Thursday, November 27, 2014

MAADIMISHO YA SIKU YA TAKWIMU AFRIKA YAFANYIKA JIJINI DAR ES SALAAM, SERIKALI YASISITIZA UWAZI KATIKA TAKWIMU

Waziri wa Fedha wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar Omar Yussuf Mzee akifungua maadhimisho ya Siku ya Takwimu Afrika yaliyofanyika leo jijini Dar es salaam” na kuwashirikisha wadau mbalimbali kutoka ndani na nje ya nchi chini ya kauli mbiu isemayo “ Takwimu Huria kwa uwajibikaji na ushirikishwaji wa wadau wote.
Mkurugenzi wa Shughuli za Kitakwimu wa Ofisi ya Taifa ya Takwimu Bi. Aldegunda Kombo akizungumza kwa niaba ya Mkurugenzi Mkuu wa Ofisi hiyo kuhusu matumizi ya takwimu sahihi katika kupanga shughuli za maendeleo nchini wakati wa maadhimisho ya Siku ya Takwimu Afrika yaliyofanyika leo jijini Dar es salaam.
Mtakwimu Mkuu wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar Bw. Mohammed Hafidh akisisitiza jambo kuhusu athari, madhara na ya matumizi ya takwimu zisizo sahihi.
Baadhi ya wadau mbalimbali na wataalam wa takwimu waliohudhuria maadhimisho ya Siku ya Takwimu Afrika wakifuatilia masuala mbalimbali leo jijini Dar es salaam.
Mwakilishi kutoka nchi washirika wa maendeleo Bw. Jacques Morisset (kushoto) akizungumza na wadau mbalimbali kuhusu mchango wa matumizi ya takwimu sahihi katika maendeleo ya taifa lolote wakati wa maadhimisho ya Siku ya Takwimu Afrika leo jijini Dar es salaam.
Msanii Stara Thomas (kulia) akiwa na waimbaji wenzake akiwasilisha ujumbe wa matumizi ya takwimu sahihi kupitia wimbo maalum wakati wa maadhimisho ya Siku ya Takwimu Afrika yaliyowashirikisha wadau mbalimbali kutoka ndani na nje ya nchi chini.
Waziri wa Ferdha wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar Omar Yussuf Mzee (wa nne kutoka kulia mbele) akiwa katika picha ya pamoja na watendaji na watumishi wa Ofisi ya Taifa ya Takwimu mara baada ya kufungua maadhimisho ya Siku ya Takwimu Afrika leo jijini Dar es salaam.Picha na Aron Msigwa – MAELEZO.

No comments: