Sunday, April 19, 2015

KINANA ASHIRIKI KATIKA BONANZA LA VILABU VYA JOGGING MKOA WA DAR ES SALAAM, VIJANA WATAKIWA KUJIANDIKISHA DAFTARI LA WAPIGA KURA

k01
Katibu Mkuu wa Chama cha Mapinduzi Ndugu Abdulrahman Kinana akianza mazoezi wakati akishiriki  katika bonanza la Jogging lililoandaliwa na Kundi la Kaza Moyo Jogging Club la Ukonga Sitakishari ili kuhamasisha vijana kujitokeza kwa wingi kujiandikisha katika daftari la kudumu la wapiga kura 
. Mazoezi hayo yameanzia katika viwanja vya Gongo Gongo la Mboto kupitia Kipawa  na kuishia kwenye uwanja wa Social Sitaki Shari Ukonga ujumbe mkuu wa Bonanza hilo ulikuwa ni kuwataka vijana kujitokeza kwa wingi kujiandikisha ili kupata haki ya kupiga kura kuliko kuwa mashabiki tu.
 Bonanza hilo la mazoezi limeshirikisha vilabu mbalimbali vya Jogging kutoka mkoa wa Dar es salaam, Kutoka kushoto ni Mwenyekiti wa serikali ya Mtaa wa Mogo George Shinga Mtambalike, Mwenyekiti wa CCM mkoa wa Dar es salaam Ramadhan Madabida na kulia ni Bona Kaluwa Diwani wa Kata ya Kipawa.k1
Katibu Mkuu wa Chama cha Mapinduzi Ndugu Abdulrahman Kinana wa tatu akiendelea na  mazoezi wakati akishiriki Mazoezi katika bonanza la Joging lililoandaliwa na Kundi la Kaza Moyo Joging Club la Ukonga Sitakishari ili kuhamasisha vijana kujitokeza kwa wingi kujiandikisha katika daftari la kudumu la wapiga kura . Mazoezi hayo yameanzia katika viwanja vya Gonga Gongo la Mboto kupitia Kipawa  na kuishia kwenye uwanja wa Social Sitaki Shari Ukonga, Kutoka kushoto ni Nape Nnauye Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi, Mwenyekiti wa serikali ya Mtaa wa Mogo George Shinga Mtambalike, Mwenyekiti wa CCM mkoa wa Dar es salaam Ramadhan Madabida
k2
Wakiendelea na mazoezi hayo.
k3
Makundi mbalimbali ya Jogging kutoka mkoa wa Dar es salaam yakishiriki katika mazoezi hayo.
k4
k6
Ndugu Abdulrahman Kinana akiendelea na mazoezi hayo katika maeneo ya Kipawa pamoja navijana na watoto wadogo kulia ni Mwenyekiti wa CCM mkoa wa Dar es salaam Ramadhan Madabida na kushoto ni Mwenyekiti wa serikali ya Mtaa wa Mogo George Shinga Mtambalike,
k7k9
Mazoezi yakiwa yapepamba moto eneo la uwanja wa Ndege
k10k11
Kinana akifurahia jambo na watoto katika mazoezi hayo huku Mwenyekiti wa CCM mkoa wa Dar es salaam Ndugu Ramadhan Madabida kulia akimuangalia.
k12
Makundi mbalimbali ya vilabu vya Jogging mkoa wa Dar es salaam yakiwasili katika viwanja vya Social Sitaki Shari Ukonga.
k13k14k15k16k17k18
Umati wa vijana kutoka Vilabu mbalimbali vya Jogging mkoa wa Dar es salaam wakiendelea na mazoezi mara baada ya kuwasili kwenye uwanja wa Social Ukonga Sitaki Shari.k19
Nape Nnauye Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi akiongoza Mazoezi hayo kwenye uwanja wa Social Sitaki Shari Ukonga.
k20k21
Msanii wa musiki wa Mchiriku Maarufu kama  Mkaanga Sumu akitumbuiza katika bonanza hilo.
k22
Mratibu wa bonanza hilo Bw.Msafiri akizungumza na vijana waliojitokeza kwa wingi.
Mk23k24
Katibu Mkuu wa Chama cha Mapinduzi Ndugu Abdulrahman Kinanakulia akifurahia jambo  na Nape Nnauye Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi
k25
Katibu Mkuu wa Chama cha Mapinduzi Ndugu Abdulrahman Kinanaakizungumza na Nape Nnauye Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi, kulia ni Mwenyekiti wa CCM mkoa wa Dar es salaam Ndugu Ramadhan Madabida.
k26
Dogo Asley wa Yamoto Band ya Mkubwa na Wanawe akifanya vitu vyake jukwaani katika bonanza hilo.
k27
Kundi zima la Yamoto Bandi likifunika kwa shoo kali katika bonanza hilo.
k28k29
Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akipiga picha na pamoja na vijana wa klabu ya Kaza Moyo Jogging Club mara baada ya kushiriki katika bonanza lao, Kulia ni Bona Kaluwa Diwani wa Kata ya Kipawa na kushoto ni Mwenyekiti wa Serikali ya Mtaa wa Mogo Ndugu George Mtambalike.
k30
Nape Nnauye akizungumza na waandishi wa habari wakati alipotoa wito kwa tume ya uchaguzi kuhakikisha wanawahamasisha vijana ili kuiandikisha kwenye daftari la kudumu la mpiga kura

No comments: