Tuesday, May 26, 2015

MAONYESHO YA PICHA ZA ALBERT MANIFESTER YAFANA JIJINI DAR

Mpiga Picha maarufu nchini, Albert Manifester, Mei 24 mwaka huu alifanya maonyesho ya baadhi ya picha alizopiga ikiwa ni sehemu ya kazi zake na baadhi ya picha zilizouzwa siku hiyo zilifanikisha kupatikana kwa kiasi cha shilingi milioni kumi na laki Tatu ambapo asilimia 50 ya mauzo hayo yalitolewa ili kusaidia huduma ya afya ya uzazi katika kijiji cha Kipamba kinachoishi watu wa jamii ya Wahadzabe.

Akizungumza katika hafla hiyo, Manifester alisema kuwa "picha inaongea haraka zaidi kuliko maneno, hivyo na amini kupitia jicho langu nitabadilisha maisha ya watanzania wengi, naanza na watanzania wenzetu Wahadzabe kuboresha huduma ya afya ya uzazi kwa wakina mama".
Mgeni rasmi katika hafla ya maonyesho ya picha zilizopigwa na Albert Manifester (kushoto), Mama Mwantum Malale (kulia) akipokea moja ya picha kama zawadi kutoka kwa mpiga picha huyo.
Mpiga Picha maarufu, Albert Manifester (kushoto) akionyesha sehemu ya kazi zake kwa Mgeni rasmi katika hafla hiyo ya maonyesho ya picha, Mama Mwantum Malale wakati alipokuwa akitembelea shemu mbali mbali kuona picha hizo. Hafla hii ilifanyika kwenye hoteli ya Hyatt Regency, Jijini Dar es salaam.
Mpiga Picha maarufu, Albert Manifester (kushoto) akiwaeleza jambo, Mgeni rasmi katika hafla hiyo ya maonyesho ya picha, Mama Mwantum Malale pamoja na Mkuu wa Wilaya ya Mkalama, Mh. Edward Ole Lenga wakati wa hafla hiyo.
Mpiga Picha, Albert Manifester akizungumza na vyombo vya habari vilivyofika kwenye uzinduzi huo.


















No comments: