Wednesday, May 27, 2015

NHIF WAZINDUA MPANGO WA HUDUMA ZA MADAKTARI BINGWA MANYARA.

 Meneja wa NHIF Mkoa wa Manyara, Innocent Mauki akiwakaribisha viongozi wa NHIF makao makuu na uongozi wa Mkoa wa Manyara, kwenye uzinduzi wa mpango wa huduma za madaktari bingwa Mkoani Manyara. 
Baadhi ya wakazi wa Wilaya ya Babati Mkoani Manyara, wakishuhudia Mkuu wa Mkoa wa Manyara, Dk Joel Nkaya akizindua mpango wa huduma za madaktari bingwa mkoani humo, zilizowezeshwa na NHIF
 Mkuu wa Mkoa wa Manyara, Dk Joel Nkaya Bendera akizungumza asubhi ya leo kwa kuwa mkoa huo kujiunga na mfuko wa afya ya jamii (CHF) kwenye uzinduzi wa mpango wa huduma za madaktari bingwa mkoani Manyara uliowezeshwa na NHIF.
 Mkuu wa Mkoa wa Mkoa wa Manyara, Dk Joel Nkaya Bendera (kushoto) akimkabidhi Mganga Mkuu wa Mkoa wa Manyara, Dk Ally Uredi vifaa tiba na dawa zilizotolewa na Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya, (NHIF) ambazo gharama zake ni shilingi milioni 5.5.
 Ofisa mawasiliano wa Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya nchini (NHIF) Luhende Singu akizungumza wakati wa zoezi la kuzindua mpango wa huduma za madaktari bingwa Mkoani Manyara, asubuhi ya leo.
 Baadhi ya wananchi wa Wilaya ya Babati Mkoani Manyara wakiwa kwenye hospitali ya rufaa ya Mkoa huo ambapo leo asubuhi Mkuu wa Mkoa huo Dk Joel Nkaya Bendera alizindua mpango wa huduma za madaktari bingwa uliondaliwa na NHIF.
Bibi Cecilia Tluway wa Wilaya ya Babati akikabidhiwa msaada wa shilingi 10,000 na Ofisa mawasiliano wa Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya nchini (NHIF) Luhende Singu, za kujiunga na mfuko wa Afya ya Jamii nchini CHF wakati wa zoezi la kuzindua mpango wa huduma za madaktari bingwa Mkoani Manyara, asubuhi ya leo.

No comments: