Monday, July 8, 2013

USIKU WA SHEREHE YA MIAKA 3 YA VIJIMAMBO NA TAMASHA LA UTAMADUNI WA KISWAHILI MAREKANI WAFANA

Dj Luke akiambatana na mgeni wake Mhe. Ali Hassan Mwinyi kuelekea ukumbini kulikofanyika Tamasha la Utamaduni wa kiswahili na sherehe ya miaka 3 ya Vijimambo Jumamosi July 6, 2013 na kuwa tamasha la kihistoria lililohudhuriwa na Watanzania wakiwemo wadau wanaozungumuza Kiswahili wapatao 600 kutoka kila kona hapa Marekani, Ulaya na Tanzania.
Kutoka kushoto ni Dj Luke, Mhe, Ali Hassan Mwinyi, Mhe. Ramadhan Muombwa Mwinyi, Mama Lily Munanka, Idd Sandaly na Baraka Daudi katika picha ya pamoja wakati wakiingia ukumbini.
Watoto wa darasa la Kiswahili DMV wakiimba wimbo wa Taifa.
Mwenyekiti wa kamati ya maandalizi akiongea machache kabla ya kumkaribisha Dj Luke.
Dj Luke akisoma hotuba yake kabla ya kumkaribisha Kaimu Balozi wa Tanzania nchini Marekani, Mama Lily Munanka.
Kaimu Balozi Mama Lily Munanka akishukuru kamati ya maandalizi na kumkaribisha mgeni rasmi Rais Mstaafu Ali Hassan Mwinyi.
Rais Mstaafu Ali Hassan Mwinyi akihutubia mamia ya Watanzania waliofika kwenye Tamasha la Utamaduni wa Kiswahili na sherehe ya miaka 3 ya Vijimambo na kulifungua rasmi.
Mwenyekiti wa Jumuiya ya Watanzania New York, Bwn. Haji akisoma shairi alilotunga maalum kwa ajili ya sherehe ya miaka 3 ya Vijimambo na tamasha la Utamaduni wa kiswahili Marekani.
Shilole na Masanja mkandamizaji wakikandamiza na kugaragaza kwenye Tamasha la Utamaduni wa Kiswahili na miaka 3 ya sherehe ya Vijimambo.
Shilole(mwenye gauni la punda milia) akimnyanyua Afisa Ubalozi Mindi Kasiga kwenye moja ya nyimbo zake alizotumbuiza kwenye tamasha hilo.
Mhe. Ali Hassan Mwnyi akiaga na kuelekea kwenye gari lililomleta tayari kwa kuondoka baada ya kumaliza sehemu ya kwanza ya tamasha hilo na sherehe ya miaka 3 ya Vijimambo.
Mhe. Ali Hassan Mwinyi akiwa tayari kuondoka.
kwa picha zaidi bofya read more.




Meza waliyokaa Kaimu Balozi Mama Lily Munanka baadhi ya wageni walikuja na masafara wa Rais Mstaafu Ali Hassan Mwinyi wakibadilishana mawazo huku wakicheka kwenye usiku wa sherehe ya miaka 3 ya Vijimambo na tamasha la Kiswahili Marekani lilofanyika Jumamosi July 6, 2013.
Afisa Ubalozi Suleiman Saleh pamoja na mkewe (kushoto) katika picha ya pamoja na Tina Magembe.
Afisa Ubalozi wa Tanzania nchini Marekani na mkwewe katika pivha ya pamoja na Kulwa (kati) kutoka North Carolina aliyekuja kwenye sherehe ya miaka 3 ya Vijimambo na tamasha la utamaduni wa Kiswahili kama muakilishi wa DICOTA.
Shilole na Masanja wakipagawisha wadau wa Kiswahili kwenye sherehe ya miaka 3 ya Vijimambo na tamasha la Kiswahili Marekani.
Shilole akicheza na Salha kwenye moja ya nyimbo zake alizopagawisha kwenye sherehe ya miaka 3 ya Vijimambo iliyofanyika Jumamosi July 6, 2013.
Shilole akizidi kuwasha moto.
Ulikuwa ni usiku wa Vijimambo kuandika historia mpya.
Dj Luke (kushoto) katika picha ya pamoja na Afisa Ubalozi wa Tanzania nchini Marekani, Mindi Kasiga (kati) na mwenyekiti wa kamati Baraka Daudi.
Vijana na wadau wakubwa wa kiswahili wakipata picha ya pamoja.
Hamprey mdau wa Kiswahili toka North Carolina.
kwa picha zaidi bofya read more.




No comments: