Thursday, March 5, 2015

KATIBU MKUU WA CCM,NDUGU KINANA AENDELEA NA ZIARA YAKE JIMBO LA KIBAKWE WILAYANI MPWAPWA.

Pichani Msafara wa Katibu Mkuu,Ndugu Abdulrahman Kinana ukielekea jimbo la Kimbakwe  Wilayani Mpwapwa mapema leo asubuhi kuendelea na ziara yake ya siku 9 mkoani Dodoma ya Kuimarisha uhai wa chama,kukagua nakuhimiza utekelezaji wa Ilani ya uchaguzi 2010 pamoja na kusikiliza kero za Wananchi ikiwemo na kuzitafutia ufumbuzi.
Katibu Mkuu wa CCM,Ndugu Kinana akisalimiana na baadhi ya vijana waliopo katika kituo cha mradi wa Wanyama kazi ndani ya kijiji cha Kibakwe,wilayani Mpwapwa.
Mmoja wa Vijana waliopo katika kituo cha mradi wa Wanyama kazi ndani ya kijiji cha Kibakwe,wilayani Mpwapwa wakitoa maelezo mafupi mbele ya Katibu Mkuu wa CCM,Ndugu Kinana namna zana hizo za kilimo zinavyotumiwa na wanyaka katika suala zima la kilimo.
Katibu Mkuu wa CCM,Ndugu Kinana akipata maelezo mafupi kuhusiana na uoteshaji wa mbegu za miti ya mikorosho  katika kituo cha mradi wa Wanyama kazi ndani ya kijiji cha Kibakwe,wilayani Mpwapwa.
Katibu Mkuu wa CCM,Ndugu Kinana akikagua shamba la mfano la Wanaushirika waitwao Mkombozi,lililopo karibu na kituo cha mradi wa Wanyama kazi ndani ya kijiji cha Kibakwe,wilayani Mpwapwa.
Mwenyekiti wa kikundi cha Mkombozi,Bwa.Athanas Kigosi akitoa maelezo mafupi mbele ya Katibu Mkuu wa CCM,Ndugu Kinana,kuhusiana na shamba la mfano ambalo limepandwa mahindi,lililopo katika kijiji cha Kibakwe,Wilayani Mpwapwa.Bwa.Athanas alieleza changamoto wazipatazo katika maandalizi yao ya kilimo kuwa suala la pembejeo limekuwa tatizo kubwa kwao,kwani zimekuwa zikiletwa kinyume na wakati,hali inayowapelekea ugumu wa kuendelea na kilimo kwa wakati,mabadiliko ya hali ya hewa ikiwemo sambamba na mazao yao kutopandishwa bei,Hivyo Bwana Athanas ameiomba serikali kuwasaidia wakulima kupelekewa pembejeo kwa wakati ili kuhakikisha maandalizi ya kilimo yanakwenda kwa wakati.
Katibu Mkuu wa  CCM,Ndugu Kinana akifafanua jambo kwa Wanahabari katika shamba la mfano ambalo limepandwa mahindi,lililopo katika kijiji cha Kibakwe,Wilayani Mpwapwa.Pichani kulia ni Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi Taifa,Nape Nnauye.
Katibu Mkuu wa CCM,Ndugu Kinana akishiriki ujenzi wa darasa la shule ya sekondari Ikuyu katika kijiji cha Luhundwa,wilaya ya Mpwapwa.Ndugu Kinana alikagua na kushiriki  mradi wa ujenzi wa darasa la shule hiyo na kuwasalimia wananchi.
Katibu Mkuu wa CCM,Ndugu Kinana akisalimiana na Wananchi wa kijiji cha Luhundwa mapema leo,alipokwenda kushiriki ujenzi wa darasa la shule ya sekondari Ikuyu katika kijiji cha Luhundwa,wilaya ya Mpwapwa.
Wananchi wa kata ya Rudi wakimsikiliza Katibu Mkuu wa CCM,Ndugu Kinana mara baada ya kukagua na kushiriki ujenzi wa ofisi ya Mtendaji Kata.
Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Kinana akishiriki mradi wa ujenzi wa ofisi ya Mtendaji Kata ya Rudi,Wilaya ya Mpwapwa mkoani Dodoma.Mwisho kulia ni Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Dodoma,Mh.Addam Kimbisha pamoja na Diwani wa kata hiyo,Mh.Nyaulingo Bulamlete.
Katibu Mkuu wa CCM,Ndugu Kinana akiweka jiwe la msingi katika ofisi ya CCM tawi la Mtamba,wilaya ya Mpwapwa.
Katibu Mkuu wa CCM,Ndugu Kinana pamoja na Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi Nape Nnauye wakifurahia jambo mara baada ya kuweka jiwe la msingi katika ofisi ya CCM tawi la Mtamba,wilaya ya Mpwapwa.
 Wakazi wa jimbo la Kibakwe wakimsikiliza Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana wakati akihutubia kwenye mkutano wa hadhara uliofanyika kwenye uwanja wa Kibakwe stendi,Katibu Mkuu aliwataka viongozi wanaosimamia sheria kuzingatia wananchi wa kawaida na kuwashirikisha kwenye jambo linalowagusa kwenye shughuli zao za kila siku kwani kufanya hivyo kutawasaidia wananchi hao kuishi maisha yao na pia kuinua uchumi wa eneo husika.
 Wakazi wa jimbo la Kibakwe wakimshangilia jambo wakati Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana wakati akihutubia kwenye mkutano wa hadhara uliofanyika kwenye uwanja wa Kibakwe stendi.
 Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi Nape Nnauye akihutubia wakazi wa Kibakwe kwenye mkutano wa hadhara uliofanyika Stendi ya Kibakwe wilayani Mpwapwa.
Mwenyekiti wa CCM mkoa wa Dodoma Mheshimiwa Adam Kimbisa akihutubia wakazi wa Kibakwe kwenye mkutano wa hadhara uliofanyika Stendi ya Kibakwe na kuwataka wana CCM kuchagua viongozi wanaowataka na kusema wilaya au mkoa hawataka jina la mtu yeyote aliyechaguliwa na wananchi.
 Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akisisitiza jambo wakati wa mkutano wa hadhara uliofanyika kwenye viwanja vya Stendi ya Kibakwe,jimbo la Kibakwe wilaya ya Mpwapwa,Katibu Mkuu yupo kwenye ziara ya kujenga na kuimarisha chama mkoa wa Dodoma akiwa ameongozana na Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi Nape Nnauye.
 Wakazi wa jimbo la Kibakwe wakimsikiliza Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana wakati akihutubia kwenye mkutano wa hadhara uliofanyika kwenye uwanja wa Kibakwe stendi,Katibu Mkuu aliwataka viongozi wanaosimamia sheria kuzingatia wananchi wa kawaida na kuwashirikisha kwenye jambo linalowagusa kwenye shughuli zao za kila siku kwani kufanya hivyo kutawasaidia wananchi hao kuishi maisha yao na pia kuinua uchumi wa eneo husika.

No comments: