Sunday, January 25, 2015

Airtel yazindua huduma ya kufanya malipo kwa kutumia kadi



11

Mfanyabiashara na mmiliki wa duka la dawa katika eneo la Mrombo Arusha Bi elizabeth mshana akiongea na Afisa Uhusiano wa Airtel Jane Matinde juu ya huduma ya kufanya malipo kwa kutumia kadi ya Airtel Money Near Field Communication (NFC) based solution ya  Airtel Money. kadi hii maalum inamuwezesha mteja kufanya malipo kwa haraka kwa kugusisha kwenye kifaa maalum tu mara moja, kisha kuweka nambari ya siri na kufanya malipo mahali popote. kwa sasa huduma hii imeanza kufanya kazi mkoani Arusha. Huduma hii ya Near Field Communication (NFC) yaani kulipa kwa kugusisha kadi na kifaa tu kupitia huduma za kifedha kwa njia ya mtandao ni yakwanza kuzindulia nchini na kampuni ya simu za mkoni ya airtel

1111

Mama elizabeth mshana mmiliki wa duka la dawa akimuuzia mteja dawa kwa kupitia kadi huduma iliyozinduliwa na Airtel mkoani Arusha inayowawezesha wateja wake kufanya malipo kwa haraka zaidi kwa kutumia kadi hiyo maalumu ya airtel Money yenye teknolojia ya Near Field Communication (NFC) based ikiwa imeunganishwa na  Airtel Money.akishuhudia ni Afisa Uhusiano wa Airtel Jane Matinde. Huduma hii ya Near Field Communication (NFC) kupitia huduma za kifedha kwa njia ya mtandao ni yakwanza kuzindulia nchini na kampuni yasimu za mkoni ya airtel.

11111

Afisa uhusiano wa kampuni ya simu za mkononi ya AIRTEL Jane Matinde akimuelekeza Moja ya wateja bi Merry Ngowi jinsi ya kutumia kifaa na kadi maalumu ambacho hutumika kukamilisha miamala ya malipo katika maduka mbalimbali. Huduma hii ya Near Field Communication (NFC) kupitia huduma za kifedha kwa njia ya mitandao ni yakwanza kuzindulia nchini na kampuni ya simu za mkoni ya airtel, tukio lifanyika mwishoni mwa wiki mkoani arusha eneo la muromboo wakati wa uzinduzi huduma hiyo ambayo inaleta njia salama, ya haraka na rahisi kwa wateja kufanya malipo. 

111

Mfanyabiashara wa duka la chakula katika eneo la Mrombo Arusha Bwana Elibariki Ngowi akipokea malipo kutoka kwa mteja kwa kupitia kadi maalum ya Near Field Communication (NFC) ya Airtel Money.  , huduma imezinduliwa na Airtel mkoani Arusha inawawezesha wateja wake kufanya malipo kwa kutumia kadi hiyo maalumu kwa haraka bila huanza kupiga *150*60# hii unagusisha tu na kulipa haraka kati kanti ni Afisa Uhusiano wa Airtel Jane Matinde akishudia huduma hiyo inavyofanya kazi.  Huduma hii ya Near Field Communication (NFC) kupitia huduma za kifedha kwa njia ya mtandao ni yakwanza kuzindulia nchini na kampuni ya simu za mkoni ya airtel.


……………………………………………

Na Mwandishi Wetu

Kampuni ya simu za mkononi ya Airtel leo (mwishoni mwa wiki) imetangaza huduma ya kwanza sokoni inayotumia kadi maalumu kwa kupitia huduma ya Airtel Money. Huduma hiyo mpya inayowawezesha wateja wa Airtel Money kufanya malipo kwa kutumia kadi  imeanza katika mkoa wa Arusha na itaendelea kufikishwa katika mikoa mbalimbali nchini.

Akiongea kuhusu huduma hiyo, Mkurugenzi wa Airtel Money Aijaza Khan alisema” technologia inakuwa kwa kasi na tumeonelea ni muhimu kwenda sambamba na mabadiliko hayo kwa kuleta huduma za kibunifu zitakazokithi mahitaji ya wateja wetu yanayokuwa kwa kasi kila siku.  Nia yetu ni kuona wateja wetu wanapata huduma za kisasa kwa wakati wote. 

Huduma hii mpya tunayoitambulisha leo itawawezesha wauzaji na wanunuzi kupata njia rahisi, ya uhakika na salama ya kufanya miamala na malipo yao ya kila siku.  ili kutumia huduma hii kila mteja atatakiwa kupata kadi maalum inayomuwezesha kufanya malipo kirahisi , kwa haraka na kwa usalama katika maduka mbalimbali yaliyopatiwa  vifaa maalumu kwaajili ya kupokea malipo toka kwa wateja. Huduma hii imeshaanza kufanya kazi kwa wafanyabiashara na wateja wetu Arusha. 


“Kadi hii maalumu imeunganishwa na akaunti ya Airtel Money ya mteja, mteja anachotakiwa ni kugusisha  kadi  yake na kifaa cha kupokea malipo (POS) ili kuweza  kufanya malipo.  Malipo yatakamilika pale mteja atakapothibitisha muamala  kwa kuweka namba yake ya siri  kwenye kifaa  cha malipo.


Tunajivunia kuwa mtandao wa kwanza Tanzania kuanzisha huduma hii ya kibunifu itakayowawezesha wateja wetu kufanya malipo ya kwa urahisi, haraka , kiusalama bila kuwa na haja ya kupiga namba ya Airtel money na kuingia kwenye orodha, Kwa kutumia kadi maalumu mteja anaweza sasa kufanya malipo. ”. aliongeza Khan.


Akiongea kuhusu faida za huduma hiyo , Afisa Uhusiano wa Airtel Bi Jane Matinde alisema” huduma hii inafaida nyingi kwa wafanyabishara na wateja ikiwa ni pamoja na njia salama ya kuifadhi pesa, ya kuhakiki na kukusanya pesa,mfanyabiashara anaweza kuzipeleka moja kwa moja benki kutoka kwenye kifaa hicho au kutoa pesa kwa wakala aliye karibu. Kwa upande wa wateja  faida hizo ni pamoja na kufurahia urahisi, usalama, uharaka wa kufanya malipo na pia  kuepusha wateja kutembea na pesa  nyingi mfukoni ili kufanya malipo. Mteja atakapopoteza au kuibiwa kadi yake pesa zake kwenye kadi yake zinabaki salama aliongeza” Matinde.


Akiongelea kuhusu uzoefu alioupata a kutumia huduma hii ya kadi kupitia Airtel Money, Mfanyabiashara na milliki wa Phamarcy Bi Elizabeth Mshana alisema” Huduma hii ni ya kipekee  na imerahisisha sana namna ya kufanya biashara maana ni rahisi kutumia na ni salama. Wateja wanapokuja dukani kununua dawa na hawana pesa taslimu mfukoni wanatumia huduma hii na mimi kama muuzaji nafurahi kwakuwa pesa zangu ziko salama na sina haja ya kufikiri kuhusu kutafuta chenji. 

Kwa kweli ni huduma nzuri na tunaifurahia na nawashauri wafanyabiashara  wenzangu na wateja kutumia huduma hii kwani inaleta ufanisi” Huduma hii inapatikana sehemu mbalimbali ikiwemo maduka ya biadhaa , maduka ya chakula, maduka ya dawa, mawakala wa Airtel Money na Baa, Mpango mkakati ni kufikisha huduma hii katika maeneo mbalimbali nchini kwa mwaka huu.


Airtel kupitia huduma yake ya Airtel Money hivi karibuni imezindua huduma nyingine ya kibunifu ijulikanayo kama Timiza inayowawezesha wateja wake kupata mikopo rahisi  papokwa papo na kurejesha baada ya wiki moja au mwenzi huduma ambayo imewawezesha watanzania wengi kuboresha mitaji ya biashara zao na kutatua changamoto ndogondogo za kila siku

No comments: