Tuesday, January 27, 2015

KATIBU MKUU WA CCM NDUGU KINANA AENDELEA NA ZIARA YAKE WETE-KASKAZINI PEMBA,AWATAKA VIONGOZI WA CUF KUTENDA HAKI KWA WANANCHI.

Msafara wa Katibu Mkuu wa CCM,Ndugu Kinana ukikatiza mapema jioni ya leo katikati ya msitu akielekea katika kijiji cha Mnarani -Makangale kuzungumza na wanachama wa chama hicho,micheweni mkoa wa Kaskazini Pemba
 Katibu Mkuu wa CCM,Ndugu Kinana akisalimiana na baadhi ya Vijana wapatao 105 waliokuwa chama cha CUF na kuhamia CCM,katika kijiji cha Mnarani Makangale,ambapo alikwenda kushiriki ujenzi wa tawi lao liitwalo Maskani tuheshimiane.
 Katibu Mkuu wa CCM,Ndugu Kinana akizungumza na Vijana wapatao 105 waliokuwa chama cha CUF na kuhamia CCM.Wakisoma taarifa yao kwa Ndugu Kinana walieleza manyanyaso wanayoyapata kutoka kwa baadhi ya viongozi wa CUF,walieleza kuwa tangu wamehama chama hicho wamekuwa wakibugudhiwa na kufanyiwa fujo kiasi ambacho wamekuwa wakishindwa kufanya kazi zao za kimaendeleo ikiwemo na shughuli zao za uvuvi kusimama,hivyo wamemuomba Katibu Mkuu wa CCM,Ndugu Kinana kulishughulikia jambo hilo ili waweze kuendelea na shughuli zao bila kubugudhiwa kwani wanataka kuishi kwa amani na utulivu.

Akizungumza Ndugu Kinana alisema kuwa chama cha CUF hakitendi haki katika suala zima la demokrasia, ''kwani kila mtu ana uhuru wa kuhamia chama anachotaka na haitaji kubugudhiwa,hivyo Viongozi wa CUF,wanapaswa kulitambua hilo na kuwaacha wananchi waamue watakavyo ili mradi hawavunji sheria za nchi wala kumbugudhi mtu'' alisema Kinana.

Kinana yupo katika ziara ya siku tano ya Kikazi kisiwani Pemba,akihimiza na kukagua utekelezaji wa Ilani ya Uchaguzi ya CCM ya mwaka 2010 ikiwa ni pamoja na kukagua uhai wa chama kisiwani humo.
 Katibu Mkuu wa CCM,Ndugu Kinana akishiri ujenzi wa  Maskani ya tawi la CCM-Tuheshimiane katika kijiji cha Mnarani Makangale,Micheweni mkoa wa Kaskazini Pemba.
 Baadhi akina mama Wakulima wa Mpunga wakisubiri kumpokea katibu Mkuu wa CCM,Ndugu Kinana aliyekwenda Bonde la Mpunga Koowe kuangalia na kushiriki ujenzi wa tuta la Kuzuia maji chumvi katika bonde hilo.
 Pichani kati ni Afisa Mkuu wa Idara ya Umwagiliaji maji-Pemba Mbarouk Ali Mgau akieleza jambo kwa Katibu Mkuu wa CCM,Ndugu Kinana alipokwenda bonde la Mpunga Koowe-wingwi, kuangalia na kushiriki ujenzi wa tuta la Kuzuia maji chumvi katika bonde hilo.Afisa Mbarouk alieleza kuwa mradi huo umegharibu kiasi cha shilingi Milioni 170 zilizotolewa na TASAF.
 Ndugu Kinana akiwa na baadhi akina Mama ambao ni wakulima wa zao la Mpunga katika Bonde la Koowe,wakishiriki ujenzi wa tuta la kuzuia maji chumvi katika bonde hilo
 Katibu Mkuu wa CCM,Ndugu Kinana akisalimia na Mganga Mkuu wa Wilaya ya  Micheweni,Dkt.Rashid Daud mara baada ya kuwasili katika hospitali ya Wilaya ya  Micheweni,Kaskaini pemba mapema leo.
  Katibu Mkuu wa CCM,Ndugu Kinana akizingumza na baadhi ya Madaktari wa hospitali ya Wilaya ya Micheweni,mara baada ya kuwasili katika hospitali hiyo,Kaskazini Pemba mapema leo.
 Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akishiriki ujenzi wa jengo la upasuaji katika hospitali ya wilaya ya Micheweni mkoa wa Kaskazini Pemba, wanaoshuhudia ni madaktari viongozi mbalimbali wa wilaya ya Micheweni na hospitali hiyo.
 Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akipata maelezo kutoka kwa  Dkt.Rashid Daud Mkasha Mganga Mkuu wa Wilaya ya Micheweni wakati alipokuwa akikagua ukarabati wa wodi katika hospitali hiyo.
 Baadhi ya Wananchi wakimsikiliza Katibu Mkuu wa CCM,Ndugu Kinana alipowahutubia jioni ya leo katika mkutano wa hadhara uliofanyika kwenye uwanja wa Majenzi mjini Micheweni.
Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akiwahutubia wananchi katika mkutano wa hadhara uliofanyika kweny uwanja wa Majenzi mjini Micheweni. 
 Katibu Mkuu wa CCM,Ndugu Abdulrahman Kinana akipokelewa na baadhi ya viongozi wa chama cha CCM,alipokuwa akiwasili katika kijiji cha Shaame Mata,Wilaya ya Micheweni mkoa wa Kaskazini Pemba mapema  leo.Pichani kulia ni Mbunge wa Viti maalum Pemba,Mh Maida Hamad Abdalllah na kushoto ni Naibu Katibu Mkuu wa CCM-Zanzibar,Ndugu Vuai Ali Vuai.
 Katibu Mkuu wa CCM,Ndugu Kinana akizungumza Wajumbe wa Halmashauri Kuu ya CCM,wilaya ya Micheweni Kaskazini Pemba

No comments: