UTANGULIZI
1.
Uteuzi wa Wajumbe wa
Bunge la Katiba Unatawaliwa na Sheria ya Mabadiliko ya Katiba, Sura, 83 (The Constitutional Review Act, Cap 83).
Sheria hii inaweka mamlaka ya uteuzi, masharti, taratibu, vigezo na mambo
mengine yote yanayopaswa kuzingatiwa katika uteuzi wa Wajumbe wa Bunge la
Katiba. Kwa mujibu wa Kifungu cha 22 (2A) na (2B) vigezo hivi vinajumuisha
umri, jinsia, uzoefu, sifa na mahali anapotoka mjumbe husika.
2.
Sheria hii inatamka
aina tatu za Wajumbe wa Bunge la Katiba kama
ifuatavyo:-
(i)
Wabunge wote wa Bunge la Jamhuri ya Muungano;
(ii)
Wajumbe wa Baraza la Wawakilishi la Zanzibar; na
(iii)
Wajumbe 201 kwa mujibu wa Kifungu Na. 22(1c) cha Sheria ya Mabadiliko
ya Katiba ambayo inaonyesha makundi mbalimbali 10 yanayohusika.
3.
Makundi hayo ni kama ifuatavyo:-
(i)
Taasisi zisizokuwa za
Kiserikali (20)
(ii)
Taasisi za Kidini
(20)
(iii)
Vyama vyote vya Siasa
vyenye Usajili wa Kudumu (42);
(iv)
Taasisi za Elimu (20);
(v)
Watu wenye Ulemavu
(20);
(vi)
Vyama vya Wafanyakazi
(19);
(vii)
Vyama
vinavyowakilisha Wafugaji (10);
(viii)
Vyama vinavyowakilisha
wavuvi (10);
(ix)
Vyama vya Wakulima
(20); na
(x)
Vikundi vya Watu
wenye Malengo yanayofanana (20).
4.
Mchakato wa uteuzi
ulianza kwa kutoa Tangazo la Mwaliko katika Gazeti la Serikali, Tangazo la Serikali Na 443 la tarehe 13
Desemba, 2013. Tangazo hilo
lilitolewa kwa lugha ya Kiswahili na Kiingereza ili kuyaalika makundi yaliyotajwa
kisheria kuwasilisha mapendekezo ya majina kwa ajili ya uteuzi katika Bunge laMaalum
la Katiba. Aidha, Tangazo hilo
la mwaliko lilitangazwa pia katika magazeti mbalimbali yanayosomwa hapa nchini.
Pamoja na mambo mengine Tangazo la Mwaliko lilitamka ukomo wa muda wa Taasisi
na Makundi kuwasilisha mapendekezo ya majina ya wajumbe kuwa ni tarehe
02/01/2014.
5.
Mapendekezo hayo
yalitakiwa kuwasilishwa kwa Katibu Mkuu Kiongozi wa Serikali ya Jamhuri ya
Muungano wa Tanzania kwa upande wa Tanzania Bara na kwa upande wa Zanzibar,
mapendekezo yalitakiwa kuwasilishwa kwa Katibu Mkuu Kiongozi wa Serikali ya
Mapinduzi Zanzibar.
6.
Kufuatia mwaliko huo,
taasisi 554 kutoka Tanzania Bara na 178
kutoka Zanzibar ziliwasilisha mapendekezo yao . Mapendekezo hayo
yalijumuisha majina 2,762 kwa upande
wa Tanzania Bara na kwa upande wa Zanzibar
mapendekezo hayo yalihusisha watu 874.
Hivyo basi, taasisi na makundi mbalimbali yalipendekeza jumla ya majina 3,636. Lakini, na kinyume na Sheria,
watu 118 walijipendekeza wenyewe na
kufanya idadi ya majina yaliyopendekezwa kuwa 3,754.
7.
Mchanganuo wa idadi
ya watu walipendekezwa katika makundi mbalimbali ni kama
ifuatavyo:
Na.
|
Kundi/Taasisi
|
Taasisi zilizoleta mapendekezo
|
Idadi ya Watu
Waliopendekezwa
|
Idadi ya Wajumbe
Wanaotakiwa
|
Idadi ya Walioteuliwa
|
|||
|
|
|
|
|
|
|||
1.
|
Taasisi zisizokuwa za
Kiserikali
|
246
|
98
|
1,203
|
444
|
20
|
13
|
7
|
2.
|
Taasisi za Kidini
|
55
|
17
|
344
|
85
|
20
|
13
|
7
|
3.
|
Vyama vya Siasa vyenye Usajili
wa Kudumu
|
21
|
14
|
129
|
69
|
42
|
28
|
14
|
4.
|
Taasisi za Elimu
|
9
|
9
|
84
|
46
|
20
|
13
|
7
|
5.
|
Makundi ya Walemavu
|
24
|
6
|
97
|
43
|
20
|
13
|
7
|
6.
|
Vyama vya Wafanyakazi
|
20
|
1
|
89
|
13
|
19
|
13
|
6
|
7.
|
Vyama Vinavyowakilisha Wafugaji
|
8
|
1
|
43
|
4
|
10
|
7
|
3
|
8.
|
Vyama vinavyowakilisha Wavuvi
|
7
|
3
|
45
|
12
|
10
|
7
|
3
|
9.
|
Vyama vya Wakulima
|
22
|
8
|
115
|
44
|
20
|
13
|
7
|
10.
|
Makundi yenye Malengo
Yanayofanana
|
142
|
21
|
613
|
114
|
20
|
14
|
6
|
|
Mapendekezo Binafsi
|
-
|
-
|
118
|
-
|
|
|
|
|
Jumla
|
672
|
178
|
2,880
|
874
|
201
|
134
|
67
|
|
Jumla
Kuu
|
850
|
3,754
|
|
|
|
8.
Sheria ya Mabadiliko
ya Katiba imeweka masharti ya kuzingatiwa katika uteuzi wa wajumbe 201 wa Bunge la Maalum la Katiba.
Masharti hayo ni pamoja na wajumbe wasiopungua theluthi moja wanatakiwa kutoka Zanzibar
na theluthi mbili kutoka Tanzania Bara. Kwa sababu hiyo, katika wajumbe
201, wajumbe 67 watatoka Zanzibar
na wajumbe 134 watatoka Tanzania
Bara. Aidha, mgawanyo wa wajumbe wanawake na wanaume unatakiwa uwe nusu kwa nusu. Pamoja na hayo, wajumbe
hao wawakilishe sura ya wananchi wa Tanzania kwa ufuasi wa vyama vya
siasa, dini, umri, na maeneo wanayotoka. Katika mazingira haya, zoezi la kupata
wajumbe 201 halikuwa rahisi hata
kidogo. Mwitikio wa makundi ulikuwa mkubwa sana ikilinganishwa na nafasi zilizopo.
9.
Kama
nilivyoeleza hapo awali, mapendekezo kutoka Tanzania Bara yalikuwa 2,880 wakati nafasi za wajumbe ni 134. Kwa upande wa Zanzibar , majina yaliyopendekezwa yalikuwa 874 ikilinganishwa na idadi ya wajumbe 67 wanaotakiwa kuteuliwa. Kwa nyongeza
ya maelezo kuhusu uwingi wa mapendekezo, ni kwamba ukichukua taasisi zisizo za
kiserikali kwa upande wa Tanzania Bara walipendekezwa watu 1,203, wakati nafasi zilizokuwa zinatakiwa kujazwa ni 13 tu. Kwa upande Zanzibar , taasisi zisizokuwa za kiserikali
zilikuwa zimependekeza majina 444 ikilinganishwa na nafasi 7 tu zilizokuwa zinatakiwa kujazwa kutokana na taasisi hizi.
WAJUMBE WA BUNGE LA KATIBA
10.
Rais wa Jamhuri wa
Muungano wa Tanzania
wakishirikiana na Rais wa Zanzibar
na Mwenyekiti wa Baraza la Mpainduzi Zanzibar wamekamilisha uteuzi wa wajumbe 201. Kabla ya kutaja orodha ya wajumbe
walioteuliwa, napenda kufafanua mambo yafuatayo:
(a)
Uteuzi umezingatia
ushiriki wa watu wa rika zote, yaani vijana,
watu wazima na wazee. Kwa ajili hiyo, wajumbe vijana yaani wenye umri wa kati
miaka 22-35, ni wajumbe 35. Wajumbe wenye umri wa kati, yaani
miaka 36-64, ni 145; na wajumbe wazee, yaani wenye umri wa miaka 65 na kuendelea ni 21.
(b)
Sheria inataka kuwepo
na uwiano sawa kwa ajumbe wanawake na wanaume. Jambo hili limezingatiwa
ipasavyo, na katika orodha hii wajumbe wanawake ni 100 na wanaume 101. Kwa
vile, haiwezekani kuwa na nusu mtu, ndiyo maana idadi ya wajumbe wanaume ni 101.
(c)
Uwakilishi wa vyama
vya siasa ambao unahitaji kila chama chenye usajili wa kudumu kiwe na wajumbe
wawili umezingatiwa. Kwa kuwa kuna vyama vya siasa vyenye usajili wa kudumu 21,
jumla ya wajumbe 42 wamechaguliwa kwa maana ya kuwa wajumbe wawili wameteuliwa
kutoka katika kila chama.
Baada
ya maelezo hayo ya utangulizi, ifuatayo ndiyo orodha ya wajumbe 201 wa Bunge Maalum la Katiba
waliobahatika kuteuliwa:
TAASISI ZISIZOKUWA ZA
KISERIKALI- (WAJUMBE 20)
|
|
|
|
1.
Magdalena
Rwebangira
|
2.
Kingunge
Ngombale Mwiru
|
3. Asha
D. Mtwangi
|
4.
Maria Sarungi
Tsehai
|
5. Paul
Kimiti
|
6.
Valerie N. Msoka
|
7. Fortunate
Moses Kabeja
|
8.
Sixtus Raphael Mapunda
|
9. Elizabeth
Maro Minde
|
10. Happiness
Samson Sengi
|
11. Evod
Herman Mmanda
|
12. Godfrey
Simbeye
|
13. Mary
Paul Daffa
|
|
|
|
1.
Idrissa Kitwana Mustafa
|
2.
Siti Abbas Ali
|
3.
Abdalla Abass Omar
|
4.
Salama Aboud Talib
|
5.
Juma Bakari Alawi
|
6.
Salma Hamoud Said
|
7.
Adila Hilali Vuai
|
|
|
|
TAASISI ZA
KIDINI- (WAJUMBE 20)
|
|
|
|
1.
Tamrina Manzi
|
2.
Olive Damian Luwena
|
3.
Shamim Khan
|
4.
Mchg. Ernest Kadiva
|
5.
Sheikh Hamid Masoud Jongo
|
6.
Askofu Mkuu (Mstaafu) Donald Leo
Mtetemela
|
7.
|
8.
Hamisi Ally Togwa
|
9.
Askofu Amos J. Muhagachi
|
10.
Easter Msambazi
|
11.
Mussa Yusuf Kundecha
|
12.
Respa Adam Miguma
|
13.
Prof. Costa Ricky Mahalu
|
|
|
|
1.
Sheikh Thabit Nouman Jongo
|
2.
Suzana Peter Kunambi
|
3.
Sheikh Nassoro Mohammed Ibrahimu
|
4.
Fatma Mohammed Hassan
|
5.
Louis Majaliwa
|
6.
Yasmin Yusufali E. H alloo
|
7.
Thuwein Issa Thuwein
|
|
|
|
VYAMA VYOTE VYA SIASA
VYENYE USAJILI WA KUDUMU – (WAJUMBE
42)
|
|
|
|
1.
Hashim Rungwe Spunda
|
2.
Thomas Magnus Mgoli
|
3.
Rashid Hashim Mtuta
|
4.
Shamsa Mwangunga
|
5.
Yusuf S. Manyanga
|
6.
Christopher Mtikila
|
7.
Bertha Ng’angompata
|
8.
Suzan Marwa
|
9.
Dominick Abraham Lyamchai
|
10.
Mbwana Salum Kibanda
|
11.
Peter Kuga Mziray
|
12.
Isaac Manjoba Cheyo
|
13.
Dr. Emmanuel John Makaidi
|
14.
Prof. Ibrahim Haruna Lipumba
|
15.
Modesta Kizito Ponera
|
16.
Prof. Abdallah Safari
|
17.
Salumu Seleman Ally
|
18.
James Kabalo Mapalala
|
19.
Mary Oswald Mpangala
|
20.
Mwaka Lameck Mgimwa
|
21.
Nancy S. Mrikaria
|
22.
Nakazael Lukio Tenga
|
23.
Fahmi Nasoro Dovutwa
|
24.
Costantine Benjamini Akitanda
|
25.
Mary Moses Daudi
|
26.
|
27.
John Dustan Lifa Chipaka
|
28.
Rashid Mohamed Ligania Rai
|
|
|
1.
Ally Omar Juma
|
2.
Vuai Ali Vuai
|
3.
Mwanaidi Othman Twahir
|
4.
Jamila Abeid Saleh
|
5.
Mwanamrisho Juma Ahmed
|
6.
Juma Hamis Faki
|
7.
Tatu Mabrouk Haji
|
8.
Fat –Hiya Zahran Salum
|
9.
Hussein Juma
|
10.
Zeudi Mvano Abdullahi
|
11.
Juma Ally Khatibu
|
12.
Haji Ambar Khamis
|
13.
Khadija Abdallah Ahmed
|
14.
Rashid Yussuf Mchenga
|
TAASISI ZA ELIMU- (WAJUMBE 20)
|
|
|
|
1.
Dr. Suzan Kolimba
|
2. Prof.
Esther Daniel Mwaikambo
|
3.
Dr. Natujwa Mvungi
|
4. Prof.
Romuald Haule
|
5.
Dr. Domitila A.R. Bashemera
|
6. Dr.
Jasmine Bendantunguka Tiisekwa
|
7.
Prof. Bernadeta Kilian
|
8. Teddy
Ladislaus Patrick
|
9.
Dr. Francis Michael
|
10. Prof.
Remmy J. Assey
|
11.
Dr. Tulia Ackson
|
12.
Dr. Ave Maria Emilius Semakafu
|
13.
Hamza Mustafa Njozi
|
|
|
|
1.
Makame Omar Makame
|
2.
Fatma Hamid Saleh
|
3.
Dr. Aley Soud Nassor
|
4.
Layla Ali Salum
|
5.
Dkt. Mwinyi Talib Haji
|
6.
Zeyana Mohamed Haji
|
7.
Ali Ahmed Uki
|
|
|
|
WATU WENYE ULEMAVU-(WAJUMBE 20)
|
|
|
|
1.
Zuhura Musa Lusonge
|
2.
Frederick Msigala
|
3.
Amon Anastaz Mpanju
|
4.
Bure Zahran
|
5.
Edith Aron Dosha
|
6.
Vincent Venance Mzena
|
7.
Shida Salum Mohamed
|
8.
Dr. Henry Mwizengwa Nyamubi.
|
9.
Elias Msiba Masamaki
|
10.
Faustina Jonathan Urassa
|
11.
Doroth Stephano Malelela
|
12.
John Josephat Ndumbaro
|
13.
Ernest Njama Kimaya
|
|
|
|
1.
Haidar Hashim Madeweyya
|
2.
Alli Omar Makame
|
3.
Adil Mohammed Ali
|
4.
Mwandawa Khamis Mohammed
|
5.
Salim Abdalla Salim
|
6.
Salma Haji Saadat
|
7.
Mwantatu Mbarak Khamis
|
|
VYAMA VYA WAFANYAKAZI-(WAJUMBE 19)
|
|
|
|
1. Honorata
Chitanda
|
2.
Dr. Angelika Semike
|
3. Ezekiah
Tom Oluoch
|
4.
Adelgunda Michael Mgaya
|
5.
Dotto M. Biteko
|
6.
Mary Gaspar Makondo
|
7.
Halfani Shabani Muhogo
|
8.
Yusufu Omari Singo
|
9.
Joyce Mwasha
|
10.
Amina Mweta
|
11.
Mbaraka Hussein Igangula
|
12.
Aina Shadrack Massawe
|
13.
Lucas Charles Malunde
|
|
|
|
1.
Khamis Mwinyi Mohamed
|
2. Jina
Hassan Silima
|
3.
Makame Launi Makame
|
4. Asmahany
Juma Ali
|
5.
Mwatoum Khamis Othman
|
6. Rihi
Haji Ali
|
|
|
VYAMA VINAVYOWAKILISHAWAFUGAJI-(WAJUMBE
10)
|
|
|
|
1.
William Tate Olenasha
|
2.
Makeresia Pawa
|
3.
Mabagda Gesura Mwataghu
|
4.
Doreen Maro
|
5.
Magret Nyaga
|
6. Hamis
Mnondwa
|
7.
Ester Milimba Juma
|
|
|
|
1. Said
Abdalla Bakari
|
2. Mashavu
Yahya
|
3. Zubeir
Sufiani Mkanga
|
|
|
|
VYAMA VINAVYOWAKILISHAWAVUVI
–(WAJUMBE 10)
|
|
|
|
1.
Hawa A. Mchafu
|
2.
Rebecca Masato
|
3.
Thomas Juma Minyaro
|
4.
Timtoza Bagambise
|
5.
Tedy Malulu
|
6.
Rebecca Bugingo
|
7. Omary
S. Husseni
|
|
|
|
1.
Waziri Rajab
|
2.
Issa Ameir Suleiman
|
3.
Mohamed Abdallah Ahmed
|
|
VYAMA VYAWAKULIMA-(WAJUMBE 20)
|
|
|
|
1. Agatha Harun Senyagwa
|
2. Veronica
Sophu
|
3. Shaban
Suleman Muyombo
|
4. Catherine
Gabriel Sisuti
|
5.
Hamisi Hassani Dambaya
|
6.
Suzy Samson Laizer
|
7. Dr.
Maselle Zingura Maziku
|
8. Abdallah
Mashausi
|
9. Hadijah
Milawo Kondo
|
10.
Rehema Madusa
|
11.
Reuben R. Matango
|
12.
Happy Suma
|
13.
Zainab Bakari Dihenga
|
|
|
|
1.
Saleh Moh’d Saleh
|
2.
Biubwa Yahya Othman
|
3. Khamis
Mohammed Salum
|
4. Khadija
Nassor Abdi
|
5. Fatma
Haji Khamis
|
6. Asha
Makungu Othman
|
7.
Asya Filfil Thani
|
|
|
|
WATU
WENYE MALENGO YANAYOFANANA – (WAJUMBE 20)
|
|
|
|
1.
Dr. Christina Mnzava
|
2.
Paulo Christian Makonda
|
3.
Jesca Msambatavangu
|
4.
Julius Mtatiro
|
5.
Katherin Saruni
|
6.
Abdallah Majura Bulembo
|
7.
Hemedi Abdallah Panzi
|
8.
Dr. Zainab Amir Gama
|
9.
Hassan Mohamed Wakasuvi
|
10.
Paulynus Raymond Mtendah
|
11.
Almasi Athuman Maige
|
12.
Pamela Simon Massay
|
13.
Kajubi Diocres Mukajangwa
|
14.
Kadari Singo
|
|
|
1. Yussuf
Omar Chunda
|
2. Fatma
Mussa Juma
|
3. Prof.
Abdul Sheriff
|
4. Amina
Abdulkadir Ali
|
5. Shaka
Hamdu Shaka
|
6. Rehema
Said Shamte
|
Imetolewa
na:
Kurugenzi ya
Mawasiliano ya Rais,
Ikulu.
Dar es Salaam.
7
Februari, 2014
Tunawaombea Mwenyezi Mungu awape akili na hekima ili tupate katiba itakayotoa fursa kwa kila mtoto wa nchi hii leo na kesho
ReplyDeleteBonny Ndengo, Musoma
Kazi haikuwa ndogo kuwapata wajumbe wa bunge la katiba. Pongezi kwa Mh Rais na wasaidizi wako wote. Tunawaombea wakafanye maamuzi sahihi katika mchakato mzima wa kujadili na atimae tupate katiba iliyo bora yenye misingi ya usawa na haki kwa kila MTZ. Mungu ibariki Tanzania.
ReplyDeleteKwa Ndugu wa Ofisi ya Rais (uliyetumwa kuleta habari hii kwa vyombo vya habari na kuwafahamisha watanzania).
ReplyDeleteNext time mwambie bossy wako issue kama hii ni nyeti, tunaomba aifikishe mwenyewe.
Pili, kama haiwezekani kuwa uwiano sawa wa wanawake 101 na wanaume 101 basi, waongeze huyo mtu mmoja awe mwanamke na atoke kwenye kndi lilosahahulika kabisa
Tatu, kuna wanasiasa wazee na wazamani sana kwenye hii list na wengine walioshindwa ubunge huko nyuma au kuchoka wenyewe, kwa kweli inatia ulakini kwa kweli, yaani ni kwamba Tanzania inarudi nyuma au inakwenda mbele? Sisi wanyomnge tunasubiri mtuletee kwenye box la kura hiyo katiba, basi tutawashangaza.