ya Sekondari Kenyamanyori ambayo ilijengwa kwa nguvu za Wananchi miaka michache iliyopita na kuanza kupokea wanafunzi mwaka 2013 baada ya kukamilika ambapo wanafunzi waliokuwa kidato cha pili katika shule zilizokuwa mbali walihamia shuleni hapo na kuendelea na kidato cha pili huku wengine walichaguliwa kujiunga na kidato cha kwanza mwaka huo.
Na:George Binagi-GB Pazzo
Ni ukweli usiopingika kuwa uongozi wa kijiji hicho pamoja na wananchi wake ambao asilimia kubwa ni wakulima, wanastahili pongezi kwani wazo lao la kujenga shule ya sekondari ni wazo bora na limewasaidia watoto wa kijiji hicho na wale wanaotoka vijiji jirani kupata elimu karibu zaidi hivyo ni vyema wakaendelea kushirikiana na serikali pamoja na wahisani wengi katika kuhakikisha kwamba wanaiboresha zaidi shule hiyo ili iweze kuwa mkombozi kwa ajili ya watoto wao kielimu.
Kulia ni jengo la Utawala na Majengo mengine matatu kushoto ni majengo ya maabara tatu za Sayansi
Majengo mawili ya Maabara
Jengo moja la Maabara
Jengo la Utawala
Madarasa
Vyoo 
Kuna majengo mawili ya nyumba za waalimu ambayo yamefikia hatua hii na moja limekamilika.
Shamba la Shule

No comments: