Thursday, October 30, 2014

Uelewa juu ya Brand na Product / Huduma na tofauti zake


Katika ulimwengu wa kijasirimali, tumekuwa tukishuhudia biashara zinazoanzishwa kila kukicha, na moja ya malengo makuu ya biashara yoyote ni kuhakikisha inafanikiwa na kupokelewa vyema na watumiaji.Na mapokeleo haya ndiyo yatakayokujenga au kukubomoa,na mapokeo hayo ndiyo yanayotengeneza brandi ya huduma au bidhaa yako.
Biashara nyingi huwa na majina kama ni njia mojawapo wa kujitambulisha au kujitofutisha na wengine wanaotoa / uza huduma au bidhaa inayofanana.
Kitu unachotakiwa kufahamu ni kuwa, bidhaa / huduma inapokuwa maarufu, inaweza kutengeneza brandi moja kwa moja, na brandi inaweza kutumika kama jina la bidhaa ila kuna utofauti kati ya brandi na huduma. Mfano, bia ya kilimanjaro (brand), watu wengi wakienda madukani husema nipe kilimanjaro ya baridi (wakimaanisha bia ya kilimanjaro),ili kuondoa mkanganyiko, hebu tuangalie tofauti kati ya bidhaa / huduma na brandi.


Makampuni yanatengeneza / toa bidhaa/huduma, wateja wanatengeneza brandi

Makampuni yanatengeneza bidhaa au kutoa huduma zenye majina ambazo hununuliwa na wateja, ila brandi huja kutokana na muono, matarajio na hata uzoefu wa wateja.
Mfano, bidhaa za Toyota ni magari, brandi kuu wanayotumia ni Toyota, na kwenye kila bidhaa zao huwa na brandi nyingine zinazotofautiana kulingana na mifumo yake, mfano Toyota Hiece, Toyota Prado nk, hivyo Prado ni brandi ndogo ya brandi kubwa Toyota. Toyota wanatengeneza magari ila Prado ni gari la toyota leye sifa fulanifulani kulingana na uzoefu wa wateja. Uzoefu huu unaotengenezwa na watumiaji ni lazima utoke kwa muuzaji bidhaa (Nini cha kipekee kwenye bidhaa / huduma yako? , nini unataka wateja wakipate kwenye bidhaa / huduma?). Kumbuka, wateja hawanunui bidhaa, bali kitokanacho na bidhaa na hiki ndicho kitatengeneza brandi yako.Hivyo ni lazima ukidhi matakwa / mategemeo ya wateja toka kwako.


Bidhaa zinaweza kubadilishwa na kukopiwa ila brandi lazima iwe ya kipekee.

Chukuli mfano,kampuni ya Bonite ilipotengeneza maji ya chupa na kuyapa jina la Kilimanjaro ambalo baadaye likaja kuwa brandi, baada ya muda kampuni ya Azam nayo ikaja na maji ya chupa wakayaita Uhai. Hivyo Azam hawakuziwa kutengeneza maji ya chupa ila haiwezekani kuja na maji ya chupa wakayaita Kilimanjaro kwakuwa Bonite tayari wanayo maji ya chupa yenye brandi ya Kilimanjaro.(Ila, kumbuka, ili uwe na haki ya watu wengine kutotumia jina la brandi yako kisheria, unatakiwa kuisajili umiliki wake (Copyright) kwenye idara husika, kwa Tanznia brela ndiyo wanahusika na hili).
Kwenye mfano huu, Brandi ya Kilimanjaro inampa mtumiaji matarajio ya kipekee, pia baada ya kuyatumia kwa muda anapata uzoefu nayo na kuyaweka kwenye kundi fulani. Hivyo kwa kila mteja, uzoefu toka brandi moja ni tofauti kabisa na ule wa brandi nyingine ingawa zote ni bidhaa sawa (kwenye mfano wetu, ni maji ya chupa).
Na hizi brandi hujumuishwa na vitu vingine vingi kama gharama, aina ya watu wanayoitumia, mahali zinapouzwa nk. Hivyo jikite kuhakikisha brandi yako kweli ina upekee.

Kutengeneza bidhaa na kukubalika / tumika ni kitendo cha haraka, lakini kutengeneza brandi inatumia muda

Chukulia mfano Google walipokuja na mtambo wa utafutaji (Search Engine) watumiaji waliutumia, ila mtambo huo (product) haukuwa na maana kwa wateja mpaka walipoutumia na kuona fauida zake na kuanza kuuona ni sehemu yao (brand). Na wakaanza kusema, brandi ya google inawawezesha kutafuta na kupata taarifa haraka online.
Na ndiyo maana, leo hii Google wakitoa huduma yoyote mpya, hutumia muda mfupi sana watu kuikubalikwakuwa watu wanaamini brandi kuu ya Google kama si longolongo.
Ndiyo maana kuna watu, wao ukiongelea magari, ni magari ya Toyota, hata kama ana pesa kiasi gani, huwezi kumuhamisha, na kuna wa Benzi, kuna wa Nissan nk, kutegemeana na uzoefu wao juu ya bidhaa.Hivyo, wateja hawa wanakuwa wamejenga uaminifu na brandi na siyo bidhaa.
Vitu vya muhimu kuzingatia ni kuwa, bidhaa / huduma zaidi ya moja inaweza kuwakilishwa na brandi moja, mfano ndani ya brandi ya Dudumizi, kuna huduma nyingi ndani yake kama kutengeneza websitekutengeneza systems nk, pia inawezekana brandi moja ikawa na brandi nyingine nyingi ndogondogo ndani yake, mfano, brandi ya toyota, ndani yake kuna brandi za Prado, Marino nk. Hapo utagundua, Huduma ya magari inawasilishwa na brandi ya Toyota, halafu kwakuwa kila gari lina uzoefu na utofuti wake, basi linawakilishwa na brandi tofauti.

Ni dhahiri makala hii itakuwa imefungua maswali mengi sana juu ya brandi, tembelea kurasa yetu ya Facebook hapa kwa maoni zaidi. Na tuonane kwenye makala ijayo juu ya jinsi ya kutengeneza brandi ya huduma / bidhaa yako.

No comments: