Friday, February 27, 2015

JK aandaliwa dhifa na Rais Lungu wa Zambia, amtembelea KK

Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete na mwenyeji wake Rais Edgar Lungu wa Zambia wakigonga glasi wakati wa dhifa ya kitaifa aliyoiandaa kwa heshima ya Rais Kikwete jijini Lusaka Zambia jana jioni.


Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akigonga glasi na Rais wa Kwanza wa taifa la Zambia Dkt.Kenneth Kaunda wakati wa dhifa ya kitaifa iliyoandaliwa kwa heshima ya Rais Kikwete jijini Lusaka Zambia jana jioni.Rais Kikwete ambaye alikuwa katika ziara ya siku mbili nchini Zambia tayari amerejea jijini Dar es Salaam.

Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete na mwenyeji wake Rais wa Zambia Edgar Lungu pamoja na wake zao Mama Salma Kikwete na Mama Esther Lungu wakinyanyua glasi juu wakati wa dhifa ya kitaifa iliyoandaliwa kwa heshima ya Rais Kikwete na ujumbe wake ambao walifanya ziara ya kikazi ya siku mbili nchini Zambia.

.
 Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akiwa katika mazungumzo na Rais wa kwanza wa Zambia Dkt.Kenneth David Kaunda nyumbani kwake  Mkango Barracks,State lodge, nje ya jiji la Lusaka leo.
 Rais wa Kwanza wa Zambia Dkt.Kenneth Kaunda akimpa zawadi Rais Dkt.Jakaya Kikwete
 Rais Dkt.Jakaya Kikwete akisindikizwa  na Rais wa Kwanza wa Zambia Mzee Kenneth Kaunda mara baada ya kumtembelea na kufanya naye mazungumzo leo
Rais Dkt.Jakaya Kikwete akiagana na Rais wa Kwanza wa Zambia Mzee Kenneth Kaunda mara baada ya kumtembelea na kufanya naye mazungumzo leo Picha na Freddy Maro

No comments: