Sunday, February 1, 2015

Yanga yashindwa kufutukuta mbele ya Ndanda,zatoka suluhu kwenye uwanja wa Taifa jijini Dar leo

 Mshambuliaji Machachari wa timu ya Ndanda,Masoud Ally akitoa pasi maridadi kabisa mbele ya beki wa timu ya Yanga,Juma Abdul wakati wa mtanange wa ligi kuu Tanzania Bara,uliomalizika hivi punde kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam.Mechi hiyo imemalizika kwa suluhu ya 0-0.PICHA ZOTE NA OTHMAN MICHUZI.
 Mrisho Ngassa wa Yanga akiondoka na mpira huku akifuatwa na Beki wa Ndanda,Paul Ngalema wakati wakati wa mtanange wa ligi kuu Tanzania Bara,uliomalizika hivi punde kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam.Mechi hiyo imemalizika kwa suluhu ya 0-0.
 Nyanda wa timu ya Yanga,Ally Mustafa akiwa makini kulilinda lango lake.
 Mshambuliaji wa timu ya Ndanda,Omega Seme akiangalia namna ya kumtoka Beki wa Yanga,Oscar Joshua mtanange wa ligi kuu Tanzania Bara,uliomalizika hivi punde kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam.Mechi hiyo imemalizika kwa suluhu ya 0-0.
 Beki Hasifiwi: Beki wa timu ya Yanga,Rajab Zahir akiruka juu kuondoa hatari iliyokuwa ikielekea langoni kwao katika mtanange wa ligi kuu Tanzania Bara,uliomalizika hivi punde kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam.Mechi hiyo imemalizika kwa suluhu ya 0-0.
 Beki wa timu ya Yanga,Rajab Zahir akiwania mpira na Jacob Massawe wa Ndanda.
 Nadir Haroub wa Yanga akijaribu kuondosha hatari ilikuwa langoni kwake.
 Dan Mrwanda wa Yanga akitafuta namna ya kumtoka beki wa Ndanda,Paul Ngalema.
 Hapiti mtu hapa: ni kama anaonekana kusema  beki wa timu ya Ndanda,Paul Ngalema wakati akimdhibiti Mshambuliaji wa Yanga,Simon Msuva.
 ajali kazini.
 Hatariiiii paleee....... daaahh.... wanakosa goli Yanga hapaaa....
 Kocha wa Timu ya Yanga,Hans Van Der Pluijm akifanyiwa mahojiano na Mtangazaji wa Michezo wa Radio Clouds,Issa Maeda.
 Chombo kiko tayari kwa kazi.
 Wadau uwanjani.
 Washabiki wa timu ya Ndanda wakiishangilia timu yao.

No comments: