Wednesday, May 2, 2012

matukio mbalimbali toka Songea leo

Afisa elimu wa mkoa wa Ruvuma Bi Paulina Mkonongo,akizungumza wakati wa mafunzo ya maboresho ya mitaala na mkakati  wa mafunzo kwa makatibu tawala wa wilaya na maofisa elimu wa mkoa huo yalifanyika katika ukumbi wa maliasili mjini songea leo kulia ni katibu tawala msaidizi wa mkoa huo Saveline Tosi.
Katibu tawala masaidizi wa mkoa wa Ruvuma Seveline Tosi akifungua mafunzo ya siku moja  ya tafakuri ya maboresho ya mitaala na mkakati wake kwa wadau wa elimu mkoani Ruvuma leo.

Wanafunzi wa shule ya msingi mfaranyaki manispaa ya songea, wakimsalimia mkuu wa mkoa wa Ruvuma Said Mwambungu,wakati wa sherehe za uwekaji jiwe la msingi jengo la mtandao wa polisi wanawake wilaya ya songea mkoani humo.
 

Mbunge wa jimbo la Peramiho Jenister Mhagama,akizungumza wakati wa uwekaji jiwe la msingi jengo la mtandao wa polisi wanawake wilaya ya songea mkoani Ruvuma leo.

Kamanda wa polisi wa mkoa wa Ruvuma Michael Kamuhanda (kushoto) akimuongoza mkuu wa mkoa wa Ruvuma Said Mwambungu katikati kwenda kuweka jiwe la msingi katika jengo la mtandao wa polisi wanawake wilayani songea,kulia mbunge wa jimbo la Peramiho Jenister Mhagama.
Mkuu wa mkoa wa Ruvuma Said Mwambungu akisalimana na maofisa wa jeshi la polisi mjkoani Ruvuma kabla ya kuweka jiwe la msingi jengo la mtandao wa polisi wanawake wilayani songea 
Mkuu wa mkoa wa Ruvuma Said Mwambungu,akizungumza wakati wa sherehe za kuweka jiwe la msingi katika jengo la mtandao wa polisi wanawake wa wilaya ya songea mkoani humo,kulia mbunge wa peramiho jenister mhagama na kushoto kamanda wa polisi mkoani humo  kamishina msaidizi mwandamizi Michael Kamuhanda.

Makatibu tawala wa wilaya za mkoa wa Ruvuma, mbinga,tunduru na namtumbo ambao majina yao hayakupatikana wakimsikiliza kaimu katibu tawala wa mkoa huo Seveline Tosi hayupo pichani, wakati wa mafunzo ya siku moja juu ya tafakuri ya maboresho ya mitaala na mkakati kwa wadau wa mkoa wa Ruvuma. Picha zote na Muhidin Amri

No comments: