Sunday, December 21, 2014

Washindi wa shindano la AppStar wakabidhiwa zawadi zao


Mshindi wa kwanza wa shindano la AppStar tabaka la wabunifu waliobobea Roman Mbwasi akielezea jambo wakati wa shughuli ya kukabidhi zawadi kwa washindi hao iliyofanyika makao makuu ya Vodacom Tanzania mwishoni mwa wiki hii. Katikati ni Meneja Uhusiano wa Nje wa Vodacom Abigail Ambweni, akimsikiliza kwa makini pamoja na mshindi wa kwanza katika tabaka la wabunifu chipukizi, George Machibya (kulia) Shindano hilo linaendeshwa na kampuni hiyo.

Meneja Uhusiano wa Nje wa Vodacom Tanzania Abigail Ambweni (kushoto) akishuhudia wakati mshindi wa kwanza wa shindano la AppStar tabaka la wabunifu waliobobea Roman Mbwasi (wa pili kutoka kushoto) akionyesha zawadi ya pesa taslimu Tsh. milioni 2/- aliyojishindia kupitia shindano la AppStar. Wakishuhudia tukio hilo pia ni mshindi wa kwanza katika tabaka la wabunifu chipukizi, George Machibya (wa tatu toka kushoto) na Athumani Mahiza, mshindi wa pili katika tabaka la wabunifu waliobobea (wa mwisho toka kushoto). Shindano hilo linaendeshwa na kampuni hiyo.

Meneja Uhusiano wa Nje wa Vodacom Tanzania Abigail Ambweni (kushoto) akimkabidhi zawadi ya pesa taslimu Tsh. milioni 2/- mshindi wa kwanza wa shindano la AppStar tabaka la wabunifu waliobobea ambao programu zao tayari zinatumiwa na watu zaidi ya 50,000 Roman Mbwasi (wa pili toka kushoto). Shindano hilo linaendeshwa na kampuni hiyo.

Washindi wa shindano la AppStar wakionyesha zawadi zao za pesa taslimu walizokabidhiwa na Meneja Uhusiano wa Nje wa Vodacom Tanzania Abigail Ambweni (wa tatu toka kushoto) Hafla hiyo ilifanyika makao makuu ya kampuni hiyo mwishoni mwa wiki. Shindano hilo linaendeshwa na kampuni hiyo.

Meneja Uhusiano wa Nje wa Vodacom Tanzania Abigail Ambweni akiwaeleza jambo washindi wa kwanza wa shindano la AppStar wakati wa shughuli ya makabidhiano ya zawadi iliyofanyika makao makuu ya kampuni hiyo mwishoni mwa wiki. Katikati ni Roman Mbwasi mshindi wa kwanza wa shindano hilo katika tabaka la wabunifu waliobobea na kushoto ni George Machibya mshindi wa kwanza katika tabaka la wabunifu chipukizi wakisikiliza kwa makini.

Washindi  4 wa shindano la kubuni programu za simu lililoandaliwa na kampuni ya mawasiliano ya Vodacom  Tanzania lijulikanalo kama AppStar leo wamekabidhiwa zawadi zao ikiwa ni fedha taslimu na washindi wawili kati yao watashiriki katika kinyang’anyiro cha shindano hilo ngazi ya kimataifa litakalofanyika Bangalore nchini India  Januari 15,2015.

Waliokabidhiwa zawadi ni Roman Mbwasi  ambaye  amejinyakulia shilingi milioni mbili na atagharimiwa safari ya kwenda nchini India kushiriki shindano hili ngazi ya kimataifa akiwa ni mshindi wa kwanza katika kundi la wabunifu wakongwe na Athumani Mahiza alinyakua shilingi milioni moja; yeye ni mshindi wa pili.

Katika kundi la wabunifu chipukizi George Machibya ndiye mshindi wa kwanza aliyejinyakulia shilingi milioni moja na atagharimiwa safari ya kushiriki katika ngazi ya kimataifa nchini India na Ilakoze Jumanne amefanikiwa kujinyakulia shilingi laki tano akiwa ni mshindi wa pili.

Akiongea wakati wa hafla ya kukabidhi zawadi hizo,Meneja wa Uhusiano wa Masuala ya Nje wa Vodacom Abigail Ambweni alisema Vodacom  inawapongeza washindi na wote waliojitokeza kushiriki katika shindano hili muhimu linalolenga kuibua  na kukuza vipaji vya Watanzania.

“Tukiwa tunaongoza katika kutoa huduma za mawasiliano kwa njia ya teknolojia, Vodacom ina jukumu la kukuza sekta hii na kuibua vipaji vya matumizi ya teknolojia ili ziwepo programu mbalimbali za kurahisisha maisha kwa watumiaji wa simu. Tutazidi kuboresha shindano hili siku za usoni ili liweze kuhusisha Watanzania wengi hususani vijana waliopo vyuoni na nia yetu ni kukuza ubunifu wa kiteknolojia hapa nchini,” alisema Ambweni.

Nao washindi wa shindano  hilo walishukuru Vodacom kwa kuwazawadia na  kuandaa shindano hili kwa kuwa linawawezesha Watanzania kuchemsha bongo zao kubuni programu zenye kuleta suluhisho katika kupambana na changamoto mbalimbali na kurahisisha maisha.

Roman Mbwasi amesema kuwa shindano hili linasaidia kuwafanya watanzania wawe wabunifu na aliongeza kuwa ana uhakika atafanya vizuri katika ngazi ya kimataifa kupitia program yake aliyoibuni ya upashanaji wa taarifa za barabarani.

Naye George Machibya alisema kuwa wakati umefika kwa Watanzania kuchangamkia fursa kama hizi kwa kuwa nchi bado inahitaji kuwa na wabunifu wa program mbalimbali za kurahisisha maisha badala ya kutegemea program za nje ambako mazingira ya kule na ya kwetu ni tofauti. “Nina uhakika wazo la program yangu ya Soko Huru litafanya vizuri katika ngazi ya kimataifa na fursa hii imenifanya nizidi kujiamini zaidi,” alisema.

Mshindi atakayepatikana  katika kinyang’iro cha awamu ya pili atashiriki katika Mkutano Mkuu wa Kimataifa  wa Mitandao ya Simu za Mkononi utakaofanyika Barcelona nchini Hispania. Mashindano ya mwaka huu yanawashirikisha washiriki kutoka nchi za Afrika ya Kusini, Misri Tanzania, Kenya, Ghana na India.

No comments: