Monday, August 31, 2015

Kinondoni, Ilala mabingwa U-17 Airtel Rising Stars Dar es salaam

Michuano ya U-17 ya Airtel Rising Stars mkoa wa Dar es Salaam chini ya Chama cha Soka Mkoa wa Dar es Salaam (DRFA) jana ilimalizika rasmi baada ya kushuhudia Kinondoni wakiibuka mabingwa kwa upande wa wasichana huku kwa upande wa wavulana Ilala wakiibuka mabingwa.
Katika mchezo wa awali ambao ulizikutanisha timu za wasichana wa Temeke na Kinondoni, Kinondoni walifanikiwa kuibuka na ushindi wa mabao 2-1. Bao la kwanza la Temeke lilifungwa katika dakika ya 20 na Maimuna Abasi baada ya kuachia shuti kali na kutinga moja kwa moja wavuni.
Bao la pili lilifungwa na Mwantumu Ramadhani dakika ya 30 kutokana na kuunganisha krosi maridhawa iliyochongwa na Maimuna Abasi na kuzama ndani ya kimia.
Bao la Temeke lilifungwa na Opa Clement mnamo dakika ya 25 kutokana na kuwatoka mabeki wa Kinondoni na kumchambua kwa uzuri kipa wa Kinondoni na kuukwamisha mpira moja kwa moja wavuni.
Mchezo wa pili ulizikutanisha timu za wavulana za Kinondoni na Temeke na matokeo kuwa, Kinondoni kuibuka na ushindi wa mabao  2-1.
Temeke waliandika magoli yao yote mawili kupitia kwa Omari Ali baada ya mara zote mbili kuwalamba vyenga mabeki wa Temeke na kuukwamisha mpira kimiani huku bao la kufutia machozi la Temeke likifungwa na Mkomola Yohana dakika ya 80, baada ya kuunganisha kwa kichwa mpira uliopigwa na nahodha wao Rajabu Jumanne.
Wasichana wa Kinondoni wameibuka mabingwa kutokana kuwa na pointi 6 baada ya kushinda michezo yao yote miwili, ikifuatiwa na Ilala yenye pointi tatu huku Temeke wakiburuza mkia wakiwa hawana pointi.
Kwa upande wa wavulana Ilala wamefanikiwa kutwaa ubingwa mara baada ya kuwa na pointi nne sambamba na Kinondoni lakini wakiwa na wastani mzuri wa mabao ya kufunga na kufungwa, Ilala wakiwa na magoli 3 ya kufungwa na 1 lakufungwa wakati Kinondoni wakiwa na magoli 3 ya kufungwa mawili huku Temeke wakiburuza mkia baada ya kupoteza mechi zote mbili.
Baada ya mchezo kumalizika washindi walipata wasaa wa kuzungumza machache ambapo kwa upande wa wasichana, nahodha wa Kinondoni Sylvia Mwacha alisema kuwa amejisikia furaha sana kuwa mabingwa na kutoa pongezi kwa Airtel kutokana na juhudi zao katika kuinua soka la vijana.
“Shukrani kwa Airtel ambao wametupa nafasi na sisi wasichana kuonyesha vipaji vyetu, ni matumaini yangu kuwa wataendelea kufanya hivi kwa siku zijazo pia”, alisema Mwacha.
Nahodha wa Ilala, Abdul Hassan alisema: “Juhudi zetu na kupambana ndio vimetuwezesha kuchukua ubingwa na tunawashukuru sana Airtel kwa sapoti yao bila kusahau TFF pia, hii ni fursa nzuri kwetu kuweza kujituma ili tufike mbali zaidi”, alisema Abdul.
Kocha wa Ilala, Saidi Ambua alisema. “ Mashindano ni mazuri na nashukuru kwa timu ya yangu kuchukua ubingwa , nawashukuru pia Airtel na TFF kwa kuwezesha michuano hii, ila ombi langu kwa Airtel na TFF ni kuweza kuvikaratbati viwanja vingine view angalau kama Karume ili kutoa ffursa kwa vijana kujiendeleza zaidi”, alisema
Kwa upande wake Meneja wa Airtel Kanda ya Dar es Salaam Fredrick Mwakitwange alisema kuwa amefurahishwa kuona vipaji vikubwa sana kwa vijana walioshiriki licha ya umri wao mdogo.
“Nizipeleke shukrani zangu kwa Shirikisho Soka nchini (TFF) kwa ushirikiano wanatupatia ili kuhakikisha mashindano hayo yanaenda vizuri zaidi, na naahidi kuwa sisi kama Airtel tutaendelea kutoa sapoti kubwa ili kuifanya michuano itoe vipaji vingi zaidi kwa manufaa ya taifa”, alisema Mwakitwange.
Naye Mwenyekiti wa Kamati ya Soka la Vijana TFF Ayubu Nyenzi alisema kuwa, anawashukuru kwa ushirikiano wao katika kukuza vipaji kwa vijana ili kuweza kutimiza ndoto za vijana wengi.
“Kwa niaba ya TFF, ningependa kutoa shukrani zangu za dhati kwa Airtel kwa kuendelea kusapoti vijana kuendesha michuano hii ya Airtel Rising Stars na naamini ushirikiano huu utazidi kudumu zaidi”, alisema Nyenzi.

Mashindano ya Airtel Rising Stars ambayo mwaka huu yanashirikisha mikoa ya Ilala, Kinondoni, Temeke, Morogoro, Mbeya, Mwanza na Arusha inatarajiwa kuingia kwenye hatu nyeti ya fainali za Taifa iliyopangwa kufanyika kwenye Uwanja wa Karume, Dar es Salaam, kuanzia Septamba 11 hadi 21 mwaka huu.
 Fredrick Mwakitwange (Right), the Airtel Manager in Dar es Salaam Region, presents  Airtel Rising Stars Trophy to Kinondoni girls skipper Sylvia Mwacha, after winning the the U-17 soccer for girls category in Dar es Salaam region at Karume Memorial Stadium in Dar es Salaam, yesterday

Fredrick Mwakitwange (Right), the Airtel Manager in Dar es Salaam Region, presents  Airtel Rising Stars Trophy to Ilala boys skipper Abdul Hassan, after winning the the U-17 soccer for the boys category in Dar es Salaam region at Karume Memorial Stadium in Dar es Salaam, yesterday.

No comments: