Sunday, November 3, 2013

Matokeo ya Mtihani wa Darasa la Saba 2013




Imeelezwa kuwa ufaulu wa mtihani wa kumaliza darasa la
 saba kwa mwaka 2013 umepanda kwa masomo yote kwa asilimia 
19.89 ikilinganishwa na ilivyokuwa kwa mwaka uliopita.

Kwamba, wakati mwaka jana wahitimu waliopata asilimia 
100 walikuwa asilimia 30.72, mwaka huu wameongezeka kuwa 
asilimia 50.61. Pia, somo ambalo watahiniwa hao wamefaulu 
zaidi katika mtihani wao ni  Kiswahili ambapo ufaulu ni 
asilimia 69.06 huku wakiwa wamefeli zaidi kwenye somo la 
Hisabati ambalo ufaulu upo chini kwa asilimia 28.62.

Kaimu Katibu Mtendaji wa Baraza la Mitihani la Tanzania (NECTA), 
Dk. Charles Msonde alisema wanafunzi 427,606 
walifanya mtihani wa kumaliza elimu ya msingi mwaka 
2013 huku kiwango cha udanganyifu kikizidi kudhibitiwa 
hivyo kupungua.

Alisema NECTA imefuta matokeo yote ya mtihani wa kumaliza 
elimu ya msingi kwa watahiniwa 13, ambao walibainika 
kufanya udanganyifu kwenye mtihani au kurudia pasipo ruhusa 
ya Baraza. Watahiniwa waliofutiwa mwaka jana ni 293.

Alisema kati ya wanafunzi hao, 844,938 waliofanya mtihani 
huo wamepata alama zaidi ya 100 katika alama 250: 
“Idadi hiyo ni sawa na asilimia 50.61. Kati yao wasichana 
walikuwa 208,227 (sawa na asilimia 46.68) na wavulana 219,379 
sawa na asilimia 55.01,” alisema.

Dk. Msonde alisema katika ufanyaji wa mtihani huo, 
pia walikuwepo watu wenye ulemavu, ambapo wasichana 
walikuwa 219 na wavulana 257.

Alisema matokeo hayo yatapelekwa maeneo yote husika 
ili mchakato wa upangaji shule ukifanyika kwa watahiniwa 
wote waliofaulu mtihani huo wa kumaliza elimu ya msingi.

Kuhusu usahihishaji mitihani, Dk. Msonde alisema ili kujiridhisha
 na usahihi wa zoezi la usahihishaji wa kutumia mfumo wa kompyuta
 (Optical Mark Reader - OMR), sampuli za karatasi 20,795 za 
majibu ya watahiniwa wa shule 200 kutoka wilaya 48 
zilichukuliwa kutoka shule za mikoa tisa ya (Iringa, Kagera, 
Shinyanga, Manyara, Njombe, Mbeya, Morogoro, Katavi na Tanga) 
na kusahihishwa kwa mkono: “Ulinganifu baina ya alama 
za watahiniwa zilizopatikana kwa kusahihishwa kwa 
mkono na zile zilizotokana na usahihishaji wa mfumo wa 
kompyuta ulifanyika na kubaini kompyuta ilikuwa sahihi,”alisema.

Amesema makosa yaliyojitokeza katika karatasi zilizosahihishwa 
kwa mkono ni kuweka pata pale ambapo kuna kosa ama kuweka 
kosa pale ambapo kuna pata, makosa ambayo kwenye usahihishaji 
wa kutumia kompyuta hakuwepo.

Matokeo ya dalasa la saba yaliyopachikwa hapo juu pia 
yanapatikana katika tovuti za: 
1.     www.necta.go.tz
2.     www.edu.udsm.ac.tz

4.     www.moe.go.tz 

No comments: